- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Charles Kitwanga (nyuma kabisa) mara baada ya kutoka Bungeni alipiga picha hizi pamoja na wabunge na madiwani kabla ya kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kwingineko.
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI.
23/05/2016.
Napenda
kuwasalimu wote na kushukuru kwa kujaliwa na uzima.
Ndugu
wanahabari tumewaiteni hapa kuja kuwaelezeni ukweli uliojificha kuhusu kitendo
klichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.
Kama
mnakumbuka kuwa Rais alichukuwa uamuzi huo Ijumaa ya Mei 20 mwaka huu kwa kwa
kosa la kwamba Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa.
Sisi
wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa na taarifa hiyo ambayo imemkuta
kiongozi wetu na Mbunge wetu kwa kuvuliwa hiyo nafasi kwa sababu nyepesi zenye
uongo mwingi wenye lengo la kumchonganisha na Rais Magufuli ili kufanikisha
lengo la waovu ambao wamebanwa na
Serikali hii ya Awamu ya tano kupitia wizara hiyo nyeti kwa usalama wa nchi.
Miongoni mwetu tulikuwa mjini Dodoma kwa
kuungana na madiwani wa Jimbo la Misungwi ambao walikwenda kumtembelea bungeni,
tulizungumza mengi kwa ajli ya jimbo letu na katika kikao chetu hapakuwa na
chembe ya kilevi chochote na hata kesho yake alipoinga bungeni alikuwa mzima wa
afya ya kimwili na akili timamu na tunawahakikishieni kuwa Kitwanga hakuwa
amelewa.
Ndugu waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 20
tulielekea bungeni kwa mwaliko wa Charles Kitwanga, tukiwa sehemu ya mualiko
uliowajumuisha Madiwani wa jimbo lake tukiwa tumeambatana naye tukaingia ndani
ya ukumbi wa bunge,tukashuhudia anajibu swali,baada ya kujibu swali la mbunge
Sakaya,tulitoka nje na kupiga picha na madiwani wote wa Misungwi waliokuja
kumtembelea Dodoma.
Baada
ya zoezi la kupiga picha kukamilika pale nje ya ukumbi wa Bunge, tulitoka na
kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kututembeza maeneo yote ya Dodoma , lakini
ilipofika jioni wakati tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa kuwa
alionekana na Waziri Mkuu akiwa amelewa.
Tukiwa
na madiwani wa CCM wa Misungwi, tunasema hizo ni habari za kupikwa na ambazo
zililenga kumchafua mbunge huyo ambaye alikuwa anaongoza huku akiwa na maadui
wengi ndani ya serikali,CCM na nje ya CCM wakiwemo mtandao wa dawa za
kulevya,walioachishwa kazi NIDA,pamoja na Uhamiaji walikuja dodoma kuhakikisha
hilo la kuondolewa Kitwanga linafanikiwa.
Ndugu
wanahabari , tulishangazwa wote kwani
tulikuwa tumekaa naye pale nyumbani kwake Sengia Dodoma (site 2) tukipata
chakula cha usiku ,alionekana kutoaamini na hata madiwani pia na wengine ambao
tulikuwepo hapa nyumbani kwake tukipata chakula hawakuamini.
Tunachosema
ni kwamba waziri Kitwanga hakulewa kama ambavyo imetafsiri sababu ya kumvua
uongozi,bali alikuwa anatafutwa ili kufanikisha lengo ambalo limefanikiwa.Mtandao
wa dawa za kulevya,pamoja na wale waliokuwa wanamshutumu kwamba amehusika
kuondolewa kwao kazini wakiwemo Watu wa NIDA, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani
Kikwete, Mfanyabiashara Said Lugumi pamoja na kundi
mafisadi waliokwapua mabilioni ya fedha
NSSF. Pia na baadhi ya wabunge wa CCM na Upinzani ambao walikuwa
hawafurahishwi na kasi ya utendaji kazi wa Kitwanga katika Wizara ya Mambo ya
ndani.
