- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem.Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia moja ya dawa zilizopo kwenye beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem.Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi.
.....................................................................................
Balozi wa
Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 ambavyo
vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Makabidhiano
ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam ambapo Balozi wa
Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi hiyo imetoa vifaa
hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya
nchi hiyo na Tanzania.
Amesema kuwa
Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya kwanza na lengo ni
kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa wanawake
wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.
Mara baada
ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru
Serikali ya Kuwait kwa msaada huo ambao utasambazwa katika hospitali mbalimbali
kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema msaada huo utasaidia sana wanawake
wajawazito na waliojifungua kupata vifaa za uzazi ambavyo vinahitajika wakati wanamke
mjamzito anapojifungua na baada ya kujifungua.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitaanza kusambazwa
kuanzia mwezi huu na mchakato wa kuainishwa hospitali zitakazopata msaada huo
unaendelea.
Makamu wa
Rais pia amesisitiza kudumishwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi ya
Kuwait na Tanzania kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.
Aidha Balozi
huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa
Serakali ya Kuwait itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania katika uimarishaji
wa sekta ya afya na elimu nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora
na za msingi.
Comments
Post a Comment