- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akifafanua jambo wakati
akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), alipotembelea makao makuu
ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa
Shirika hilo Bw. Macrice Mbodo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa
Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Macrice Mbodo (kulia), akitoa maelezo kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu
huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika
la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (hayupo pichani), wakati alipozungumza nao
kuhusu changamoto zinazowakabili, jijini Dar es Salaam .
Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu akitoa ufafanuzi kwa Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, namna huduma za
vivuko zinavyotolewa kati ya Magogoni na kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa mifumo ya
TEHAMA, Peter Mungo, akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani namna mfumo huo unavyofanya kazi, wakati
alipofanya ukaguzi eneo la Magogoni kujionea utendaji kazi wa Vivuko vinavyotoa
huduma kati ya Magogoni na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (mwenye suti), pamoja na abiria
wengine wakishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. Kazi kinachotoa huduma kati ya
Magogoni na Kigamboni, wakati alipokagua kivuko hicho, jijini Dar es salaam.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Seriklaini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Shirika la
Posta Tanzania (TPC), limetakiwa kuangalia na kuona namna ya kuboresha
mishahara ambayo itatoa motisha kwa watumishi wake ili kufanikisha kutekeleza
majukumu yao na hatimae shirika kujiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa
Serikali.
Akizungumza na
uongozi pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesisitiza kuwa ipo haja kwa uongozi
wa shirika hilo kurekebisha mishahara ya watumishi wake kulingana na mazingira
ya sasa.
"Angalieni
namna ya kuboresha viwango vya mshahara angalau vikidhi matakwa ya wafanyakazi
hawa ambao wana hali mbaya ili nao waweze kujikimu kama watumishi wengine”,
amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Eng. Ngonyani,
amewataka watumishi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi, ujuzi na ufanisi
ili kuongeza uzalishaji wa shirika hilo na hatimae kukuza pato la Taifa.
Aidha, ameutaka
uongozi wa shirika hilo kuongeza na kupanua wigo wa kufikisha huduma za posta
kwa wateja wake hususan katika mikoa ya nyanda za juu kusini na mikoa ya Kanda
ya Ziwa kwani huduma hizo katika mikoa hiyo zimekuwa zikisuasua.
Naye, Kaimu
Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo, amemshukuru Naibu Waziri huyo kwa ujio wake
katika shirika hilo na kumuahidi kutekeleza maagizo yote ili kuleta tija kwa
shirika na kukuza pato la Taifa.
Ameongeza kuwa
Shirika liko kwenye hatua za mwisho za kuwekeana mikataba ya kibiashara na
taasisi za Serikali kama vile MSD, NIDA, TBS na nyinginezo ili kuhakikisha
inafikia wateja wote mahali popote nchini.
Katika hatua nyingine,
Naibu Waziri huyo ametembelea Ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),
pamoja na kukagua shughuli zinazoendelea katika karakana ya Magari ya Serikali (M.T.
Depot) iliyopo eneo la Kurasini na kusisitiza kuongeza wataalam wa ufundi hususan
mafundi mchundo na mafundi sanifu ili kutatua changamoto zinazokabili karakana
za Wakala huo mikoani.
Ameitaka TEMESA
kuboresha miundombinu ya vivuko katika visiwa vya Ukerewe na Ukara vilivyopo
mkoani Mwanza, ambapo changamoto za uharibifu na uchakavu wa vivuko hivyo
umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara.
Kwa upande
wake, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu, amebainisha baadhi ya miradi
ambayo inatarajiwa kutekelezwa na wakala wake kwa mwaka wa fedha 2017-2018
ikiwemo ununuzi wa kivuko kipya cha Kigongo - Busisi na ukarabati mkubwa wa
vivuko vya MV. Sengerema, MV. Misungwi, MV. Kigamboni na Boti ya MV. Kiu
ambapo lengo likiwa ni kuongeza na kurahisisha huduma za usafiri kwa watumiaji.
Naibu Waziri Ngonyani anaendelea na ziara ya kikazi jijini Dar es salaam ambapo jana ametembelea na kukagua utoaji huduma katika Shirika la Posta nchini na Wakala wa Umeme na Ufundi (TEMESA).
Naibu Waziri Ngonyani anaendelea na ziara ya kikazi jijini Dar es salaam ambapo jana ametembelea na kukagua utoaji huduma katika Shirika la Posta nchini na Wakala wa Umeme na Ufundi (TEMESA).
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Comments
Post a Comment