Featured Post

TANAPA YAWAKUMBUKA WADAU WA UTALII, YAWAPA TUZO WALIOFANYA VIZURI KATIKA UHIFADHI NA UTALII

Waziri wa Malisili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua  mkataba wa huduma bora kwa mteja wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA, Dkt Allan Kijazi, Mjumbe wa Bodi -Tanapa, Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.

Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua  amzezindua Mfumo a uendeshaji wa viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015 Quality management system) wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa utalii wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ni miongon mwa waalikwa walioshiriki hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii.
Makamishna wasaidizi wa TANAPA wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo.
Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya TANAPA, Kamishna Nsato Marijani akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC) Dkt Ayoub Ryoba akiwa na Mkurugenzi wa Channel Ten Jafary Haniu pia walikuwa ni miongoni mwa waalikwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Makamishna wasaidizi wa Uhifadhi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo. 
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi -Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete akitangaza utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo kwa wadau wa utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika pich ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, Emilian Mallya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa tatu katika kutangaza hifadhi za taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji, Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Ryoba (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro (kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adventure baada ya kuibuka mshindi wa Jumla kwa watoa huduma za Utalii katika Hifadhi za Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mshindi wa jumla, Zainabu Ansel, Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Adventure pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA, Dkt Allan Kijazi, Mjumbe wa Bodi -TANAPA, Kamishna Nsato Marijani na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jeryy Muro. 
Washindi wa tuzo za Gold wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla.

Na Dixon Busagaga
Arusha

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  kwa mara ya kwanza limekabidhi tuzo kwa Wadau mbalimbali wa masuala ya Utalii  na Uhifadhi ,tuzo zilizokabidhiwa na Waziri wa Malisili na Utalii jijini Arusha kwa lengo la kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika masuala ya Utalii na Uhifadhi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Maount Meru ,Waziri Dkt Kigwangalla pia amezindua Mfumo wa uendeshaji wa viwango vya kimataifa  yaani ISO 9001:2015 Quality management system pamoja na mkataba wa huduma bora kwa mteja .

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi kutoka kampuni  na taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya Utalii na Uhifadhi ,Mgeni rasmi ,Waziri ,Dkt Hamisi Kigwangala aliipongeza  TANAPA kwa uamuzi wa kutoa tuzo kwa wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.

“Niwapongezeni TANAPA ,Bodi ya wadhamini na Menejenti ya TANAPA mnafanya kazi nzuri sana hasa katika kuisimamia ipasavyo sekta ya utalii, Hongereni sana.”alitoa pongezi hizo Dkt Kigwangalla.

“Nampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa kuweka mkazo kwenye sekta ya miundombinu na sekta ya anga kwani zimekuwa kichocheo katika ukuaji wa sekta ya utalii,niwahakikishie wadau wa Sekta binafsi katika sekta hii ya utalii, tutaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha lengo ni kuhakikisha tunakuza na kuendeleza sekta hii kwa kasi kubwa kabisa.”aliongeza Dkt Kigwangalla.

Dkt Kigwangalla alisema tuzo walizopata wadau wa sekta ya Utalii kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya ziwe chachu katika kuimarisha ushindani katika utoaji huduma bora katika sekta ya utalii ambapo zitasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu.

“Natoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii kuwekeza katika maeneo ya usafiri na malazi kwenye maeneo ya Kusini  na Magharibi mwa nchi yetu.”alisema Dkt Kigwangalla.

Mjumbe wa Bodi ya TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani aliyemwakilisha mwenyekiti wa bodi hiyo,Jenerali George Waitara alisema  uzinduzi wa Mkabata wa Huduma kwa Mteja utawezesha utoaji huduma kwa Haraka, ufanisi na kwa wakati ili kuondoa malalamiko na urasimu usio na tija kwa pande zote mbili.

“Sisi kama Bodi tunaahidi kuendelea kusimamia sekta hii kwa kikamilifu ili iwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini.”alisema Kamishna Nsato.

Kwa upande wake KAmishna Mkuu wa Uhifadhi ,Dkt Allan Kijazi alisema TANAPA inatambua mchango mkubwa wa wadau wetu wote katika sekta ya utalii kwa jitihada zote wanazozifanya katika sekta hiyo  ikiwemo kuiletea heshima nchi.

“ Tunathamini na tutaendelea kuthamini kila mdau anayefanya kazi na TANAPA,shirika limefanikiwa kuongeza ulinzi wa rasilimali zetu, tutaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwezesha kufikika kwa urahisi katika hifadhi zetu.”alisema Dkt Kijazi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa kampuni za Utalii nchini (TATO) Wilbert Chambulo ameishukuru TANAPA kwa tuzo hizo na kwmba shirika hilo limekuwa likijitoa kwa wadau wa utalii hali ambayo imechangia kampuni hizo kukua kiuchumi.

“TANAPA imebadilika sana.nakuahidi Mhe. Waziri Tutaendelea kulinda na kudhitibi uharibufu wa hifadhi zetu na nina kukabidhi magari mawili kwa ajili ya zoezi hilo”alisema Chambulo.

Comments