- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika kwa engo la kujitabulisha .
|
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla (kulia)akimsikiliza kwa makini Meneja utwala na fedha wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,Ally Bakari wakati akizungumza mambo mbalimbali yahusuyo benki hiyo.
|
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakiwa makini katika mkutano huo.
|
Mgeni rasmi katika picha ya Pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo.
|
Na EmanuelMadafa, JamiiMojablogu Mbeya
SERIKALI MKOANI Mbeya imeitaka benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya kufanya utatifi juu ya kuwepo kwa ununuzi wa mazao kwa wakulima mapema kabla ya kuanza kukomaa hususani mazao ya ndinzi hasa katika halmsahuri ya wilaya ya Rungwe Mkoani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla wakati akizungumza na wafanyakazi wa benki Kuu Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo yenye lengo la kujitambulisha.
Amesema kwa muda mrefu sasa wakulima wa mkoa huo wamekuwa wakinyonywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakinunua mazao mapema yakiwa shambani na kupangia bei ya chini ambayo haiendani na bei hali ya sokoni .
Amesema nivema benki hiyo ikajaribu kulifanyia utatiti suala hilo ili kuona kama mfumo huo unaweza kuleta tija kwa mkulima kwani benki hiyo inanafasi nzuri ya kuisaidia serikali katika uchocheaji wa ukuaji wa uchumi.
Amesema lengo la serikali ni kuwalinda wananchi wake sanjali na kuwaondolea umaskini hivyo lazima ifanyike kila aina ya jitihada katika kufanikisha suala hilo.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa mbeya Amosi Makalla ameipongeza benki hiyo kwa kuweka jitihada za makusudi katika kudhibiti mfumuko wa bei nchini .
Amesema kama mfumuko wa bei utashindwa kudhibitiwa tafsiri halisi ya kukua kwa uchumi haitakuwa na maana yeyote kwa mwananchi wa kawaida hivyo lazima benki hiyo ikaongeza jitihada zaidi katika kudhibiti hali hiyo.
Kwa upande Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania( BOT)tawi la Mbeya Ndugu Juvent Rushaka amesema benki hiyo iko tayari kufanya utafiti suala lolote la kiuchumi
Aidha Mkurugenzi huyo ameelezea changamoto mbalimbali ambazo tawi hilo linakutana nazo likiwemo suala la kutopata takwimu mbalimbali kwa usahihi na kwa wakati .
Amesema changamoto nyingine ni miundombinu ya kiusalama ya majanga ya moto kwa kipindi kirefu sasa kwa ukosefu wa maji katika bomba la kuzimia moto hali ambayo ni hatarishi endapo litatokea janga la moto katika twi hilo .
Comments
Post a Comment