- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummuy Mwalimu akihutubia wadau
(hawapo pichani) wa kifua kikuu toka nchi mbalimbali walioshiriki Mkutano wa
Dunia wa 12 wa masuala ya Kudhibiti Kifua kikuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa
Hoteli ya Hyatt Regency jijini hapa.
Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Mohammad Bakari Kambi akiwasilisha mada mada kwenye mkutano huo
ambao unafanyika kwa siku tatu na umewashirikisha Serikali,Sekta
binafsi,Mashirika Binafsi na wadau mbalimbali wa afya.
Waziri ummy Mwalimu
akionesha kitabu cha mapambano dhidi ya kifua kikuu chenye mikakati mbalimbali
ya kudhibiti ugonjwa huo.
Waziri Ummy Mwalimu
akifuatalia Mada iliyokuwa ikiwasilishwa,kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Mohammad kambi.
Washiriki mbalimbali wa
mkutano huo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja ya
washiriki wa Mkutano wa Dunia wa 12 wa masuala ya Kudhibiti kifua Kikuu
Duniani.Nchi zilizohudhuria mkutano huo Afrika (Tanzania, Ethiopia,Kenya,
Malawi, Namibia, Uganda ,Zambia na Afrika kusini) nchi za Asia ni (India,Pakistan,Bangladesh) Picha
zote na Rayson Mwaisemba-Wizara ya Afya)
Comments
Post a Comment