- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
UNESCO YOUTH FORUM WAENDESHA SEMINA YA KUWAELEKEZA VIJANA NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI ZA UMOJA WA MATAIFA,CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO JIJINI DAR
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali.
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia Global Peace Foundation (GPF) Tanzania
aliyewakilisha katika Semina hiyo Bi. Anna Mwalongo akielezea kwa kifupi
kuhusu Asasi hiyo.
Mshauri
wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi Bw. Anthony Luvanda akitoa
masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea
kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Baadhi ya vijana wakiendelea kusikiliza kwa makini mambo mbalimbali katika Semina Hiyo
Bi.
Bernice Fernandes akielezea namna alivyopata nafasi ya kwenda kusoma
Marekani kupitia 'Scholarship' na kuwasihi vijana wasikate tamaa kwa kuwa nafasi za kwenda
kusoma nje zipo nyingi
Muandaaji
wa Semina hiyo na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza
namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za
Umoja wa Mataifa.
Mwakilishi
kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo
wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi
mbalimbali za Kiraia.
Baadhi ya vijana wakiuliza maswali mbalimbali kwa wasemaji
Picha
ya pamoja ya watoa mada mbalimbali Kutoka Kushoto ni Frank
Joash,Anthony Luvanda, Evance Exaud,Alice Norbert, Anna Mwalongo,
Bernice Fernandes, Nelson Amar na Jackson Ogonga.
Watoa Mada wakiwa pamoja na Baadhi ya washiriki waliohudhuria Semina hiyo
Picha na Fredy Njeje
Katika kuhakikisha vijana
wanashiriki na kujikwamua katika mambo mbali mbali UNESCO Youth Forum waliandaa semina ambayo ilihusu
vijana kushiriki katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa, Kudumisha amani
kutoka ngazi ya vijana na jamii kwa ujumla ambapo Global Peace Foundation
Tanzania walitoa mafunzo juu ya maswala hayo, kuhusu kusoma nje na kuelekezwa
njia mbali mbali za kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi mbalimbali za
kiraia.
Akizungumza na vijana hao kutoka
vyuo mbalimbali na wale ambao walimaliza vyuo mwakilishi wa asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF)
nchini Tanzania Bi. Anna Mwalongo alisema kuwa Global Peace Foundation ni Taasisi
isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote
ile ina makao yake makuu
katika jiji la Washington DC nchini
Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya
Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015
ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani
nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.” Alisema Anna.
Aliongeza kuwa Mnamo mwezi wa
saba mwaka 2015 Global peace foundation waliandaa Mkutano mkubwa wa amani uliofanyinka
Zanzibar uliojulikana kwa jina la Global peace Leadership Conference (GPLC
Zanzibar) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais Mh. Balozi Seif
Ali na kuhudhuriwa na marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali.
"Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha
kampeni ya “AMANI KWANZA” ambapo aliwalenga wanawake na vijana kushiriki katika
uchaguzi huo kwa amani, alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa GPF wanampango wa
kupanua wigo zaidi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi kueleza mambo
mbalimbali ya amani kupitia kampeni yao ya “VIJANA NA AMANI” " Alisema Anna
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa
program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa
uelewa ili wapate kujiunga.
Nae Bi. Bernice Fernandes pamoja
na Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili
‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi
zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi
hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.
Mwisho Mshauri na mwezeshaji
katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na
kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia
vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza
kutimiza malengo yao
Semina hiyo ilihudhuriwa na
vijana kutoka vyuo vya, Chuo kikuu cha Dar es salaam, DUCE,TIA, NIT,Bagamoyo
University,DIT na TIA , wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine ambapo
jumla yao walikuwa zaidi ya 196.
Comments
Post a Comment