Featured Post

WAANDISHI WA NURU FM WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZA KIJINSIA

Gerald Malekela ambaye ni program meneja wa radio akiwasilisha mada walizojadiliana kwenye kundi lao walipopata wakiwa darasani wakati wa mafunzo yanayodhaminiwa na mradi wa Boresha Habari unaoendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID.
 Baadhi ya waandishi wa Radio Nuru fm wakiwa wanasikiliza kwa umakini elimu inayotolewa na mkufunzi Temigunga Mahondo kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Waandishi wa habari wa kituo cha radio cha Nuru Fm Iringa wamepigwa msasa juu ya kuandika habari za kijinsia kupitia Mradi wa Boresha Habari unaoendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID.

Akitoa mafunzo hayo mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo alisema kuwa waandishi wengi wamekuwa wakiandika habari bila kuangalia kwa kina juu ya habari za kijinsia.

“Niwaombe waandishi wa habari hakikisheni mnaandika habari za kijinsia ili kutengeneza usawa katika jamii zetu na kuwa na kizazi ambacho kitakuwa kinaishi kwa usawa” alisem Mahondo

Mahondo alisema kuwa ni vyema waandishi wa habari wakajikita kuandika habari zinazogusa maisha ya wananchi wote bila kujali jinsia

Aidha Mahondo amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanajukumu la kuandika habari ambazo zitakuwa zinaelimisha maswala ya jinsia ili kujenga na kizazi cha kuwa na usawa.

Akichangia mada wakati wa semina mhariri wa radio Nuru fm Hafidh Ally alisema kuwa mafunzo kuwa mafunzo hayo yatawaongezea waandishi wa habari wa radio hiyo kuandika habari za kuelimisha jamii kuhusu jinsia

“Hii kwetu ni moja ya mafunzo bora ambayo yatatusaidia kuongeza uelewa wa kuandika habari za kijinsia na kukuelimisha jamii kwa kuandika habari za aina hiyo ambazo zitakuwa na mguso kwa jamii husika” alisema Ally

Ally alisema atahakikisha waandishi wa habari wa kituo cha NURU FM wanayafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo ili waweze kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa sugu katika jamii.

Lengo la mafunzo hayo ni kuondoa mfumo dume ambao umekuwa kwenye jamii zetu na umekukuwa ukilalamikiwa na taasisi mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi

Comments