- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa
kampuni ya Hari Singh & Sons, Jaspal Singh (kushoto), wakati akikagua
maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye
urefu wa KM 2.6 kwa kiwango cha lami, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Hari
Singh & Sons, Jaspal Signh, akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa
barabara ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 kwa
kiwango cha lami, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa sehemu ya barabara
ya Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa KM 2.6 inayojengwa kwa
kiwango cha lami, ambapo ujenzi wake umefika asilimia 57.
Mhandisi wa miradi kutoka
Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Ngusa Julius, akimuonesha Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ramani ya Daraja
la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15 kila upande linalojengwa na Kampuni ya
Milembe & Kika JV eneo la Kawe, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa
Kampuni ya Milembe & Kika JV anayejenga Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa
mita 15 kila upande, lililoko barabara ya Mwai Kibaki, wakati akikagua ujenzi
wake, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa sehemu ya chini ya
ujenzi wa Daraja la Mlalakuwa lenye urefu wa mita 15 kila upande, lililoko
barabara ya Mwai Kibaki, jijini Dar es Salaam.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano,
Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROADS)
Serikali imetoa
siku 60 kwa mkandarasi wa Kampuni ya Hari Singh & Sons kumaliza ujenzi wa
kipande cha barabara cha kilomita 1.5 kilichobaki kwa kiwango cha lami katika
barabara ya Kimara Baruti-Msewe-Chuo Kikuu yenye jumla ya urefu wa kilomita 2.6.
Akitoa agizo
hilo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.
Edwin Ngonyani, amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anamaliza mradi huo
haraka na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba ili idumu kwa muda mrefu.
"Ikifika mwezi Oktoba nataka unikabidhi barabara hii ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami na vigezo vinavyokubalika, amesisitiza Eng. Ngonyani.
"Ikifika mwezi Oktoba nataka unikabidhi barabara hii ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami na vigezo vinavyokubalika, amesisitiza Eng. Ngonyani.
Aidha, Naibu
Waziri Ngonyani amefafanua kuwa mkandarasi huyo hatoruhusiwa kutekeleza mradi
mwingine wa barabara nchini endapo atashindwa kukamilisha ujenzi wa barabara
hiyo kwa wakati.
Kwa upande wake
Mhandisi Mradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Ngusa Julius,
amesema kuwa TANROADS tayari imeshatoa notisi kwa mkandarasi huyo kuwa kama
hatakamilisha kazi ya ujenzi ndani ya muda wa mkataba hatua za kudai fidia
kulingana na mkataba zitafuata na baadae kukatisha mkataba.
Ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unasimamiwa na TANROADS kupitia kitengo chake cha wahadisi washauri wazalendo (TECU) na unagharimu Shilingi bilioni 5.7 ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia mia moja.
Ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unasimamiwa na TANROADS kupitia kitengo chake cha wahadisi washauri wazalendo (TECU) na unagharimu Shilingi bilioni 5.7 ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia mia moja.
Katika hatua
nyingine, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amekagua daraja la Mlalakuwa lenye urefu
wa mita 15 kila upande, lililopo barabara ya Mwai Kibaki jijini Dar es salaam
na kusisitiza kwa mkandarasi Milembe & Kika JV kuhakikisha anamaliza ujenzi
wa daraja hilo kwa wakati.
Ujenzi wa
Daraja la Mlalakuwa unagharimu shilingi Bilioni 4.8 na unatarajiwa kukamilika
mwezi Oktoba mwakani.
Comments
Post a Comment