- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Nikamtazama akikatiza kwenye chumba hicho na kwenda mahali simu
ilikokuwa kwenye baa. Wakati alipokuwa anapiga simu, mmoja wa mabaharia wa
Kimarekani akamwendea na kuweka mkono wake begani mwake. Akamwashiria anyamaze
ambapo Mmarekani huyo aligeuka kunitazama na kunipungia. Nami nikampungia. Mazingira
ya kwenye baa hii yalikuwa tulivu mno na rahisi. Hakukuwa na ugumu wowote
katika biashara hii niliyotaka kuifanya. Wakati mwanamke aliporudisha mkonga wa simu chini, kila mmoja, wakiwemo wahudumu, walijua nilikuwa
nimeagiza msichana na alikuwa njiani anakuja. Wote walionekana kufurahia tukio
hilo.
Mwanamke yule akazungumza na baharia na akanyanyua mkonga tena.
Biashara ilionekana kwenda vizuri.
Nilimaliza kinywaji changu, nikawasha sigara, halafu nikamuashiria
muhudumu aniletee kinywaji kingine.
Wamarekani wawili waliovalia mashati ya fujo, walikuja na kuketi
kwenye meza mbali kidogo na mimi. Baada ya mwanamke wa Kichina kumaliza kupiga
simu akanijia.
“Atawasili baada ya dakika kumi,” akasema. “Nitakueleza mara baada
ya kuwasili,” na baada ya kumwitikia, akawaendea Wamarekani wawili na kuketi
nao. Baada ya mazungumzo ya dakika tano akainuka na kwenda kupiga simu tena.
Takriban robo saa baadaye, mlango wa baa ukafunguliwa na binti wa
Kichina akaingia. Alikuwa mrefu na amejengeka vizuri. Alikuwa amevalia gauni la
Ki-Ulaya lililombana lenye rangi nyeusi na nyeupe. Mkoba wenye rangi nyeusi na
nyeupe ulining’inia kwenye mkanda ambao aliuzungusha kwenye mkono wake. Alikuwa
mzuri, mrembo na mwenye mvuto. Alimtazama mwanamke wa Kichina ambaye
alimuashiria kwangu. Binti huyo akanitazama na kutabasamu, halafu akakatisha
kwenye baa, akitembea kwa madoido huku baadhi ya mabaharia wa Kimarekani
wakimtazama, na kunionyesha ishara ya kukubali.
Akaketi pembeni yangu.
“Hello,” akasema. “Unaitwa nani?”
“Nelson,” nikamwambia. “Wewe unaitwa nani?”
“Jo-An.”
“Jo-An—nani?”
Akanyoosha mkono na kuchukua sigara katika paketi yangu iliyokuwa
mezani.
“Ni Jo-An tu.”
“Siyo Wing Cheung?”
Akanitazama ghafla na kutabasamu. Alikuwa na meno mazuri meupe.
“Hilo ni jina langu. Umejuaje?”
“Rafiki yangu alikuwa hapa mwaka jana,” nikamwambia, nikijua
kwamba alikuwa ananidanganya. “Aliniambia nikutafute nikija.”
“Nimefurahi sana.” Aliiweka sigara katikati ya midomo yake na
kuiwasha. “Unanipenda?”
“Tena sana.”
“Tunaweza kuondoka?”
“hakuna shida.”
“Unaweza kunipa denye dhahabu.
“Umeridhika naye?”
“Nani ambaye ahawezi kuridhika naye?”
Akachukua dola tatu.
“Njoo unitafute tena,” akasema. “Siku zote niko hapa.”
Binti aliyejiita mwenyewe Jo-An akasimama na kuelekea mlangoni.
Nikamfuata, nikiwapungia kwa kuwaaga mabaharia. Mmojawao akatengeneza herufi ‘O’
kwa vidole vyake gumba na shahada. Nikaachana nao na kutoka nje ambako binti
alikuwa ananisubiri.
“Ninaifahamu hoteli safi na nafuu,” akasema.
“Hata mimi naijua,” nikamwambia. “Nimefikia Celestial Empire. Tutakwenda
pale.”
“Itakuwa vyema twende kwenye hoteli yangu.” Akanitazama kwa
kijicho-pembe.
“Tutakwenda kwenye hoteli yangu,” nikasema, na kumkamata mkono,
nikamuongoza katika ya msongamano wa watu mtaani kuelekea hotelini.
Akatembea pembeni yangu. Alikuwa amejipulizia manukano aghali sana.
