- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
HOTUBA
YA WAZIRI WA FEDHA NA
MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI
MAPENDEKEZOYA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2019/20
13 Juni, 2019 Dodoma
HOTUBA
YA WAZIRI WA FEDHA NA
MIPANGO, MHESHIMIWA DKT. PHILIP I.
MPANGO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI
MAPENDEKEZO
YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO
YA
MAPATO NA MATUMIZI KWA
MWAKA 2019/20
I.
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika,
naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kukubali
kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2019/20. Hii ni
bajeti ya nne ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bajeti hii
inawasilishwa kwa kuzingatia matakwa ya Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 26 cha Sheria
ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015.
2.
Mheshimiwa
Spika, hotuba hii inaambatana
na vitabu vinne vya bajeti. Kitabu cha Kwanza ni Makadirio ya Mapato; Kitabu
cha Pili ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Wizara, Idara zinazojitegemea,
Taasisi na Wakala wa Serikali; Kitabu cha Tatu ni Makadirio ya Matumizi ya
Kawaida kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na Kitabu
cha Nne ni Makadirio ya Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2019 pamoja
na Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Serikali wa mwaka 2019 ambavyo ni sehemu ya
bajeti hii.
3.
Mheshimiwa
Spika, naomba nianze kwa kumuinulia
Mungu moyo wangu wote kwa shukrani, kwa kuwa amenijalia mema mengi katika
maisha yangu na katika utumishi wangu kwa Taifa. Ninamshukuru kwa kuendelea
kuijalia nchi yetu amani na umoja na kutupatia safu ya juu ya uongozi wa Taifa
hili unaomtanguliza Mungu katika kuwatumikia Watanzania wote na kujielekeza
kutatua kero za wanyonge.
4.
Mheshimiwa
Spika, baada ya shukrani hizo kwa
Mwenyezi Mungu, naomba nimpongeze kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti
wa CCM Taifa, kwa uongozi wake shupavu na wa mfano katika bara la Afrika hususan
katika kufanya maamuzi magumu yenye maslahi mapana kwa Taifa. Katika kipindi
cha uongozi wake: amesimamia kwa ujasiri uvunaji adili wa rasilimali za Taifa; ameongoza
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi bila kigugumizi; amedhibiti biashara
haramu ya madawa ya kulevya; ameimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi
wa umma; na ameendelea kusikiliza na kushughulikia malalamiko na kero za
makundi mbalimbali katika jamii, wakiwemo wajasiriamali wadogo (wamachinga na
mama/baba lishe), wafanyabiashara wadogo wa madini, wakulima na wafugaji, na wafanyabiashara
wa kati na wakubwa kutoka katika wilaya zote nchini. Vile vile, ameendelea
kudumisha amani na usalama katika nchi. Aidha, amethubutu kutekeleza miradi
mikubwa ya kielelezo ili kujenga Tanzania mpya. Nitaeleza hapo baadaye mafanikio
makubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mabadiliko chanya ya
kiuchumi na kijamii nchini. Kwa sasa itoshe tu niseme kuwa yalihitajika maamuzi
magumu kutoka kwa kiongozi jasiri kuelekeza utekelezaji wa mageuzi makubwa na miradi
ya kielelezo ambayo yameleta maendeleo makubwa na ya kuvutia katika miaka hii
mitatu na nusu tu! Watanzania tunayo kila sababu ya kujivunia kumpata kiongozi
shupavu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mwenye uthubutu na uzalendo
wa hali ya juu.
5.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na pongezi hizo, ninapenda kumshukuru kipekee Mheshimiwa Rais kwa
kuendelea kuniamini katika dhamana hii kubwa ya Waziri wa Fedha na Mipango na
hivyo kuniwezesha kuandaa na kusoma hotuba ya bajeti kuu ya Serikali hivi sasa
kwa mara ya nne mfululizo. Kwa unyenyekevu, ninasema asante sana Mheshimiwa
Rais kwa heshima hii kubwa uliyonipatia mimi na wananchi wenzangu wa wilaya ya
Buhigwe na mkoa wa Kigoma kwa ujumla. Ninayasema haya nikitambua kwamba wapo Watanzania
wengi wenye sifa za kuwa Waziri wa Fedha na Mipango. Mimi ni nani basi hata
nikateuliwa na kukabidhiwa majukumu haya makubwa? Kama alivyonijibu yeye
mwenyewe siku aliponiteua, kazi hii nimepewa kwa neema tu kutoka kwa Mungu.
Hivyo, napenda niwaahidi tena Watanzania kuwa nitaendelea kuifanya kazi hii ya
Mungu kwa uadilifu.
6.
Mheshimiwa
Spika, naamini Watanzania watakubaliana nami kuwa nguzo ya uongozi thabiti ni wasaidizi imara na
wanaojituma. Hivyo, kwa namna ya pekee, napenda nimpongeze Mheshimiwa Mama
Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa
busara na bidii katika kazi zake za kumsaidia Rais kuongoza Taifa letu.
Nimpongeze pia Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kuiongoza
Zanzibar kwa hekima, hali ambayo imewaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo
yanayoonekana katika kipindi cha uongozi wake. Kadhalika, napenda kumpongeza
kwa dhati Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na mbunge wa jimbo la Ruangwa, kwa uongozi hodari ndani ya Serikali na
hapa Bungeni pamoja na kumsaidia Rais
kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi zilizomo katika Ilani ya CCM kwa Ajili
ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Vile vile kwa namna ya pekee sana nimpongeze
Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mkuu wa CCM kwa utendaji wake uliotukuka na
kusimamia misingi ya Chama Cha Mapinduzi ya kupigania usawa wa binadamu na haki
za wanyonge.
7.
Mheshimiwa
Spika, niwapongeze pia wakuu
wa mihimili mingine ya dola kwa usimamizi na uongozi shupavu, hususan wewe
Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa kuongoza vema mhimili wa Bunge.
Hakuna shaka hata kidogo na kila mtu sasa anajua kwamba Bunge hili ni chombo
chenye nguvu sana chini ya Mheshimiwa Spika, Job Ndugai na Naibu Spika Mheshimiwa
Dkt. Tulia Ackson (Mb). Aidha, ninampongeza sana Mheshimiwa Profesa Ibrahim
Hamisi Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania kwa uongozi makini wa mhimili wa Mahakama.
8.
Mheshimiwa
Spika, nichukue fursa hii
kumpongeza Mheshimiwa Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni
Katibu wa Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa Umma, kwa kutekeleza kazi
zake kwa weledi mkubwa.
9.
Mheshimiwa
Spika, napenda niwapongeze na
kuwashukuru kwa dhati wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama, makamanda na
askari wote (wanaovaa na wasiovaa sare za majeshi) kwa utumishi wao makini na
uzalendo wa hali ya juu. Kipekee naomba niwatambue Mkuu wa Majeshi, Jenerali
Venance Salvatory Mabeyo; Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Nyakoro Sirro;
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Faustine Martin Kasike; Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala; Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Dkt.
Modestus Francis Kipilimba; Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa, Kamishna wa Polisi, Diwani Athuman Msuya; Kamishna Jenerali wa
Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Rogers William Siang’a; na
Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. Hakika, Watanzania
tunatembea kifua mbele na kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi
bila wasiwasi kwa sababu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko macho na imara
kuliko chuma! Tunawaomba muendelee kutimiza wajibu wenu wa kulinda mipaka na
amani ya nchi yetu kwa wivu na moyo wa kizalendo na hivyo kuzidi kuimarisha
mazingira ya kuwasha moto wa maendeleo na ustawi wa Taifa letu na wananchi
wake.
10.
Mheshimiwa
Spika, kwa namna ya pekee ninamshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Profesa Adelardus Lubango Kilangi kwa kutayarisha kwa wakati
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2019 na Muswada wa Sheria ya Matumizi wa
mwaka 2019. Napenda pia nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti
Mheshimiwa George Boniface Simbachawene, Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, na Makamu
wake Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,
kwa umakini wao katika kuongoza shughuli za Kamati hii muhimu sana. Chini ya
uongozi wao, Kamati ya Bajeti imetupatia maoni mengi na ushauri wa kujenga
ambao umeisadia sana Serikali katika kuboresha mapendekezo ya bajeti hii.
11.
Mheshimiwa Spika, kwa kipindi chote ambacho nimekuwa kwenye nafasi hii,
napenda nishuhudie kwa Bunge hili na Taifa kwa ujumla kwamba, Kamati hii ya
Bajeti imetoa mchango mkubwa sana katika kuboresha sera za uchumi na bajeti
kuliko Watanzania wengi wanavyofahamu. Kusema kweli wanastahili kutambulika
kipekee. Kama kuna nishani au tuzo ya Spika kwa Kamati ya Bunge inayojitanabaisha
kwa utumishi uliotukuka, basi kama itakupendeza Mheshimiwa Spika, napendekeza
iwe Kamati ya kwanza kutunukiwa heshima hiyo. Aidha, ninawapongeza Wenyeviti,
Makamu wenyeviti na wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge kwa michango yao
waliyoitoa kupitia vikao vya kamati za kisekta katika kuboresha makadirio ya mapato
na matumizi ya wizara mbalimbali na Serikali kwa ujumla kwa mwaka 2019/20.
