- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (aliyevaa koti) akiwasili katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad
Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake
Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga
nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kushoto
ni Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd na Shekhe Mohammed Mussa
(aliyevaa miwani). Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya
iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake
Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga
nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kulia
kwake ni Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia aliyekaa) akimsikiliza Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe
Hamid Masoud Jongo alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu
bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,
jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni,
katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo
yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo
yakigundulika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia aliyekaa) na Kadhi wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo (wapili kulia waliokaa)
wakimsikiliza Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd alipokuwa akizungumza na
Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika
katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi
katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa
makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza
kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
*****************************************************************************
Na Felix
Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni amewataka vijana nchi kuwa makini na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya
Serikali ambayo yanajishughulisha na uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja
(ushoga).
Mhandisi Masauni
alisema, Mashirika hayo hayapaswi kuwepo nchini kwani yanafanya kazi kinyume na
mila na desturi ya nchi yetu na yanapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo endapo
yatagundulika.
Akizungumza
katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya
ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar
es Salaam, Mhandisi Masauni aliongeza kuwa, vijana wanapaswa wawe makini katika
maisha yao, kamwe wasikubali kupotoshwa pamoja na kuendeshwa na kundi lolote
ambalo linafanya kazi kinyume na taratibu za nchi.
“Kuna
baadhi ya mashirika ambayo yanajihusisha kwa kutoa elimu na kuhamasisha ndoa za
jinsia moja, mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na sheria ya nchi, hivyo
tunayachunguza na tukiyagundua hakuna cha Mswalie Mtume, tutayafuta haraka
iwezekanavyo,” alisema Masauni.
Pia aliwataka
Watanzania kutoa taarifa ya uwepo ya taasisi hizo binafsi zinazofanya shughuli
hizo nchini muda wowote wakizigundua ili zifuatiliwe kwa umakini na hatimaye zifutwe
haraka iwezekanavyo kwa kuwa zinaharibu jina zuri la Tanzania.
Masauni ambaye
alikuwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo katika
sherehe hiyo, licha ya kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo kwa kumualika, pia
aliwahasa Waislam nchini wawe na umoja, wapendane na waache kulalamika kwa kuwa
mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza mambo mema ambayo kila Muislam anatakiwa
kuyafuata.
Comments
Post a Comment