- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mtu mnene, mwenye ndevu zilizoloa jasho na kichwa chenye
kipara, aliinuka na kuinama kwa mbele kuchungulia dirishani wakati bango la ‘No
Smoking’ lilipoonekana.
“Sawa, tumekwishaingia—Hong
Kong,” alisema akigeuka kwa begani kunitazama. “Inaonekana ni pazuri. Wanasema
hakuna mahali pazuri duniani kama hapa. Wanaweza wakawa sahihi.”
Wakati kichwa
chake kikubwa kilipokuwa kinanikinga, nilikuwa nahangaika kuufunga mkanda
wangu. Baadaye alipoketi na kuufunga mkanda wake, nikafanikiwa kuiona milima ya
kijani, bahari ya buluu iliyong’ara na boti kadhaa kabla ya ndege kutua kwenye
njia ya kurukia.
Mtu huyu mnene
ambaye alikuwa jirani yangu tangu tulipoondoka Honolulu, alisimama kuchukua
kamera yake na begi lenye nembo ya Pan-American Airways.
“Unafikia hoteli
ya Peninsula?” akaniuliza.
“Mimi niko
upande wa pili.” Nikamjibu.
Uso wake
ulionyesha kutoridhika.
“Kowloon ni
nzuri: maduka mazuri: hoteli nzuri, lakini pengine uko hapa kwa shughuli za
biashara?”
“Ni kweli kabisa,”
nilimjibu.
Jibu hilo
lilionekana kumfurahisha.
Abiria wengine
kwenye ndege wakaanza kuchukua mabegi yao. Pilika za daima za utulivu na
kusukumana zikaendelea kwa muda kabla ya mimi kupata nafasi kutoka nje kwenye
jua linaloangaza.
Ilikuwa safari
nzuri, kidogo ndefu, lakini niliifurahia. Dakika kumi baadaye, nilikuwa
nimepita kwenye forodha na kutoka nje kwenye kelele nyingi za uwanja wa ndege.
Nilimuona jirani yangu akichukuliwa na basi la hoteli. Alinipungia mkono name
nikampungia. Vijana kadhaa wa mikokoteni wakanizunguka, wakipiga kelele na
kuninyooshea mikono. Walikuwa na nyuso zilizozeeka pengine kutokana na hali ya
maisha. Wakati nikiwa nimesimama kwa kusita, Mchina mmoja mnene, mfupi,
aliyevalia nadhifu suti maridadi, akanijia na kuinama kidogo.
“Samahani,
tafadhali,” akasema. “Pegine naweza kukusaidia? Unahitaji teksi?”
“Nahitaji kufika
Celestial Empire Hotel huko Wanchai,” nikamwambia.
“Hiyo iko
kisiwani, mheshimiwa.” Alionekana kushangaa kwa namna ya ukarimu. “Itakuwa
vyema ukichukua teksi hadi Feri halafu uvuke kwenda Wanchai. Hoteli ipo karibu
na Feri kwa upande wa ng’ambo.”
“Asante sana,” Nikamwambia.
“Dereva wa teksi atakuwa anafahamu kuzungumza Kiingereza?”
“Wengi wao
wanafahamu Kiingereza kidogo.” Akamuashiria dereva wa teksi mmoja katika
maegesho. “Kama utaniruhusu. . .”
Akanitangulia
mbele. Nilibeba begi langu na kumfuata. Alizungumza na dereva kwa lugha ya Ki-
Cantonese. Dereva mwenyewe Mchina, mwembamba na mchafu, aliguna, akanitazama,
halafu akatazama pembeni.
“Atakupeleka
Feri, mheshimiwa,” Mchina mfupi akaniambia. “Nauli yake ni dola moja: siyo dola
ya Marekani, umeelewa, ni dola ya Hong Kong. Kama unavyofahamu, dola moja ya
Marekani ni sawa na sola sita za Hong Kong.” Akatabasamu. Kila jino mdomoni mwake
lilikuwa limepachikwa jino la dhahabu. “Huwezi kusumbuka kuipata hoteli
utakapofika ng’ambo. Inatazamana na Feri.” Alisita kidogo, halafu akasema kwa
hadhari, “Unajua hoteli hii mara nyingi Wamarekani huwa hawafikizii? Samahani
kwa kuingilia, lakini Wamarekani wengi wanapendelea hoteli za Gloucester au Peninsula.
Hii Celestial Empire ni kwa ajili ya Waasia.”
“Yeah, ni hapo
ndipo ninataka kufikia,” nikamwambia. “Asante kwa msaada wako.”
“Karibu sana,
mheshimiwa,” alisema, akachukua pochi yake na kunipatia kadi. “Unaweza kuhitaji
muongozaji. Ndiyo kazi yangu kuwaongoza Wamarekani wanaotembelea Hong Kong. Wewe
piga simu tu. . . .”
“Asante. Nitakumbuka.”
Nikaibana kadi kwenye mkanda wa saa yangu ya mkononi, nikainama kidogo, na
kuingia kwenye teksi.
Wakati nikiwa
kwenye ndege nilikuwa nimepitia ramani ya Hong Kong, nikagundua kwamba upande
wa bara mahalli ulipo uwanja wa ndege wa Kai Tak uliitwa Kowloon Peninsula na
eneo la Straits lenye maji ni katikati ya kisiwa cha Hong Kong, ambacho
kinafikiwa na boti za mwendokasi kwa mwezo wa dakika nne au tano.
Wanchai, ambako Jefferson
alikuwa akiishi, lilikuwa eneo la mbele ya maji hapo Hong Kong.
Mwendo wa kutoka
uwanja wa ndege hadi Feri ulichukua dakika chache tu. Eneo la ufukweni mwa
Kowloon lilisheheni watu wengi wengine wakiwa wanakimbia. Ilionekana kwamba
kuna Mzungu mmoja kati ya Wachina mia moja: hali iliyonikumbusha kwamba ni eneo
lenye pilika za wenyeji. Makuli, wakiwa wamebeba mizigo mizito kwa kutumia
fimbo za mianzi, walikimbia kukatiza barabarani, wakati mwingine wakkinusurika
kugongwa na magari. Magari makubwa ya Kimarekani, yakiendeshwa na
wafanyabiashara wanene wa Kichina, vijana wa mikokoteni wakiwa wamebeba makreti
na bidhaa za ajabu na malori makubwa ndiyo yaliyojaza mtaa. Mabango ya rangi
nyekundu yaliyoandikwa Kichina yalipamba sehemu za mbele za maduka. Watoto
wadogo wa Kichina, wakiwa wamebeba watoto migongoni mwao, walikuwa wakicheza
kwenye vibaraza na viambaza. Familia za Kichina zilikuwa zimechuchumaa kwenye
viambaza mbele ya maduka yao, wakila wali kwa kutumia vijiti.
Nilipofika Feri,
nilimlipa dereva wa teksi, nikannunua tiketi na kuingia kwenye boti ambayo
tayari ilikuwa imesheheni wafanyabiashara wa Kichina, watalii wa Kimarekani na
mabinti kadhaa wa Kichina waliovalia nguo aina ya Cheongsams, zilizokatwa
pembeni kuonyesha miguu yao minene.
Nilipata siti
karibu na ngazi na mara boti ilipoanza kukatisha maji ya Straits kuelekea
kisiwa cha Hong Kong, nikajaribu kuyazowea mazingira yaliyonizunguka.
Itaendelea
kesho…
Comments
Post a Comment