Featured Post

VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA KUANZA KUONEKANA BAIDU SEPTEMBA HII

 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi (wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi kwa mtaalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo akikabidhi zawadi ya khanga kwa mtaalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) jijini Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO) 

Na Paschal Dotto-MAELEZO
Tanzania imeelekeza juhudi zake katika kuvutia watalii hasa wale kutoka nje ya nchi na ikilenga zaidi kuliteka soko la china lenye watu wengi duniani, ambapo kwa siku za karibuni Bodi ya utalii Tanzania ilifanya ziara kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika Miji ya Beijing, Shanghao, Chengdu, Guangzhuo, Hong Kong, Najing na Changsha.

Comments