Maboresho hayo yalilenga kuwapatia Watanzania maendeleo hususan uboreshaji wa
huduma za kijamii na miundombinu.
12.
Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka 2019/20
imeandaliwa kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuwainua wananchi wanyonge kiuchumi na kuboresha mazingira ya kufanya biashara
na kuwekeza hapa nchini. Dhima kuu kama ilivyokubaliwa na nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki bado itaendelea kuwa “kujenga uchumi wa viwanda
utakaochochea ajira na ustawi endelevu wa jamii”. Bajeti hii inaendelea
kufungamanisha juhudi za kuimarisha sekta ya viwanda na uendelezaji wa sekta ya
kilimo inayoajiri wananchi wengi na hasa waishio vijijini huku msisitizo ukiwa
katika kuhamasisha tija na uzalishaji, kujenga miundombinu ya kiuchumi,
kutafuta masoko, kupunguza kero kwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara
na wawekezaji na kuimarisha huduma za jamii.
13.
Mheshimiwa Spika, leo asubuhi niliwasilisha Hotuba ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka
2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/20 ambapo nilieleza kwa
kina mwenendo wa viashiria mbalimbali vya uchumi katika mwaka 2018. Aidha,
katika hotuba hiyo, nilifafanua juu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa
wa mwaka 2018/19 na kuainisha maeneo ya vipaumbele kwa mwaka 2019/20. Hivyo,
katika hotuba hii, nitajielekeza kutoa tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya
mwaka 2018/19 na ahadi zilizomo katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka
2015, kuwasilisha maboresho ya mfumo na viwango vya kodi na tozo mbalimbali,
pamoja na mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2019/20,
ambayo yanatoa picha ya namna gani Serikali inakusudia kuendelea kukuza uchumi,
kuboresha kilimo, miundombinu, huduma na kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza
ajira na kuboresha ustawi wa Watanzania.
II.
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2018/19
Mwenendo
wa Mapato
14.
Mheshimiwa Spika, Katika bajeti ya mwaka 2018/19, Serikali ilitarajia kupata jumla ya
shilingi trilioni 32.48 kutoka katika vyanzo vyote vya ndani na nje. Mchanganuo
wa mapato yaliyopatikana hadi Aprili 2019 ikilinganishwa na lengo la kipindi
hicho ni kama ifuatavyo:
(i)
Mapato ya kodi yalifikia
shilingi trilioni 12.9, sawa na asilimia 87.4 ya lengo;
(ii)
Mapato yasiyo ya
kodi yalifikia shilingi trilioni 2.04, sawa na asilimia 122 ya lengo. Mapato
yasiyo ya kodi yalivuka lengo kutokana na kuimarika kwa matumizi ya teknolojia
katika ukusanyaji wa maduhuli kwenye taasisi za Serikali kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Serikali wa Ukusanyaji wa Mapato (Government
electronic Payment Gateway –GePG);
(iii)
Mapato ya
Halmashauri yalifikia shilingi bilioni 529.25, sawa na asilimia 72 ya lengo;
(iv)
Misaada na Mikopo
nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ilifikia shilingi trilioni 1.70 sawa na asilimia 86 ya lengo;
(v)
Mikopo ya ndani
ikijumuisha mikopo ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva ilifikia shilingi
trilioni 3.3, sawa na asilimia 57.4 ya lengo; na
(vi)
Mikopo ya masharti
ya kibiashara ya nje ilifikia shilingi bilioni 692.3.
15.
Mheshimiwa Spika, kutofikiwa kwa malengo ya mapato ya kodi kulitokana na sababu
mbalimbali, zikiwemo; ugumu wa kutoza kodi sekta
isiyo rasmi; kuendelea kuwepo kwa upotevu wa mapato kunakosababishwa na tatizo
la magendo hususan kupitia bandari bubu kwenye mwambao mrefu wa Bahari ya
Hindi; na mwamko mdogo wa wananchi kudai risiti za kielektroniki wanapofanya
manunuzi au baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutotoa risiti
wanapofanya mauzo.
16.
Mheshimiwa Spika, kutopatikana
kwa mikopo ya ndani kama
ilivyotarajiwa kumetokana na kupungua kwa washiriki katika soko la fedha la
ndani hususan mifuko ya hifadhi ya jamii iliyokuwa kwenye zoezi la
kuunganishwa. Kwa upande wa mikopo ya nje ya kibiashara, upungufu uliojitokeza
ulitokana na hali ya masoko ya fedha kimataifa kubana zaidi (tighter global
financial conditions) hususan kuimarika kwa dola ya Marekani, na riba kubwa za
mikopo. Hali hii pia ilipelekea majadiliano na taasisi za fedha za Kimataifa
kuchukua muda mrefu ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mikopo hiyo kwa
gharama zinazohimilika.
17.
Mheshimiwa
Spika, mwenendo wa upokeaji wa misaada na mikopo nafuu kutoka
kwa Washirika wa Maendeleo ulikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi
ya Washirika wa Maendeleo kutotimiza ahadi zao kama walivyoahidi kwenye bajeti
kinyume na misingi ya makubaliano kama ilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa
Ushirikiano wa Maendeleo Tanzania (Development Coperation Framework – DCF).
Mwenendo
wa Matumizi
18.
Mheshimiwa Spika, bajeti ya mwaka 2018/19 iliyoidhinishwa na Bunge ilikuwa shilingi
trilioni 32.48 ambapo shilingi trilioni 20.47 ni matumizi ya kawaida na
shilingi trilioni 12.01 ni matumizi ya maendeleo. Katika kipindi cha Julai,
2018 hadi Aprili 2019, Serikali imetoa jumla ya shilingi trilioni 22.19
zikijumuisha shilingi bilioni 529.25 kutoka kwenye makusanyo ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 16.75 zilikuwa kwa
ajili ya matumizi ya kawaida ambazo zinajumuisha shilingi trilioni 6.28 kwa
ajili ya mishahara ya watumishi wa umma, shilingi trilioni 2.49 kwa ajili ya
matumizi mengineyo na shilingi trilioni 7.98 kwa ajili ya kugharamia deni la
Serikali na mahitaji mengine ya Mfuko Mkuu.
19.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili 2019 Serikali imetoa jumla ya shilingi
trilioni 5.44 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo shilingi
trilioni 4.89 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 547.38 ni fedha za nje.
Hata hivyo, kiasi hiki hakijumuishi baadhi ya fedha kutoka kwa Washirika wa
Maendeleo zilizopelekwa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi (D-Funds)
ambazo hazikupita kwenye mfumo wa malipo wa Serikali. Fedha hizi zitajumuishwa
pindi taratibu za kiuhasibu zitakapokamilika mwishoni mwa mwaka wa fedha.
20.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mamlaka za Serikali za Mtaa hadi kufikia Aprili 2019 jumla
ya shilingi bilioni 529.25 ambazo zinatokana na makusanyo yao ya ndani
zimetumika. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 211.7 zimetumika kugharamia
miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 317.55 zimetumika kugharamia matumizi
ya kawaida.
21.
Mheshimiwa Spika, miongoni mwa maeneo ya kimkakati ambayo yamepatiwa fedha katika kipindi
cha Julai 2018 hadi Aprili 2019 ni pamoja na:
(i)
Kulipa
mishahara ya watumishi kila mwezi kwa wakati ambapo hadi Aprili 2019 jumla ya
shilingi trilioni 6.3 zimelipwa;
(ii)
Kuendelea
kulipa madeni ya Serikali kwa mujibu wa mikataba ambapo jumla ya shilingi
trilioni 5.7 zilitumika, ikijumuisha shilingi trilioni 2.8 kwa ajili ya kulipa
mtaji wa deni la ndani kwa utaratibu wa “rollover”.
(iii)
Kugharamia
uendeshaji wa ofisi ambapo jumla ya shilingi trilioni 2.2 zimelipwa;
(iv)
Mradi wa
kufua umeme utokanao na nguvu za maji katika Mto Rufiji ambapo kiasi cha shilingi bilioni 723.6 kimetolewa;
(v)
Kugharamia
elimu msingi bila ada na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, ambapo zimetolewa
shilingi bilioni 616.9;
(vi)
Awamu ya
Tatu ya Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) jumla ya shilingi bilioni 269.3 zimetolewa;
(vii)
Ununuzi na
uendeshaji wa ndege mpya ambapo zimetolewa shilingi bilioni 238.8;na
(viii)
Kuendeleza
ujenzi wa meli mpya katika maziwa makuu, zimetolewa shilingi bilioni 27.6.
Ulipaji
wa Malimbikizo ya Madai
22.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhakiki na kulipa madeni ya wazabuni, makandarasi
na watumishi ambapo hadi Mei 2019 kiasi cha shilingi bilioni 598.4 kimelipwa kati ya bajeti
iliyotengwa ya shilingi bilioni 600.0 kwa mwaka 2018/19. Kati ya kiasi
kilicholipwa shilingi bilioni 300.5 ni kwa ajili ya wakandarasi, shilingi
bilioni 232.9 ni kwa ajili ya watoa
huduma, na shilingi bilioni 65.0 ni kwa ajili ya watumishi. Aidha, Serikali imelipa
malimbikizo ya kimshahara ya watumishi 790 waliostaafu kabla hawajalipwa,
ambapo hadi Aprili, 2019 jumla shilingi bilioni 3.10 zililipwa.
