- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini
Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya kutaka
kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL
Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya Mtendaji huyo
kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza nia ya kuzitumia
fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya Kielektroniki
(EFDs) yalivyoongeza Makusanyo ya Mapato ya Serikali alipotembelewa na
Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto),
Ofsini kwake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) akielezea riba nafuu ambayo wananchi wengi hupendelea kutoka
katika Benki baada ya kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL
Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall, Ofsini kwake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Sekta ya
Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada ya kukutana na
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall OfIsini kwake jijini Dr es
salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-WFM)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Benki ya UBL imesema iko tayari
kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata
fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi
na Watanzania pamoja na Serikali yake.
Hayo yalisemwa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini
Dar es Salaam.
Bw. Jamall alisema kuwa kwa
sasa Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala la ukuaji wa uchumi ingawa kuna
baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa fedha zimeadimika mitaani lakini ni wazi
kwamba Taifa linarudi kwenye utaratibu. Hivyo wameonesha nia ya kuwekeza hasa
katika Sekta ya Kilimo.
Naye Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa hali inabadilika na Jumuiya
ya Mabenki inaanza kuwa na imani na Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha
Benki ya UBL kuonesha nia ya kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni
jambo jema katika maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa Sekta hii mama bado
inakabiliwa na changamoto nyingi.
Alisema dhamira kubwa ya Benki
ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja
na uvuvi. Na Serikali imeahidi kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze kupiga
hatua ya haraka zaidi hasa katika kipindi ambacho imedhamiria kuwa nchi ya
Viwanda.
Akitoa ufafanuzi kuhusu
matumizi ya dola katika uchumi badala ya shilingi ya Tanzania, hasa kwenye
mikopo, Waziri Mpango alisema kuwa suala hili Serikali imeshaanza kulifanyia
kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa karibu biashara ya
maduka ya fedha za kigeni.
“Tumepiga hatua ya kufunga
mashine za kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuona
kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe kodi inayostahili. Aidha zoezi
hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania – BoT, kuona kiasi cha fedha za kigeni zilizopita
katika maduka na itaimarisha matumizi ya shilingi ya Tanzania; japo tuna
changamoto kubwa ya wananchi kutokudai risiti pindi wanapopata huduma ya
kubadilisha fedha za kigeni,” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Katika kuhitimisha majadiliano
hayo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mpango alisema Serikali itaongeza
ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa Benki
hiyo ni miongoni mwa Benki kubwa katika nchi za Uarabuni.
Imetolewa na:
Kitengo
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Fedha na Mipango
16
Februari, 2017
Comments
Post a Comment