Kwa
niaba ya wananchi wenzetu tunamtahadharisha Mhe. Rais awe makini na makundi la
wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, pamoja na lile kundi la wanamtandao
masalia ndani ya CCM na serikalini na
kwenye vyombo nyeti vya ulinzi na usalama, ambayo kwa ujumla yalikuwa na
mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamtenganisha na Rais.
Ndugu
waandishi wa habari, kilichotushangaza zaidi baada tu ya Kitwanga kuvuliwa
madaraka yake ya uwaziri, kuna watu walianza kufanya sherehe wakishangilia
hususani wale waliovuliwa madaraka NIDA pamoja na NSSF,Uhamiaji na wale
wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.
Ndugu
waandishi wa habari, tunajua namna kundi la Said Lugumi,Ridhiwani Kikwete na
kampuni yao walivyokuwa wanadhamini kwa
mbinu za kifedha katika vita hii ya
kitwanga ili aondolewe, lakini baada ya kuondolewa, wakajifanya kutoa taarifa
ya kushangazwa kuondolewa kwake,
Kitwanga
amekuwa mtumishi wa serikali akiwa mtumishi mwaandamizi benki kuu Tanzania (BOT),amekuwa
mbunge na Naibu waziri kwa miaka 10,lakini hata siku moja hakuwahi kuonekana
amelewa.
=Tunaliomba
Bunge kumuomba radhi Mhe. Charles Kitwanga kwa kumdharirisha mbele ya wapiga
kura wake wa Jimbo la Misungwi familia yake pamoja na watanzania wote waliokuwa
wanaamini utendaji wake kupitia video iliyochezewa na wataalamu wa IT katika
studio za Bunge ili kufanikisha lengo la kumuonyesha Kitwanga kuwa alikuwa
amelewa bungeni.
=Tunamuomba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali bungeni
atoe uthibitisho wa kikemia unaotanabaisha wazi kama Kitwanga alikuwa katumia kilevi wakati akiwa
bungeni.
=Tunaliomba
Bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote walisambaza ile video inayoonyesha
Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana amelewa wakati kiuhalisia hakulewa na
alijibu maswali yote vizuri
=Tunaliomba
Bunge kuchunguza idara ya habari ya Bunge pamoja na studio ile ya Bunge ambao
wamehusika na kuhariri ile picha ya video iliyokuwa inasambazwa kwenye mitandao
ya kijamii.
=Tunahoji
uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu ya ulevi bila uthibitisho wa daktari
ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo kugundua kilevi cha mtu.
=
Tunaomba Watanzania wote waliosikitishwa na taarifa hizi wajue tu kwamba ile
video ambayo imemtia hatiani Kitwanga ilihaririwa kwa ustadi mkubwa kupitia
wafanyakazi wa Bunge ambao wanapitia zile asadi za bunge pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakupenda
kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya kumhujumu na sasa wanasema kwenye
vyombo vya habari ili kuhalalisha uhujumu huo.
=Tunaomba
mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia picha zinazosambazwa kwenye
mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge wa Misungwi ambazo zinaonekana
kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao kwani kisiasa zinaendelea kumchafua
na kumharibia kwa wapigakura wake,familia yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .
=Tunajiandaa
kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria kama watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo
dhidi ya Charles Kitwanga ambazo tunaamini zimetengenezwa kwa maslahi ya
makundi yanayompinga ndani ya Serikali wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.
Pia
tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini kundi la
wanamtandao walio ndani ya serikali ambalo linaongozwa wahafidhina wasio taka
mabadiliko ndani ya serikali.
Imeandaliwa na Madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja na wakereketwa wa jimbo hilo
Baraka
Kingamkono, Gaudency Tungaraza na IDDY Majumuisho.
Asanteni na Mungu
awabariki.
Comments
Post a Comment