23.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa madai
yaliyohakikiwa na kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kupunguza ulimbikizaji
wa madai ikiwa ni pamoja na kuhimiza uzingatiaji wa Sheria ya Bajeti Na. 11 ya
mwaka 2015; Sheria ya Ununuzi wa Umma SURA 410; Sheria ya Fedha za Umma SURA
348 na miongozo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Serikali.
24.
Mheshimiwa Spika, napenda nisisitize kuwa japokuwa rasilimali fedha zinazopatikana
hazitoshi kugharamia mahitaji yote ya kawaida na miradi ya maendeleo, hakuna
shaka kwamba kupitia jitihada tunazofanya hivi sasa, tunapanda mbegu leo ambazo
zimeanza na zitaendelea kuzaa matokeo mazuri ya Tanzania ya uchumi wa kati.
Mafanikio
ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Kutekeleza Ilani ya CCM 2015
25.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza kwa dhati ahadi zake kama
zilivyobainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 na vipaumbele
vilivyobainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ufunguzi
rasmi wa Bunge la 11 mnamo tarehe 20/11/2015.
26.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa bajeti hii ni ya nne, niruhusu tujikumbushe kwa uchache maeneo
ambayo Mheshimiwa Rais aliyawekea mkazo mkubwa mwanzoni mwa utawala wake.
Maeneo hayo ni pamoja na: kuendeleza
ukuaji wa uchumi na kujenga uchumi wa kipato cha kati; kuongeza mapato na
kuimarisha usimamizi wa matumizi ya Serikali; kuendeleza na kuimarisha ujenzi
wa miundombinu ya barabara na madaraja, viwanja vya ndege, reli mpya, bandari
na umeme; ujenzi wa viwanda; kuongeza kasi ya kuzalisha ajira na kupunguza
umaskini; kuhakikisha kwamba madini na maliasili zetu zinatumika kwa manufaa ya
Taifa letu; kuboresha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza ubora na
upatikanaji wa huduma za maji, afya na elimu (ikiwa ni pamoja na kuweka mkazo
katika viwango vya ubora wa elimu na stadi za kazi); mapambano dhidi ya rushwa
na ufisadi; kuboresha mazingira ya uwekezaji; Kuendeleza utalii; kushughulikia
migogoro ya ardhi; kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma; na kuhakikisha
kila mmoja wetu anafanya kazi.
.
27.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ya uongozi wa Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli, mafanikio mengi yamepatikana katika maeneo niliyoyataja hapo
juu, ikiashiria kwamba Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 inatekelezwa
ipasavyo.
28.
Mheshimiwa Spika, miongoni mwa mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ya Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na:
(i)
Ujenzi wa reli ya
kati kwa kiwango cha standard gauge, ambapo hadi Aprili 2019
ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam –
Morogoro (km 300) umefikia asilimia 48.9 na kipande cha Morogoro – Makutupora
(km 422), ujenzi umefikia asilimia 7.12. Mradi huu utakapokamilika utaboresha
usafiri nchini na kuwezesha usafirishaji wa mizigo (mazao, mifugo, madini,
mazao ya misitu) na abiria kwenda na kutoka nchi jirani zisizo na bahari
(Uganda, Rwanda, Burundi, DRC) na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha biashara
na huduma (trade and logistics hub) katika nchi za maziwa makuu. Aidha, mradi
huu utapunguza uharibifu wa barabara unaotokana na usafirishaji wa mizigo
mizito kwa malori, utapunguza msongamano wa shehena ya mizigo katika bandari ya
Dar es Salaam na kutoa fursa za ajira;
(ii)
Ufufuaji wa Shirika
la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo hadi Aprili 2019 jumla ya ndege sita mpya
zimenunuliwa na kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga nchini (Dar es Salaam,
Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songea, Mtwara, Arusha,
Mpanda) na kimataifa (Hahaya – Comoro, Lusaka, Harare, Entebbe, Bujumbura).
Aidha, ndege nyingine mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Bombadier Q400
zinatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka 2019. Hivi karibuni, ATCL
inatarajiwa kuanza safari kwenda Mumbai (India), Johannesburg (Afrika Kusini)
na Guangzhou (China). Kuimarishwa kwa usafiri wa anga kutasaidia sana kukuza biashara
na sekta ya utalii nchini;
(iii)
Ujenzi wa jengo la
tatu la abiria (Terminal III) na miundombinu yake katika kiwanja cha ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa
mwaka umekamilika;
(iv)
Ujenzi wa barabara
kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami, ikiwemo daraja la juu la Mfugale katika
makutano ya TAZARA; ujenzi wa barabara ya juu yenye ngazi tatu (ubungo
interchange) katika makutano ya Ubungo; barabara ya njia nane kutoka Kimara Dar
es Salaam hadi Kibaha (km 19); daraja la Magufuli katika mto Kilombero; na
kuanza ujenzi wa daraja jipya la Selander jijini Dar es Salaam ikijumuisha
barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2;
(v)
Ujenzi wa meli mpya za
kubeba mizigo na abiria kwenye Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa;
(vi)
Kukamilika kwa upanuzi
wa gati namba moja, kuanza ujenzi wa gati namba mbili, na kuendelea na ujenzi
wa sakafu ngumu katika gati la kupakua na kupakia magari katika bandari ya Dar
es Salaam. Upanuzi huu utawezesha meli kubwa kuingia na kutoka bandarini kwa
ajili ya kushusha na kupakia mizigo;
(vii)
Ujenzi wa mradi wa
kihistoria wa kufua umeme utokanao na nguvu ya maji katika Mto Rufiji wenye
uwezo wa kuzalisha MW 2,115 ambapo ujenzi wa miundombinu wezeshi imekamilika na
mkandarasi wa kutekeleza ujenzi huo ameshapatikana. Mradi huu utaiwezesha nchi
yetu kuwa na umeme wa uhakika na wa gharama nafuu ambao ni wa lazima katika
jitihada na dhamira yetu kama Taifa ya kujenga uchumi wa viwanda. Mradi huu pia
utafungua fursa za utalii, uvuvi na kilimo cha umwagiliaji; na
(viii) Kuendelea na utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kupeleka
Umeme Vijijini (REA) ambapo hadi Mei 2019, jumla ya vijiji 7,127
vimeunganishiwa umeme.
29.
Mheshimiwa Spika, yapo pia mafaniko makubwa yaliyopatikana katika kuongeza ubora na
upatikanaji wa huduma za jamii kwa kipindi cha Awamu ya Tano ambayo ni pamoja
na;
(i)
Kuendelea na
utekelezaji wa ahadi ya kugharamia elimu msingi (kuanzia shule ya msingi hadi
kidato cha nne) bila ada na kuongezeka kwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa
elimu ya juu;
(ii)
Ujenzi na ukarabati
wa miundombinu ya vyuo vikuu ikiwemo kukamilika na kuzinduliwa kwa maktaba ya
kimataifa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,100 kwa wakati mmoja katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam;
(iii)
Kuboreshwa kwa
huduma za afya katika hospitali za rufaa, mikoa, wilaya, vituo vya afya na
zahanati nchini. Aidha, upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na huduma
za kibingwa umeimarika. Vile vile, idadi ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa
kutibiwa nje imepungua na hivyo kuokoa fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya
matibabu nje ya nchi; na
(iv)
Kuimarika kwa
upatikanaji wa huduma za maji safi mijini na vijijini ambapo katika Jiji la Dar es Salaam umefikia asilimia 85,
katika mikoa mingine asilimia 80, miji midogo asilimia 64 na vijijini asilimia
64.8.
30.
Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine yaliyopatikana katika utawala wa Serikali ya Awamu
ya Tano ni:
(i)
Kutengamaa kwa
viashiria vya uchumi jumla ikiwemo ukuaji wa Pato la Taifa kwa wastani wa
asilimia 6.9 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2016 – 2018), kukua kwa
sekta ya kilimo kwa wastani wa asilimia 5.3, mfumuko wa bei wa tarakimu moja ya
kiwango cha wastani wa asilimia 4.7 katika kipindi hicho, utulivu wa thamani ya
shilingi, na kupungua kwa kiwango cha umaskini kutoka asilimia 28.2 hadi
asilimia 26.4.
(ii)
Serikali kuhamia
makao makuu ya nchi, Dodoma na kuendeleza eneo la Mji wa Serikali kwa kujenga
majengo 23 ya ofisi za wizara zote na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
miundombinu yake (umeme, maji, barabara).
