- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia) akieleza kuhusu juhudi za Serikali katika
kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara wakati wa mkutano na Mjumbe wa
Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick
katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza
anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kushoto) akifafanua jambo wakati
wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango
(Mb) (hayupo pichani) kuhusu nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege
wa Msalato Dodoma, Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah
Cooke, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Mkutano walioongozana na
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick,
wakisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Mpango (Mb) (hayupo pichani), kuhusu umuhimu wa kufanya biashara ya bidhaa
zilizoongezwa thamani ili kukuza viwanda vya ndani, wakati wa mkutano huo
jijini Dr es salaam.
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza
anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kulia) akisisitiza kuhusu kuendelea
kuimalisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Uingereza huku Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini
katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa
Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kulia) baada ya
kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu Mahusiano ya kibiashara kati ya nchi
hizo mbili, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Benny
Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameitaka nchi ya Uingereza kutazama
uwezekano wa kufanya biashara na Tanzania kwa kununua bidhaa zilizoongezwa
thamani badala ya hali ya sasa ambapo nchi hiyo imekuwa ikinunua bidhaa ghafi
ilihali ikiingiza nchini bidhaa zake za viwandani.
Dkt. Mpango ameyasema
hayo alipokutana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia masuala
ya Biashara Bw. Lord Hollick ailipo tembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini
Dar es salaam.
Amesema
Tanzania inataka kuona inauza bidhaa zake zenye thamani ambazo zitatokana na
maendeleo makubwa ya viwanda hapa nchini ikiwa ni Sera ya nchi kuwa na uchumi
wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.
Nchi ya Uingereza
imekuwa ikifanya biashara na Tanzania kwa kiasi kikubwa na takwimu zinaonesha
nchi hiyo inaingiza bidhaa zenye thamani mara nane ya Tanzania jambo ambalo
linatakiwa kurekebishwa ili biashara iwe na manufaa kwa pande zote mbili.
Miongoni mwa bidhaa
ghafi ambazo zimekuwa zikisafirishwa kwenda uingereza ni pamoja na Chai, kahawa
na madini ya vito huku Uingereza ikiingiza bidhaa za viwandani zenye thamani
kubwa ikijumuisha mashine (mitambo),vifaa vya umeme, bidhaa za plastiki na
madawa.
Kwa upande wake,
Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick
amebainisha nia ya nchi yake kutaka kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika nchi za
Afrika ikiwemo Tanzania baada ya Taifa hilo kuamua kujiondoa katika
Umoja wa Ulaya.
Maeneo ambayo
Uingereza inapenda kuwekeza Tanzania ni katika Sekta ya Kilimo, Nishati ya
Umeme na Usafirishaji huku kwa sasa akionesha nia ya ya nchi yake kuwekeza
katika ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato katika Makao Makuu
ya nchi - Dodoma.
Pia nchi hizo mbili
zimekubaliana kuandaa mkutano utakao wakutanisha Serikali na Sekta Binafsi ya
Tanzania kwa upande mmoja na wawekezaji wakubwa kutoka Uingereza na nchi
nyingine za Ulaya ambao utasaidia kukuza uwekezaji na biashara na kufungua
fursa mbalimbali za kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na nchi
hizo za Ulaya ikiwemo Uingereza.
Comments
Post a Comment