- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
TAARIFA KWA UMMA
Tunapenda kuwafahamisha wanachama wa ACT Wazalendo na umma wa Watanzania kwa ujumla, kuwa kampeni kwa ajili ya chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar na kata mbali mbali kwa Tanzania Bara ambazo chama kimesimamisha wagombea zitafunguliwa rasmi Desemba 31, 2016.
Kwa upande wa udiwani chama kilisimamisha wagombea saba na waliopitishwa na Tume ya Uchaguzi ni wagombea sita baada ya mgombea wa Kata ya Misugusugu mkoani Pwani kuenguliwa kutokana na pingamizi alilowekewa
Kata ambazo chama cha ACT Wazalendo imesimamisha wagombea ni pamoja na Isagahe, iliyopo Kahama mkoani Shinyanga, Kijichi, iliyopo Temeke jijini Dar esSalaam, Nkome iliyopo Mkoani Geita, Tanga iliyopo mkoani Ruvuma na Ihumwa iliyopo mkoani Dodoma.
Chama cha ACT Wazalendo kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika maeneo tuliyosimamisha wagombea wetu na kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kiuawajibikaji katika maeneo hayo huku tukitanguliza uzalendo kwa Taifa letu.
Pale ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda demokrasia na mabadiliko ya kweli tunawaomba wahakikishe wanamchagua mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo.
Tunawahimiza wanachama wetu na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanaiondoa CCM kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao.
Imetolewa na Abdallah Khamis
Afisa Habari ACT Wazalendo
27/12/2016
Comments
Post a Comment