(iii)
Kudhibiti utoroshaji
na uuzaji wa madini nje ili kuwezesha Taifa kunufaika na rasilimali zake ikiwa
ni pamoja na kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, kutunga
Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya Mwaka 2017,
ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la migodi ya Tanzanite Mirerani na kuanzisha masoko
ya madini;
(iv)
Kuanza utekelezaji
wa Mkakati wa Kuharakisha Maendeleo ya viwanda Nchini (Fast Tracking
Industrialization Strategy). Aidha, sekta binafsi pamoja na mifuko ya hifadhi
ya jamii zimewekeza kwenye miradi ya viwanda ambapo mifuko hiyo inaendeleza
miradi 7 kati ya miradi 25;
(v)
Mifumo ya
kielektroniki ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato imeimarishwa;
(vi)
Usimamizi wa fedha
za Serikali umeimarishwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha Akaunti Jumuifu ya
Hazina;
(vii)
Kuimarishwa kwa
taasisi za umma na zile ambazo Serikali ina hisa. Serikali imeendelea
kufuatilia na kusimamia kwa karibu zaidi utendaji katika mashirika ya umma ili
kuhakikisha kuwa michango na gawio stahiki inatolewa kwa Serikali. Katika
kuimarisha mashirika ya umma na taasisi ambazo Serikali ina hisa, Serikali
imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na mashirika mengi ambayo yalikuwa
hayatoi gawio na michango stahiki kwa Serikali kuanza kufanya hivyo. Mwaka
2015/16 kulikuwa na mashirika 13 tu yaliyotoa gawio kwa Serikali kiasi cha
shilingi bilioni 119.2 na sasa yameongezeka kufikia mashirika 28 ambayo hadi
Mei 2019 yalikuwa yametoa gawio la jumla ya shilingi bilioni 497.5.
(viii) Serikali imefanya majadiliano yenye maslahi kwa Taifa na
baadhi ya makampuni ikiwemo kampuni ya “Airtel Tanzania” ambayo yameleta
mafanikio yafuatayo: Umiliki wa hisa za Serikali kuongezeka kutoka asilimia 40
hadi asilimia 49 bila kuzilipia, Mwenyekiti wa Bodi na Afisa Mkuu wa Ufundi
(Chief Technical Officer) kuteuliwa na Serikali, Kampuni kuilipa Serikali
shilingi bilioni moja kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kiasi cha
shilingi bilioni 3 kimeshalipwa kwa kipindi cha mwezi Aprili, Mei na Juni 2019,
Kupatikana kwa kiasi cha dola za Marekani milioni moja kutoka kwa Mwenyekiti wa
“Bharti Airtel” kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii (Corporate Social
Responsibility) ambazo zimeelekezwa kujenga hospitali mpya ya kisasa Dodoma, Kufutwa
kwa madeni na madai ya “Bharti Airtel” kwa Airtel (T) kiasi cha shilingi
bilioni 937 (Dola milioni 407.38), na Serikali kupata gawio maalum kutoka
mapato ghafi ya Airtel Tanzania kwa mwaka 2019; na
(ix)
Mafanikio katika
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo ripoti ya uwazi ya kimataifa (Transparency
International) ya mwaka 2018 imeonesha Tanzania imeshika nafasi ya 16 kwa nchi
za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara ikilinganishwa na nafasi ya 27 mwaka
2015.
31.
Mheshimiwa Spika, kwa matokeo haya niliyoeleza, ni wazi kabisa kuwa Taifa
letu linakwenda mbele chini ya Serikali hii ya tano ya CCM na liko katika mwelekeo
sahihi (moving forward in the right direction). Serikali ya CCM chini ya
Jemadari Dkt. John Pombe Joseph Magufuli inawashukuru sana wananchi wote wa
Tanzania waliotimiza wajibu wao wa msingi kwa kulipa kodi ipasavyo na hivyo
kuwezesha Taifa kupata mafanikio hayo makubwa sana katika kipindi kifupi.
Wananchi wamejitoa na kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kushiriki kwenye
ujenzi wa Tanzania mpya. Mafanikio haya pia ni matunda mazuri ya kutunza
nidhamu katika usimamizi wa uchumi, udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato na
matumizi yasiyo na tija ya fedha za umma. Bajeti hii ninayowasilisha mbele ya
Bunge lako Tukufu itaendelea kutekeleza malengo ya Serikali kama yalivyoanishwa
katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa
Taifa wa mwaka 2016/17-2020/21.
III.
SERA ZA BAJETI
KWA MWAKA 2019/20
Shabaha za Uchumi Jumla
32.
Mheshimiwa Spika, Shabaha za uchumi jumla katika kipindi cha mwaka 2019/20 ni kama ifuatavyo:-
(i)
Pato la Taifa
kukua kwa asilimia 7.1 mwaka 2019 kutoka ukuaji halisi wa asilimia 7.0 mwaka
2018;
(ii)
Mfumuko wa
bei kuendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja kati ya asilimia 3.0 hadi 4.5
katika kipindi cha muda wa kati;
(iii)
Mapato ya
ndani kufikia asilimia 15.8 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20 kutoka matarajio ya
asilimia 14.3 mwaka 2018/19;
(iv)
Mapato ya
kodi kufikia asilimia 13.1 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20 kutoka matarajio ya
asilimia 12.1 mwaka 2018/19;
(v)
Matumizi ya
Serikali kufikia asilimia 22.7 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20 kutoka matarajio ya asilimia 21.6
mwaka 2018/19; na
(vi)
Nakisi ya
bajeti inakadiriwa kufikia asilimia 2.3 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20 kutoka
matarajio ya asilimia 2.0 mwaka 2018/19.
Sera na Mikakati ya Kuongeza Mapato
33.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Serikali imekusudia kuongeza na kuimarisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa lengo la kuiwezesha kugharamia shughuli za
Serikali ikiwemo miradi mikubwa ya miundombinu na huduma za jamii. Katika
kufanikisha azma hii, Serikali itatekeleza sera zifuatazo:
(i)
Kuboresha
mazingira ya kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji, ukuaji wa biashara ndogo
na za kati ili kupanua wigo wa kodi na mapato mengine ya Serikali;
(ii)
Kurekebisha
viwango vya kodi kwa lengo la kuhamasisha uzalishaji na kulinda viwanda vya
ndani dhidi ya ushindani kutoka nje;
(iii)
Kuboresha
mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari, upanuzi wa wigo wa kodi na matumizi ya
TEHAMA katika usimamizi wa kodi;
(iv)
Kuimarisha
usimamizi wa sheria za kodi ili kutatua changamoto za ukwepaji kodi na kupunguza
upotevu wa mapato, pamoja na kuweka mkazo zaidi katika kutoa elimu kwa
mlipakodi;
(v)
Kuimarisha
makusanyo yasiyo ya kodi kwa kuhimiza matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA;
(vi)
Kuendelea kuwianisha
na kupunguza tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na wakala, taasisi na Mamlaka
za Serikali za Mitaa; na
(vii)
Kuiongezea
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania uwezo hususan watumishi, vitendea kazi bora na
mafunzo ili kutambua na kudhibiti mbinu za ukwepaji kodi.
34.
Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo ya makadirio ya mapato ya ndani, Serikali imeandaa
mikakati mahsusi ya kiutawala itakayotekelezwa katika kipindi cha muda wa kati.
Mikakati hiyo inajumuisha:
(i)
Kuongeza
ufanisi katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi za ndani kwa kutekeleza Mfumo
Jumuishi wa Usimamizi wa Mapato ya Ndani (Integrated Domestic Revenue Admistrative System-IDRAS);
(ii)
Kupanua wigo
wa kodi kupitia utambuzi na usajili wa walipakodi wapya pamoja na kuendelea na
zoezi la urasimishaji wa sekta isiyo rasmi;
(iii)
Kuwekeza
kwenye maeneo ambayo Serikali inaweza kupata mapato zaidi hususan katika uvuvi
wa bahari kuu kwa kujenga bandari ya uvuvi na ununuzi wa meli za uvuvi;
(iv)
Kuimarisha
uwezo wa ufuatiliaji na udhibiti wa uhamishaji wa faida unaofanywa na kampuni
za kimataifa;
(v)
Kuimarisha
usimamizi wa misamaha ya kodi kwa kuhakikisha inaelekezwa kwenye miradi
inayokusudiwa;
(vi)
Kuhakikisha
kuwa maduhuli yote yanapitia katika Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa
Ukusanyaji wa Mapato (GePG) ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato;
na
(vii)
Kuimarisha
mifumo ya ufuatiliaji katika taasisi za Serikali ili kuhakikisha kuwa michango
stahiki ya taasisi za umma kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali inawasilishwa kwa
wakati.
35.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa misaada na mikopo
nafuu kutoka nje, Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Washirika
wa Maendeleo. Aidha, Serikali itaendeleza mazungumzo na Washirika wa Maendeleo ili kila upande uzingatie
misingi na kanuni za ushirikiano wa maendeleo pamoja na kuendeleza majadiliano ya
kimkakati (Strategic Dialogue) na kumaliza tofauti za kisera au kimtazamo pindi
inapojitokeza, pasipo kuathiri utoaji wa fedha za utekelezaji wa Bajeti ya
Serikali.
36.
Mheshimiwa Spika, kuhusu mikopo ya kibiashara ya ndani na nje, Serikali itaimarisha
uhamasishaji wa wadau katika soko la ndani kwa lengo la kuimarisha ushiriki wao
katika minada ya dhamana za Serikali. Aidha, jitihada zinafanyika ili kuvutia
wawekezaji mbalimbali kutoka nje ya nchi wenye nia ya kuikopesha Serikali ili
kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye tija kwa uchumi
wa Taifa letu.