Sikujua ni aina gani, lakini yalikuwa mazuri. Uso wake ulionekana kuwa na
mawazo mengi mno. Hatukuzungumza chochote wakati tukitembea. Alipandisha ngazi
ndefu za hoteli. Umbile lake kwa nyuma lilivutia sana na miguu mizuri mirefu. Alitingisha
nyunga yake kitaalam wakati akipanda ngazi moja hadi nyingine. Nikajikuta
nimezama kuangalia mwendo wake kuliko hata hali iliyokuwepo mbele yangu.
Yule mzee wa mapokezi alikuwa anasinzia. Alifumbua jicho moja na
kumtazama msichana, halafu mimi, akafumba jicho tena.
Nikamuongoza kwenye korido. Leila alikuwa amesimama kwenye mlango
wa chumba chake uliokuwa wazi, akipaka rangi kucha zake. Alimtazama msichana na
kunikonyeza kwa dhihaka. Nami nikamkonyeza, nikafungua mlango na kumuongoza
msichana wangu kwenye chumba chenye joto.
Nilifunga mlango na kuweka komeo.
Akaniambia, “Unaweza kuniongeza zaidi ya dola thelathini? Nitakuwa
mzuri zaidi ukinipa hamsini.”
Akafungua zipu ya gauni lake kuonyesha umbile lake. Alikuwa
amefungua nusu ya gauni lake kabla sijamzuia.
“Subiri kwanza,” nikamwambia, nikichukua pochi yangu. “Hatupaswi
kuharakisha mambo katika hili.”
Akanitazama. Nikachukua picha ya marehemu Jo-An iliyopigwa akiwa
mochwari na kumpatia. Uso wake mwembamba, wa kuvutia ukaonyesha mashaka. Akaitazama
picha, halafu akanitazama.
“Hii ni nini?” akauliza.
“Picha ya Jo-An Wing Cheung,” nilisema, nikiketi kitandani.
Taratibu akaifunga zipu ya gauni lake. Uso wake sasa ukaonyesha
fadhaa.
“Ningejuaje kama ulikuwa na picha yake?” akasema. “Madame alisema
usingeweza kujua jinsi alivyo huyo msichana.”
“Ulikuwa unamfahamu?”
Akapandisha midomo yake hadi puani.
“Kwani yeye ni muhimu sana? Mimi ni mzuri kuliko yeye. Hupendi
kufanya mapenzi na mimi?”
“Nimekuuliza tu kama ulimfahamu.”
“Hapana. Sikumfahamu kabisa.” Akasogea pembeni kwa mashaka. “Ninaweza
kuchukua vitu vyangu?”
Nikahesabu noti tano za dola kumi kumi, nikazikunja na kuzishika
mkononi ili azione.
“Aliolewa na Mmarekani. Jina lake alikuwa Herman Jefferson,” nikamwambia.
“Ulikuwa unamfahamu huyo mwanamume?”
Akajifanya kama kukumbuka.
“Nilikutana naye.” Akaitazama tena picha ya Jo-Ann. “Kwanini
anaonekana hivi. . . anaonekana kana kwamba amekufa.”
“Ndivyo alivyo.”
Akaidondosha picha chini kama imemng’ata.
“Ni mkosi kutazama picha za watu waliokufa,” akasema. “Nipe vitu
vyangu. Nataka kuondoka.”
Nikachukua picha ya Herman Jefferson na kumuonyesha.
“Je, huyu ndiye mumewe?”
Hakuweza kuitazama vizuri picha hiyo.
“Nimekosea. Sijawahi kukutana na mumewe. Naomba vitu vyangu
niondoke.”
“Umesema uliwahi kukutana naye.”
“Nimekosea.”
Tukatazamana. Nikaona kwa kumwangalia tu kwamba nilikuwa napoteza
muda wangu. Hakuwa tayari kuniambia chochote. Nikampatia fedha ambazo aliziweka
kwenye mkoba wake.
“Kuna fedha nyingi zilikotoka hizo kama unaweza kunipatia taarifa
kuhusu Jefferson,” nikamwambia bila matumaini yoyote.
Akaelekea mlangoni.
“Sijui chochote kumhusu. Asante sana kwa kunipatia fedha.”
Akatoa komeo, akafungua mlango na kuondoka.
Nilijua alikuwa amedanganywa tu ili aje anidanganye, lakini kwa
vile nilikuwa natumia fedha za Jefferson, sikufikiria lolote kuliko kama
ningekuwa natumia fedha zangu mwenyewe.
Itaendelea
Jumatatu…
Comments
Post a Comment