- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) akiwasili Chuo
cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo mkoani Mwanza wakati wa ziara ya
kikazi mwishoni wa wiki kujionea namna
chuo hicho kinavyoendesha programu zake katika jitihada za kuendeleza sekta ya
michezo nchini. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa chuo Richard Mganga na wa
kwanza kulia ni Rais wa Serikali ya wananchuo Cletus Mutakyawa.
Na
Eleuteri Mangi, WHUSM
Wakurugenzi wa halimashauri wameaswa kutumia fursa uwepo
wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya
kilichopo mkoani Mwanza kwa kuwaruhusu
walimu wa michezo wengi zaidi kuongeza ujuzi wao ili kuinua sekta ya
michezo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipotembelea
chuo hicho kujionea namna chuo hicho kinavyoendesha programu zake katika
jitihada za kuendeleza sekta ya michezo nchini.
“Nawapongeza
viongozi, wafanyakazi na wanachuo kwa juhudi mnazofanya katika kukiimarisha
chuo hiki ambacho ni hazina ya michezo mbalimbali nchini, mmepiga hatua kubwa ya
kimaendeleo” alisema Prof. Ole Gabriel.
Chuo
hicho kimekuwa msingi wa kujenga wataalam wa michezo nchini kwa lengo la
kuimarisha mahusiano na maendeleo ya
kielimu kijamii, kielimu, kikazi na kiuchumi kwa kuzishirikisha
halmashauri zote nchini.
Katika
kuenedeleza michezo nchini, Prof. Ole
Gabriel amewaambia viongozi wa chuo hicho kuwa wawe wabunifu kwa kuongeza
programu nyingi zaidi chuoni hapo ambazo zitaongeza kipato na tija kwa chuo,
wanachuo, wananchi wanazunguka chuo na taifa kwa ujumla.
Aidha, Prof. Ole Gabriel ameongeza kuwa ni vema chuo
hicho wapange na kuanzisha mafunzo ya muda mfupi ili kurahisishs watu kupata
elimu ya michezo na kuongeza tija katika utendaji kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo Richard Mganga akitoa taarifa yake kwa Katibu Mkuu mwenye
dhamana ya michezo Prof. Ole Gabriel
alisema kuwa chuo hicho kimepata Ithibati kamili mwaka 2015 na kinafundisha
kozi ambazo zinafuata mitaala iliyopitishwa na Baraza la Taifa La Elimu
ya Ufundi (NACTE).
Mkuu huyo aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza chuo
kimekuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili kwa kozi za Stashahada ya Utawala na Uongozi katika Michezo, Stashahada
ya Elimu ya Michezo, Stashahada ya Ukocha tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na wanafunzi mwaka moja tu.
Hali hiyo imefanya idadi ya wanachuo mwaka huu wa
masomo 2016/2017 kuongezeka ambapo hadi sasa wapo wanachuo 99 ambapo mwaka wa
kwanza idadi yao ni 46 na mwaka wa pili wakiwa 53.
Comments
Post a Comment