Sera za
Matumizi
37.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Serikali itaendelea kusimamia nidhamu katika
matumizi ya fedha za umma na kufanya
ufuatiliaji na tathmini ya matumizi hususan katika miradi ya maendeleo. Lengo kuu ni
kuwa na matumizi bora ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya fedha. Aidha, Serikali itaendelea
kuhakiki, kulipa na kuzuia kuongezeka kwa malimbikizo ya madai kwa Serikali. Pia,
Serikali itaendelea kuelekeza fedha kwenye maeneo
ya kipaumbele yenye kuchochea ukuaji wa uchumi.
Maeneo ya
vipaumbele kwa mwaka 2019/20
38.
Mheshimiwa Spika, katika Hotuba niliyoiwasilisha asubuhi kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa
kwa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/20, niliainisha vipaumbele
kwa mwaka 2019/20 ambavyo vitatekelezwa kwa kuzingatia umuhimu wa pekee wa
kulinda mazingira nchini (environmental sustainability). Bajeti hii inalenga
kutekeleza vipaumbele hivyo kama ifuatavyo:
(i)
Viwanda na kilimo: Katika kuendeleza azma ya kujenga uchumi wa viwanda, katika mwaka
2019/20 Serikali itajikita kuvutia uwekezaji zaidi kwenye viwanda vinavyotumia
malighafi zinazopatikana nchini kama vile mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi,
misitu na madini; kuzalisha bidhaa
kwa ajili ya soko la ndani na ziada kwa ajili ya kuuza nje, pamoja na kuongeza
fursa za ajira. Vile vile kama wote tunavyofahamu, sekta ya kilimo (mazao,
uvuvi, mifugo na misitu) ni muhimu sana kwa uendelezaji wa viwanda Tanzania kwa
kuwa sehemu kubwa ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo. Katika
kuimarisha sekta hii, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Kuendeleza
Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II) hususan kuhakikisha upatikanaji wa mbegu
bora, pembejeo, huduma za ugani, masoko, miundombinu wezeshi na tafiti, ikiwa ni
pamoja na kupeleka fedha zaidi kwenye maeneo wezeshi kwa kilimo na kutoa nafuu
za kikodi. Aidha, Serikali
itaendelea kuimarisha bodi za mazao, kuboresha na kuhamasisha uanzishwaji wa
vyama vya ushirika vya mazao ili kuviwezesha kupata mikopo kutoka kwenye
taasisi za fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali za kilimo na
uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuongeza thamani ya mazao.
(ii)
Ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu: Licha ya kutilia mkazo kuongeza ukuaji wa sekta kuu
za uchumi zinazotegemewa na kuajiri Watanzania wengi, bajeti ya 2019/20
itaelekezwa kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu na ujuzi, chakula
na lishe bora na huduma za maji safi na salama. Aidha, kupitia bajeti hii,
msukumo utawekwa katika kuongeza ubora wa nguvukazi ili iendane na mahitaji ya
soko la ajira.
(iii)
Uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara
na uwekezaji: Bajeti hii imeweka
msisitizo mkubwa katika kuendeleza ujenzi na ukarabati wa miundombinu hususan reli,
bandari, nishati, barabara, madaraja, na viwanja vya ndege. Aidha, Serikali
itaendelea kupitia na kuimarisha mifumo
ya kisera, kisheria na kitaasisi, sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama ili
kushawishi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje. Napenda niwahakikishie wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi kwa ujumla kuwa kuanzia mwaka
ujao wa fedha, Serikali itaanza kutekeleza kwa nguvu zaidi mpangokazi wa
kuboresha mazingira ya biashara (Blueprint
for the Regulatory Reforms to improve the Business Environment) ili
mazingira ya biashara nchini yawe rafiki zaidi na yenye gharama nafuu.
(iv)
Ufuatiliaji na tathmini Bajeti hii pia inakusudia kuimarisha zaidi ufuatiliaji
na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi zote. Aidha,
Serikali itaimarisha usimamizi wa ukusanyaji mapato ya kodi na yasiyo ya kodi
ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa bajeti lakini wakati huo huo
kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa kodi unafanyika bila kuathiri biashara. Napenda
kuwasisitiza tena watumishi wa TRA kwamba hairuhusiwi kufunga biashara ili
kushinikiza mfanyabiashara alipe kodi au malimbikizo ya kodi isipokuwa kwa
kibali cha Kamishna Mkuu wa TRA.
IV. MABORESHO
YA MFUMO WA KODI, ADA NA TOZO MBALIMBALI
39.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi ikiwemo baadhi ya
viwango vya kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya Sheria mbalimbali na pia
taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya Serikali. Marekebisho haya
yamezingatia dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwa na mfumo wa kodi ambao ni
tulivu na wa kutabirika (stable and predictable). Vilevile yanalenga pamoja na
mambo mengine, kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya
kilimo, viwanda, kukuza ajira, na kuongeza mapato ya Serikali. Aidha, Serikali imeanza kutekeleza Mpango wa
Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (BluePrint) ulioidhinishwa mwaka
2017/18 kwa kuanza kupitia mfumo wa tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na
Mamlaka za Udhibiti kwa lengo la kupunguza au kuzifuta baadhi ya tozo na ada,
kupunguza na kuondoa muingiliano katika kutoza tozo hizo. Marekebisho
yanayopendekezwa yanahusu Sheria zifuatazo:-
(a)
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA
148;
(b)
Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
(c)
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
(d)
Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438;
(e)
Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168;
(f)
Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2004;
(g)
Sheria ya Bajeti, SURA 439;
(h)
Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya
Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali;
(i)
Kuanza utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha
Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint) kwa kurekebisha Ada na Tozo
mbalimbali;na
(j)
Hatua za Kisera na Kiutawala katika
Kuboresha ukusanyaji wa mapato.
(a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani,
SURA 148
40.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani, Sura 148 kama ifuatavyo:-
(i)
Kusamehe
Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye makasha yenye majokofu (HS Code 8418.69.90)
yanayotumika kwenye Kilimo cha Kisasa cha mboga mboga (horticulture) kwa
wakulima watakaoingiza makasha hayo kutoka nje ya nchi kwa matumizi ya kilimo.
Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama na kutoa unafuu katika uzalishaji
na kuhamasisha kilimo cha kisasa
cha mboga mboga nchini;
(ii)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 68(3)(d) ili kisihusishe uuzaji wa mazao ghafi
ya kilimo nje ya nchi. Lengo la hatua
hii ni kuwawezesha wauzaji wa mazao ghafi ya kilimo nje ya nchi kuendelea
kufanya biashara hiyo kwa kadri ya kibali kitakavyotolewa na Serikali;
(iii)
Kusamehe
Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vifaa vya kukaushia nafaka (Grain Drying Equipment
HS Code 8419.31.00). Msamaha huu unatarajiwa kutoa unafuu kwenye gharama za
kukausha nafaka kwa ajili ya kuzihifadhi. Aidha hatua hii itachochea ukuaji wa
kilimo cha mazao ya nafaka;
(iv)
Kupunguza
kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani kutoka asilimia kumi na nane (18) hadi
asilimia sifuri (0) kwenye huduma ya umeme unaouzwa kutoka Tanzania Bara kwenda
Tanzania Zanzibar ili kuwapunguzia gharama za maisha wananchi wa Tanzania
Zanzibar. Serikali iliridhia na kuelekeza kuwa umeme unaouzwa kutoka Tanzania Bara
kwenda Tanzania Visiwani utozwe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha
asilimia sifuri;
(v)
Kutoa
msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa vilainishi vya ndege vinavyoingizwa
nchini na waendeshaji wa ndani, Shirika la ndege la Taifa, au mashirika ya
ndege yanayotambulika katika Mikataba ya Kimataifa ya Huduma za Anga (Bilateral
Air Services Agreements) kwa Kufanya marekebisho ya Sehemu ya Pili ya Jedwali
la Misamaha la Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani katika kipengele cha 11.
Hatua hii itawezesha nchi yetu kusaini Mikataba ya Kimataifa ya Huduma za Anga
ambayo ilishindikana kusainiwa hapo awali kutokana na kutokuwepo kwa msamaha
huo;
(vi)
Kusamehe
Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye tiketi za ndege, vipeperushi, kalenda,
shajara, karatasi zenye nembo na sare za wafanyakazi zilizowekwa nembo ya
Shirika husika la ndege, kwa kufanya marekebisho ya Sehemu ya Pili ya Jedwali
la Misamaha la Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kuongeza kipengele
kipya kinachotoa msamaha pale vinapoingizwa nchini na mashirika ya ndege
yanayotambulika katika Mikataba ya Kimataifa ya Huduma za Anga. Hatua hii
itawezesha nchi yetu kusaini Mikataba ya Kimataifa ya Huduma za Anga ambayo
ilishindikana kusainiwa hapo awali kutokana na kutokuwepo kwa msamaha huo; na
(vii)
Kufuta
msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani uliokuwa unatolewa kwenye taulo za Kike
(HS Code 9619.00.10) kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bidhaa hiyo muhimu
kwa bei nafuu kwa walengwa na badala yake unawanufaisha wafanyabiashara. Aidha,
wakati Serikali ilipoweka msamaha huu ilitarajia kwamba wazalishaji wa taulo za
kike wataziuza kwa bei nafuu baada ya kusamehewa kodi.
