- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Dada Neema Mwita Wambura (32)
akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena
uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt.
Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao
kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada
huyo kiasi cha Shilingi laki tano. Dada
Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto
uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani
Mara.
Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi
Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis
Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye
kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli
amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi
Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime
mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki
tano.
Dada Neema Mwita Wambura (32)
wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa
ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia
tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa
uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni kitendo kilichofanywa na mume wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema Mwita
Wambura (32) mara baada ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada Neema Mwita
alifanyiwa upasuaji mara nne katika siku za nyuma hospitalini hapo Muhimbili
ili kutibu majeraha yake hayo ya moto.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya
dharura na Ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga
akizungumza kuhusu hali ya mgonjwa Dada Neema Mwita Wambura (32) aliyefikishwa
tena katika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.
Dada Neema Mwita Wambura (32)
akiwa katika hali ya majonzi kufatia majeraha makubwa mwilini mwake kufatia
kumwagiwa uji wa moto na mume wake mkoani Mara.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa
ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Dkt. Ibrahim Mkoma akizungumzia historia ya mgonjwa huyo ambaye yeye
pamoja na jopo la madaktari bingwa walimfanyia upasuaji ili kutibu majeraha
yake ya ngozi katika kipindi cha nyuma. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment