- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na Naibu wake
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Bustani kilichoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma,
walipotembelea bungeni mjini Dodoma, siku ambayo Bunge limepitisha kwa kishindo
Bajeti ya Sh. trilioni 31.7 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James (wa
nne kulia-mbele), akiongoza Vongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango
kufuatilia tukio la Wabunge wakipiga kura kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya
shilingi trilioni 31.7, Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Chakwa-Zanzibar, Mhe. Bhagwanji Meisuria (katikati), na mkewe
Kissum Biin Bhagwanji Meisuria, wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya
Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7,
mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Charles Kitwanga akimkumbatia kwa furaha na bashasha
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwa kufanikisha
kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni
31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Mnauye akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa
kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018,
mjini Dodoma
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), akimpongeza
kwa furaha na bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali
ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini
Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiteta jambo na
maafisa waandamizi wa Wizara yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya
Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipongezwa na Askari
wastaafu wa Jeshi la KAR waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939-1945
baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi
trilioni 31.7, bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Dkt.
Ashatu Kijaji (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa
Wizara hiyo baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Shilingi
trilioni 31.7 mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akimshukuru na kumpongeza
Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kwa ushirikiano mkubwa aliompatia hadi
kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa na kusimamia Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi
trilioni 31.7 iliyopitishwa na Bunge kwa kishindo mjini Dodoma.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Comments
Post a Comment