Hatua zote za Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 1,646.7
(b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332
41.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura
332 kama ifuatavyo:-
(i)
Kupunguza
kiwango cha Kodi ya Mapato ya Makampuni (Corporate Income Tax) kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato kutoka asilimia 30
hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka miwili (2) kuanzia mwaka 2019/20 hadi
mwaka 2020/21 kwa wawekezaji wapya wa viwanda vya kuzalisha taulo za kike.
Aidha, Serikali itaingia mkataba wa makubaliano (Performance Agreement) na kila
mwekezaji ambao utaainisha wajibu wa kila upande. Lengo la hatua hii ni kuvutia
uwekezaji katika uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu, kuongeza ajira na mapato ya
Serikali. Vile vile hatua hii itapunguza matumizi ya fedha za kigeni
zinazotumika kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje na kuhamasisha uzalishaji wake
ndani ya nchi;
(ii)
Kusamehe
Kodi ya Zuio inayotozwa kwenye gharama zinazoambatana na mikopo (mfano ada za
bima, gharama ya usimamizi, na uandaaji wa mkopo, na ada nyingine zinazoendana
na gharama za mkopo) kwa mikopo inayotolewa na Benki, Taasisi za Fedha za nje
na wahisani mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Serikali. Lengo la
hatua hii ni kuiwezesha Serikali kupata mikopo kwa gharama nafuu na kwa muda
mfupi. Aidha, msamaha huu utaiwezesha Serikali kutekeleza miradi yake kwa
wakati;
(iii)
Kutoa
msamaha wa kutengeneza hesabu ambazo zinatakiwa kuwasilishwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwa ajili ya ukokotoaji wa Kodi ya Mapato kutoka kiwango cha sasa cha
shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) hadi shilingi milioni mia moja (100,000,000/=).
Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa mlipa kodi ya kutafuta mtaalam
(Certified Public Acountant) kwa ajili ya kutengeneza hesabu. Aidha, hatua hii
inalenga pia kuchochea ulipaji kodi wa hiari na kuongeza mapato ya Serikali; na
(iv)
Kusamehe
kodi kwenye mauzo ghafi yasiyozidi shilingi milioni nne (4,000,000/=) kwa wenye
vitambulisho vya wajasiriamali na kupunguza kiwango cha chini cha kodi kutoka
shilingi laki moja na nusu (150,000/=) kwa mwaka hadi shilingi laki moja
(100,000/=) kwa mwaka kama ilivyofafanuliwa kwenye Jedwali Na. 1 na Na. 2.
Lengo la hatua hii ni kupunguza mzigo wa kodi kwa walipakodi wadogo pamoja na
kuoanisha viwango vya kodi na kiwango cha chini kinachotakiwa kwa
mfanyabiashara kutumia mashine ya kodi ya kielektroniki (EFD) ambacho kwa sasa
ni shilingi milioni kumi na nne (14,000,000/=). Aidha, hatua hii inalenga pia
katika kusisitiza matumizi ya mashine za kielektroniki (Electronic Fiscal
Device- EFD) ili kuwezesha ukokotoaji wa kodi ulio sahihi na kuongeza ulipaji
kodi wa hiari.
Jedwali Na.1: Viwango vya sasa vinavyotozwa kodi kwa
Wafanyabiashara wasiotengeneza Vitabu vya Hesabu
Mauzo
(Shilingi)
|
Kodi ya
kulipa kwa Mfanyabiashara asiye na Kumbukumbu kamili kwa mujibu wa kifungu
cha 35 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi
|
Kodi ya kulipa kwa Mfanyabiashara mwenye kumbukumbu
kamili kwa mujibu wa kifungu cha 35 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi
|
Mauzo yasiyozidi Shilingi
4,000,000
|
Hamna
|
Hamna
|
Mauzo yanayozidi shilingi
4,000,000 lakini hayazidi shilingi 7,500,000
|
Shilingi
150,000
|
Asilimia 3 ya kiasi cha
mauzo kinachozidi shilingi 4,000,000
|
Mauzo yanayozidi shilingi
7,500,000 lakini hayazidi shilingi 11,500,000
|
Shilingi
318,000
|
Shilingi 135,000 jumlisha
asilimia 3.8 ya kiasi cha mauzo kinachozidi Shilingi 7,500,000
|
Mauzo yanayozidi shilingi
11,500,000 lakini hayazidi shilingi 16,000,000
|
Shilingi
546,000
|
Shilingi
285,000 jumlisha asilimia 4.5 ya kiasi cha mauzo
kinachozidi Shilingi 11,500,000
|
Mauzo yanayozidi shilingi
16,000,000 lakini hayazidi shilingi 20,000,000
|
Shilingi
862,500
|
Shilingi
487,000 jumlisha asilimia 5.3 ya kiasi cha mauzo kinachozidi shilingi
16,000,000
|
Jedwali Na. 2: Viwango
Vipya vinavyopendekezwa kutozwa kodi kwa Wafanyabiashara wasiotengeneza Vitabu
vya Hesabu
Mauzo (Shilingi)
|
Kodi ya
kulipa kwa Mfanyabiashara asiye na Kumbukumbu kamili kwa mujibu wa kifungu
cha 35 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi
|
Kodi ya
kulipa kwa Mfanyabiashara mwenye kumbukumbu kamili kwa mujibu wa kifungu cha
35 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi
|
|
Mauzo yasiyozidi Shilingi 4,000,000
|
Hamna
|
Hamna
|
|
Mauzo yanayozidi shilingi 4,000,000 lakini hayazidi shilingi 7,000,000
|
Shilingi 100,000
|
Asilimia 3 kiasi cha mauzo kinachozidi shilingi 4,000,000.
|
|
Mauzo yanayozidi shilingi 7,000,000 lakini hayazidi shilingi 11,000,000
|
Shilingi 250,000
|
Shilingi 90,000 jumlisha asilimia 3 kiasi cha mauzo kinachozidi
Shilingi 7,000,000.
|
|
Mauzo yanayozidi shilingi 11,000,000 lakini hayazidi shilingi
14,000,000
|
Shilingi 450,000
|
Shilingi 230,000 jumlisha asilimia 3 ya kiasi cha mauzo kinachozidi
Shilingi 11,000,000
|
|
Mauzo yanayozidi shilingi
14,000,000 lakini hayazidi shilingi 100,000,000
|
Shilingi 450,000 jumlisha asilimia 3.5 ya
kiasi cha mauzo kinachozidi shilingi 14,000,000
|
||
Hatua hizi za Kodi ya
Mapato kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 35,192.5
(c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
42.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Kifungu cha 124(2),
marekebisho ya viwango maalum vya Ushuru wa Bidhaa (specific duty rates) kwa
bidhaa zote zisizo za petroli yanaweza kufanyika kila mwaka ili kuviwianisha na
mfumuko wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla. Kwa msingi huo wa sheria,
napendekeza kutokufanya mabadiliko ya
viwango maalum vya Ushuru wa Bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli.
Aidha, hatua hii inazingatia kiwango kidogo cha mfumuko wa bei nchini na azma
ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda, na hivyo kuhamasisha uwekezaji kwenye
Sekta ya Viwanda, kuvilinda na hatimaye kukuza ajira na mchango wa sekta hiyo
kwenye Pato la Taifa. Hata hivyo, napendekeza kurekebisha Sheria ya Ushuru wa
Bidhaa kwa bidhaa chache tu kama ifuatavyo:-
(i)
Kupunguza
Ushuru wa Bidhaa kwenye mvinyo uliotengenezwa kutokana na usindikaji wa matunda
(kama ndizi, mabibo, rozela/choya, nyanya, nk) yanayozalishwa hapa nchini
tofauti na zabibu kwa kiwango kinachozidi asilimia 75 kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 61 kwa lita ikiwa ni punguzo la
shilingi 139 kwa lita. Lengo la
hatua hii ni kuhamasisha ulipaji wa kodi wa hiari na pia kuvutia uwekezaji
kwenye viwanda vidogo vidogo vya aina hii. Aidha, bei ya mvinyo huu kwa lita
inafanana na bei ya vinywaji baridi;
(ii)
Kutoza
Ushuru wa Bidhaa wa asilimia 10 kwenye
nywele za bandia zinazotengenezwa ndani ya nchi na asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa
kutoka nje ya nchi zinazotambuliwa kwa HS Code 67.03; 67.04 na 05.01. Lengo la
hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali;
(iii)
Kusamehe
Ushuru wa Bidhaa kwenye vilainishi vya ndege (lubricants) vinavyoingizwa nchini
na Shirika la ndege la Taifa au mashirika ya ndege yanayotambulika katika
mikataba ya Kimataifa ya huduma za anga. Lengo la hatua hii ni kuiwezesha nchi
yetu kusaini mikataba ya Kimataifa ya Huduma za Anga ambayo ilishindikana
kusainiwa hapo awali kutokana na kutokuwepo kwa msamaha huo; na
(iv)
Kutoza
Ushuru wa Bidhaa wa asilimia 10
kwenye bidhaa za mabomba na vifaa vya plastiki vinavyotumika kwenye ujenzi wa
miradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya maji kwa kuwa hivi sasa kuna viwanda vingi
vyenye uwezo wa kuzalisha bidhaa hizo na kutosheleza mahitaji hapa nchini.
Hatua hii inahusisha bidhaa za mabomba na plastiki zinazotambuliwa katika HS
Code 39.17. Lengo la kuanzisha Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa hizo ni kulinda
viwanda na kuongeza fursa za kazi, ajira na mapato ya Serikali.
Hatua za Ushuru wa Bidhaa
kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 2,955.50.
(d) Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438
43.
Mheshimiwa
Spika; napendekeza kuongeza muda wa ziada wa miezi sita (6)
hadi Disemba 2019 kwa walipa Kodi waliokubaliwa kulipa kodi wanazodaiwa kwa
utaratibu maalum wa kusamehe malimbikizo ya nyuma ya riba na adhabu (Tax
Amnesty on Interest and Penalties) kwa asilimia 100 kwa kufanya marekebisho ya
Kifungu cha 70 (2) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015 . Hatua hii
inapendekezwa kutokana na muitikio mzuri wa walipakodi wakati msamaha huo
ulipotolewa mwezi Julai 2018 ambapo dhamira ya Serikali ilikuwa ni kutoa ahueni
kwa walipakodi waliokuwa na malimbikizo makubwa yanayoathiri biashara zao.
Hatua hiyo ya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi
inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 367,000.
(e) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168
44.
Mheshimiwa
Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya
Usalama Barabarani, Sura 168 kama ifuatavyo:-
(i)
Kuongeza
muda wa Leseni za udereva kutoka miaka mitatu (3) ya sasa hadi miaka mitano
(5);
(ii)
Kuongeza
tozo ya Leseni ya udereva kutoka shilingi elfu arobaini (40,000) kwenda
shilingi elfu sabini (70,000); na
(iii)
Kuongeza
ada ya kadi ya usajili wa magari kutoka shilingi elfu kumi (10,000/=) hadi
shilingi elfu hamsini (50,000/=); pikipiki za matairi matatu kutoka shilingi elfu kumi (10,000/=) hadi shilingi
elfu thelathini (30,000/=) na pikipiki
kutoka shilingi elfu kumi (10,000/=) hadi shilingi elfu ishirini
(20,000/=).
Lengo
la mapendekezo haya ni kupunguza gharama za kuchapisha leseni kwa kipindi cha
miaka mitatu kwani leseni hizo zinaweza kudumu zaidi ya miaka mitano. Aidha,
marekebisho haya pia yanalenga katika kuoanisha gharama za uchapishaji wa leseni
na kipindi cha leseni husika.
Hatua hizi kwa pamoja
zinatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 18,147.0
(f) Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2004
45.
Mheshimiwa
Spika, kikao cha Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti (Pre-Budget consultations of Ministers of
Finance) kilichofanyika tarehe 3 Mei, 2019 mjini Arusha, kilipendekeza kufanya
marekebisho ya Viwango vya Ushuru wa Pamoja wa Forodha (EAC – Common External
Tariff “CET”) na Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs
Management Act, 2004) kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Mapendekezo hayo yanalenga
katika kuendeleza viwanda, kukuza ajira na kuboresha maisha ya wananchi katika
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
46.
Mheshimiwa
Spika, Mapendekezo ya Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho
kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha yanahusisha hatua mpya na
zinazoendelea ambazo zimekuwa zikitekelezwa katika mwaka 2018/19.
(i)
Mapendekezo
ya hatua mpya za viwango vya Ushuru wa Forodha ni kama ifuatavyo:-
(a)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye malighafi ya kutengeneza taulo za watoto (Baby Diapers)
zinazotengenezwa hapa nchini kwa mwaka mmoja. Aidha, Watakaonufaika na punguzo
hili ni viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo hapa Tanzania na utaratibu
utakaotumika katika kuagiza malighafi hizo ni ule wa kuwapa unafuu wa Ushuru wa
Forodha “Duty Remission”. Aidha,
Serikali itaendelea kutoza ushuru wa Forodha wa asilimia 25 kwa taulo za watoto
(Baby Diapers) za kutoka nje ya nchi. Hatua hii inatarajiwa kutoa unafuu wa
gharama za uzalishaji, ajira na mapato ya Serikali. Aidha ni matarajio ya
Serikali kuwa viwanda vinavyonufaika na msamaha huu wa Ushuru wa Forodha
vitazalisha bidhaa hizi muhimu kwa afya ya watoto na kuziuza kwa bei nafuu ili
watanzania wengi waweze kuzinunua. Malighafi zitakazohusika katika msamaha huu
ni zile zinazotumbulika katika HS Code 3506.91.00; PE Film HS Code 3926.90.90;
Super Aborbent Polymer HS Code 3906.90.00; Wet Strength Paper HS Code
4803.00.00; Non Wovens HS Code 5603.11.00; Polyethylene Laminated Non Wovens HS
Code 5903.90.00; Spandex HS Code 5402.44.00; na Dust Free Paper Hs Code
4803.00.00;
(b)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka kiwango
cha asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifaa
vinavyotumika katika kukata, kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya vito.
Hatua hii itawanufaisha wanaofanya shughuli hizo na utaratibu wa “Duty Remission” ndio utatumika katika
kuagiza vifaa hivyo. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu wa gharama na
kuhamasisha ukataji na usafishaji wa madini hayo hapa nchini na hivyo kuongeza
thamani yake kabla ya kuuzwa. Aidha, hatua hii itaongeza mapato ya Serikali na
ajira. Vifaa vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS Codes
3606.90.00; 6804.10.00; 6813.20.00; 7018.90.00; 7020.00.99; 8202.20.00;
8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90;
8513.10.90; na 9002.19.00;
(c)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye makaratasi (HS Code 4805.11.00 na
4805.19.00) yanayotumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio vya mboga
mboga kwa ajili ya kuuza nje ya nchi. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika ambapo viwanda vinavyotengeneza
vifungashio hivyo tu ndivyo vitakavyonufaika. Lengo la kuondoa Ushuru wa
Forodha kwenye malighafi hizo ni kupunguza gharama ya utengenezaji wa
vifungashio ili kulinda viwanda vya ndani dhidi ya ushindani wa nje, kuvutia uwekezaji katika
uzalishaji wa vifungashio vya aina hii na hatimaye kuhamasisha uuzaji nje wa
mboga mboga kwa ajili ya kupata fedha za kigeni;
(d)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya mbegu vinavyotumiwa na
wazalishaji wa mbegu hapa nchini. vifungashio vitakavyohusika ni vile
vinavyotambulika katika HS codes 3923.29.00; 6305.10.00; 4819.40.00;
7310.29.90; 6305.33.00; 6305.20.00; 6304.91.90; 7607.19.90. Lengo la hatua hii
ni kuongeza ubora wa mbegu na pia kuzipa unafuu wa gharama Taasisi
zinazozalisha mbegu hapa nchini. Aidha utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika kuagiza vifungashio hivyo;
(e)
Kupunguza ushuru wa forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwa utaratibu wa “Duty Remmission” kwenye malighafi (Alluminium Alloys) zenye HS
Code 7606.92.00 zinazotumika katika kutengeneza sufuria (Alluminium pots).
