- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Akazungumza na mhudumu kwa Kichina kibovu, halafu akachukua
ufunguo wa chumba cha Leila.
Wakati tukipita ukumbini, akasema, “Huyu kizee ni mpumbavu.
Tutalifunga hili danguro lake. Hataki kukiri kwamba alikuwa kahaba — siwezi
kumlaumu.”
Nikamchukia kwa sababu za kihisia. Leila, nilihisi, alistahili
jambo zuri kuliko kuitwa kahaba na polisi huyu wa Kiskochi.
MacPherson alifungua mlango wa chumba cha Leila na kuingia kwenye
chumba hicho kidogo. Nikabaki nje, nikichungulia ndani. Kwa ustadi mkubwa wa
kipelelezi, akaanza kupekua chumba. Kulikuwa na magauni matatu tu
yaliyotundikwa kwenye kabati na seti moja ya chupi kwenye saraka. Vitu vya Leila
vilikuwa vichache sana.
MacPherson alitoa mguno wa ghafla wakati alipochungulia chini ya
kabati.
“Nilifikiria zaidi . . .” akasema, akainama na kutoka na kutoa
kibunda kidogo. Akakitoa taratibu. Ilionekana kama kimetoka kwenye pakiti ya
sigara kumi.
“Unajua hii ni nini?” akauliza, akinionyesha. Katikati yake
kulikuwa na alama nyeusi ya moshi.
“Wewe uniambie,” nikasema.
Aliinama tena na kuchungulia kwenye kabati na safari hii akatoka
na mshumaa mdogo ulioungua nusu: ni aina ya mishumaa unayoiweka kwenye keki za
siku ya kuzaliwa.
Akaketi kwenye upande mmoja wa kitanda, akiwa amemshikilia
kitambaa na mshumaa na kukitanua.
“Alikuwa mtumiaji wa heroin,” akasema. “Watu zaidi ya kumi
wanaotumia dawa za kulevya hujiua kila wiki.”
“Nini kinachokufanya uwe na uhakika huo?” nikamuuliza.
“yeyote ambaye ana vitu hivi viwili ni mraibu wa dawa za kulevya,”
akasema MacPherson. “Unajua inafanyaje kazi? Wanaweka heroin kwenye kitambaa. Wanaweka
mshumaa mdogo chini ya kitambaa na kunusa moshi wake. Inafanyika kwa sekunde
chache. Unajua nini? Kitu cha kipumbavu ambacho Serikali ilifanya ni kutangaza
vita kwa watumiaji wa dawa za kulevya. Walidhani ndicho kitu rahisi zaidi
duniani kukifanya na kukizuia. Wavutaji wa dawa za kulevya lazima wawe na
chumba, kitanda na vifaa kama hivi vya kuvutia ambavyo ni ghali. Huwa hatuppati
shida kuvipata vyumba vyao na kuharibu vifaa vyao. Mtemba wa kuvutia dawa za
kulevya unagharimu fedha nyingi sana, na baada ya muda wavutaji wakachoshwa na
sisi kuvunja vitanda vyao na mitemba yao na kuwafukuza kwenye paa za nyumba. Tulijidanganya
kwamba tulikuwa tunafanikiwa katika vita hiyo ya dawa za kulevya, lakini sasa
kumbe tulikosea.” Akasogeza kofia yake nyumba ya kichwa chake wakati
akinitazama. “Watumiaji waligundua kwamba wanaweza kupata heroin kutokana na
opium na walichokuwa wanahitaji ni kipande cha kitambaa na mshumaa. Wanaweza kuvuta
sumu hii mahali popote: kwenye sinema, kwenye maeneo ya umma, kwenye treni,
mabasi, teksi – mahali popote. Kama utakkuwa unachunguza utashangaa kukuta
alama za mishumaa katika maeneo yasiyotarajiwa. Hiyo itakueleza, kama
tunavyoelewa sisi, kwamba kuna watu wamevuta heroin. Kuvuta opium ni uraibu,
lakini haiui. Lakini usije ukakosea: heroin inaua. Kama tungewaacha Wachina
wavute opium, tusingekuwa tunahangaika kupambana na wavutaji wa heroin.”
Nikakuna upande wa taya langu.
“Nashukuru wa darasa,” nikamwambia, “lakini sidhani kama amejiua
na sidhani kama alikuwa mtumwa wa dawa za kulevya. Nadhani ameuawa na hivi vitu
vimekuja kupandikizwa tu hapa ili uvione.”
Uso mkavu wa MacPherson haukuonyesha hali yoyote. Akachukua mtemba
wake na kuujaza tumbaku.
“Ndivyo unavyodhani?” akauliza, akiwa amekerwa. “Mkuu amesema wewe
ni kachero wa kujitegemea. Nimesoma kuhusu Chandler na Hammet — waliandika
riwaya. Hii inaonekana kuwa ni maisha halisi.”
“Ndivyo ilivyo,” nikamwambia. “Sawa, usijali. Sidhani kama ina
umuhimu sana.”
“Nini kinanchokufanya ufikirie kwamba ameuawa?” akauliza bila kuwa
na hamu yoyote.
“hakuna ambacho kinaweza kukushawishi. Utavifanyaje vitu vyake?”
“Nitavipeleka polisi. Pengine atatokea mtu akavidai. Huyo mzee
hapo mapokezi hajui kama alikuwa na ndugu yeyote. Nimewahi kuzungumza naye –
hajui chochote kuhusu chochote.” Akasimama. “Nashauri usimfikirie sana.” Akaweka
vitu vya Leila kwenye mkoba mdogo alioukuta juu ya kabati. “Kama ungekuwa
unashughulika na kesi nyingi kama sisi tunavyofanya, wala usingemfikiria
kabisa.”
“Nina uhakika. Hilo ndilo wazo lenyewe.”
Akanitazama kwa makini.
“Wazo gani?” akauliza.
“Watu waliomuua wasingependa wewe ufikirie mara mbili, au siyo?”
Akatabasamu.
“Oh, achana nalo. Tunakabiliana na mamia ya kesi hizi za kujiua. .
. .”
Alikuwa amenichosha.
“Nimekusikia tangu mwanzo.” Nikaelekea chumbani kwangu. “Nitakuwepo
hapa kwa siku chache kama utanihitaji.”
Akanichungulia, akiwa amepoteza kujiamini kwake.
“Nini kinachokufanya udhani kwamba nitakuhitaji?” akauliza.
“Sawa, tunaweza kusoma hadithi ya kachero pamoja,” nilisema na
kufunga mlango.
Itaendelea
kesho…
Comments
Post a Comment