Hatua hii inalenga katika kupunguza gharama za uzalishaji, kuhamasisha
uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu hapa nchini, kulinda viwanda vya ndani ili
viweze kuongeza uzalishaji wa kutosheleza mahitaji na kuongeza ajira;
(f)
Ili kulinda na kuhamasisha uzalishaji wa
kahawa hapa nchini pamoja na kuongeza mapato ya Serikali napendekeza kuongeza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye kahawa inayoagizwa nje ya nchi (HS Code
09.01);
(g)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za kimarekani 125 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric
ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa
badala ya asilimia 10 pekee. Bidhaa
hizo ni “Flat -rolled products of iron or
Non-alloy steel na Flat –rolled products of other alloy steel.” Bidhaa hizi hutambulika katika HS Codes
7209.16.00; 7209.17.00; 7209.18.00; 7209.26.00; 7209.27.00; 7209.28.00;
7209.90.00; 7211.23.00; 7211.90.00; 7225.50.0 na 7226.92.00. Lengo la kuweka
viwango hivyo vya Ushuru wa Forodha ni kudhibiti udanganyifu wa thamani halisi
ya bidhaa hizo na kulinda viwanda vya
hapa nchini na ajira;
(h)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric
ton) kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa
badala ya asilimia 25 pekee. Ushuru
huo unahusu bidhaa zinazotambulika katika HS Code 7212.30.00; 7212.40.00 na
7212.50,00. Hatua hii ina lengo la kulinda viwanda vya ndani kutokana na
udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje
(under-invoicing and under valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(i)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric
ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa kwenye bidhaa za mabati
zinazotambulika katika HS Code 7212.60.00 badala ya kutoza ushuru wa asilimia 10 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda
viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo
zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under valuation), na kulinda
ajira na mapato ya Serikali;
(j)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 250 kwa kila tani moja ya ujazo (metric
ton) kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa
badala ya ushuru wa asilimia 25
pekee. Hatua hii inahusu bidhaa zinazotambulika katika HS codes 7210.41.00;
7210.49.00; 7210.61.00; 7210.69.00; 7210.70.00 na 7210.90.00. Lengo la hatua
hiyo ni kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini kutokana na ushindani
wa nje;
(k)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 250 badala ya kiwango cha asilimia 25 au dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (metric
ton) kwenye bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kipi ni kikubwa
kwenye nondo kwa mwaka mmoja. (Reinforment bars and hallow profile). Hatua hii
inahusu bidhaa zinazotambulika katika Hs codes 7213.10.00; 7213.20.00;
7213.99.00; 7214.10.00; 7214.20.00; 7214.30.00; 7214.90.00; 7214.99.00;
7215.10.00; 7215.50.00; 7215.90.00; 7225.90.00; 7225.92.00; 7225.99.00;
7306.30.00; 7306.50.00; 7306.61.00; 7306.69.00; na 7306.90.00. Lengo la hatua
hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha nondo hapa nchini na kuongeza ajira;
(l)
Kwa kuwa mbogamboga zinalimwa kwa wingi hapa
nchini, napendekeza kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mboga mboga (horticultural
products) zinazotambulika kwenye HS codes 0603.11.00; 0603.12.00; 0603.13.00; 0603.14.00;
0603.19.00; 0604.20.00; 0604.90.00; 0701.90.00; 0702.00.00; 0703.10.00;
0703.20.00; 0706.10.00; 0710.10.00; 0710.21.00; 0710.22.00; 0710.30.00;
0714.10.00; 0714.20.00; 0804.30.00; 0804.40.00; 0804.50.00; 0805.10.00;
0805.40.00; 0805.50.00; 0806.10.00; 0807.11.00; 0807.20.00; 0808.10.00;
0808.20.00. Aidha, hatua hii itaongeza mapato ya serikali; na
(m) Kutoza
ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 10
badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja
kwenye bidhaa za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC Profiles HS Code 3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo
hutumika kwa ajili ya kutengenezea fremu za milango, madirisha n.k. Lengo la
hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali.
(ii)
Mapendekezo
ya kuendelea na utekelezaji wa viwango vya Ushuru wa Forodha vya mwaka 2018/19
ni kama ifuatavyo;-
(a)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye karatasi
zinazotambulika kwenye HS codes 4804.11.00; 4804.21.00; 4804.29.00; 4804.31.00
na 4804.41.00. Karatasi hizi ni zile zinazozalishwa na kiwanda cha Mufindi;
(b)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 35 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code
1001.99.00 na HS Code 1001.99.90. Hatua hii imezingatia kwamba uzalishaji wa
ngano katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hautoshelezi mahitaji, na
bidhaa hii ni muhimu katika kutengeneza vyakula mbalimbali. Lengo la Serikali
ni kuwezesha Viwanda na walaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa ngano waweze
kupata vyakula husika kwa bei nafuu na tulivu. Aidha utaratibu wa “Duty Remission” utaendelea kutumika
katika kuagiza ngano hiyo ambapo Viwanda vinavyotumia ngano ya aina hii katika
uzalishaji ndivyo vinavyohusika katika kutumia kiwango hicho nafuu cha Ushuru
wa Forodha. Kutokana na mahitaji makubwa ya ngano katika Jumuia ya Afrika
Mashariki na SADC, wakati umefika sasa kwa wananchi kuchangamkia fursa ya
Kulima ngano katika maeneo mbalimbali nchini yanayofaa kwa kilimo cha ngano
ikiwemo eneo la shamba la Basuto;
(c)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia
10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja
kwenye mashine za kielektroniki zinazotumika kukusanya mapato ya Serikali
(Electronic Fiscal Device) zinazotambulika katika HS Code 8470.50.00;
(d)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa
ijulikanayo kama “Printed Alluminium
Barrier Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90 ambayo hutumika kama malighafi
ya kutengeneza dawa ya meno kwenye viwanda vya ndani;
(e)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye bidhaa ya kutengeneza sabuni ijulikanayo
kama RBD Palm Stearin (HS Code 1511.90.40);
(f)
Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa
asilimia 25 au dola za kimarekani 1.35 kwa kilo moja ya viberiti (safety
matches) vnavyotambuliwa kwenye HS code 3605.00.00 kutegemea kiwango kipi ni
kikubwa;
(g)
Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha
wa asilimia 25 au dola za kimarekani 350
kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kutegemea kiwango kipi ni kikubwa
kwenye bidhaa za chuma za misumari zinazotambulika katika HS code 7317.00.00
(nails, tacks, drawing pins, corrugated nails, staples other than those of
heading 83.05);
(h)
Kutoza ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye soseji
(sausages) na bidhaa za aina hiyo (HS code 1601.00.00);
(i)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye chingamu
(chewing gum) zinazotambulika katika HS code 1704.10.00;
(j)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye peremende (HS
code 1704.90.00);
(k)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye chokoleti (chocolates) HS
code 18.06 kwa mwaka mmoja;
(l)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye biskuti (HS code 1905) kwa
mwaka mmoja;
(m) Kutoza
Ushuru wa Forodha wa asilimia 35
badala ya asilimia 25 kwa mwaka
mmoja kwenye nyanya zilizosindikwa (tomato sauces) zinazotambulika katika HS
code 2103.20.00;
(n)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 60 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye maji (mineral
water) yanayotambulika katika HS code 2201.10.00;
(o)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye nyama (meat and edible meat
offal in chapter 2) kwa mwaka mmoja;
(p)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 kwenye mafuta Ghafi ya kula (mfano
alizeti, mawese, soya, mizeituni, nazi, karanga, mahindi n.k) kwa mwaka mmoja.
Hatua hii inalenga katika kulinda na kuhamasisha uzalishaji wa mbegu za mafuta
na mafuta ya kula hapa nchini. Nchi yetu ina fursa kubwa ya kukuza uzalishaji
wa bidhaa hiyo. Hivyo, kuna umuhimu wa kuchochea na kuhamashisha uzalishaji wa
mbegu za mafuta na uchakataji wa mafuta ghafi kwa kutumia mbegu zinazozalishwa
hapa nchini. Lengo la hatua hii ni kuongeza ajira mashambani, viwandani na pia
kulinda fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta hayo nje ya nchi. Mafuta
ghafi hayo yanatambulika kwenye HS code 1507.10.00; 1508.10.00; 1511.10.00;
1512.11.00; 1513.11.00; 1514.11.00; 1514.91.00; 1515.11.00; 1515.21.00;
1515.30.00;
(q)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye mafuta ya
kula yaliyochakatwa kwa kiwango cha mwisho (semi-refined, refined/double
refined oil) mfano alizeti, mawese, soya, mizeituni, karanga, nazi, mahindi
n.k. Ongezeko la Ushuru wa Forodha linatarajiwa kuhamasisha uchakataji wa mbegu
za mafuta hapa nchini na kuongeza ajira viwandani na mashambani. Aidha ongezeko
la Ushuru wa Forodha linahusu mafuta yote ya kula yaliyochakatwa yanayoingizwa
nchini na yanayotambulika kwenye HS codes 1507.90.00; 1508.90.00; 1509.90.00;
1510.00.00; 1511.90.10; 1511.90.30; 1511.90.90; 1512.19.00; 1512.29.00;
1513.19.00; 1513.29.00; 1514.19.00; 1514.99.00; 1515.19.00; 1515.20.00;
1515.50.00; 1515.90.00;
(r)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwenye “Gypsum Powder” HS code
2520.20.00 kwa mwaka mmoja;
(s)
Kupunguza ushuru wa forodha kutoka asilimia 100 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye sukari ya matumizi ya kawaida
(consumption sugar) inayoagizwa kutoka nje ya nchi kwa vibali maalum kwa lengo
la kuziba pengo (gap sugar) la uzalishaji hapa nchini. Lengo la hatua hii ni
kulinda viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari, ajira na mapato ya Serikali;
(t)
Kutoza kwa mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa
asilimia 35 kwenye mitumba
inayoingia kutoka nje (badala ya asilimia 35
au dola za marekani 0.40 kwa
kilo moja kutegemea kiwango kipi kikubwa);
(u)
Kusamehe Ushuru wa Forodha kwenye malighafi,
vipuri na mashine vinavyotumika katika kutengeneza nguo na viatu vya ngozi.
Aidha, Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameridhia orodha iliyooanishwa
(harmonized list) ya malighafi na vipuri ili kutoa msamaha wa Ushuru wa Forodha
na kuziwezesha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ziweze kufanya biashara kwa
bidhaa za nguo na viatu vya ngozi vitakavyozalishwa ndani ya Jumuiya; na
(v)
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
zimekubaliana kutoza Ushuru wa Mauzo nje (Export Levy) wa asilimia 10 kwenye ngozi iliyosindikwa kwa
kiwango cha kati (wet blue). Lengo la hatua hii ni kuhamasisha usindikaji wa
ngozi, kuongeza thamani, na kuongeza ajira katika nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
47.
Mheshimiwa
Spika, Mawaziri wa Fedha wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki walifanya pia marekebisho kwenye Sheria ya Forodha ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC Customs
Management Act, 2004) kama ifuatavyo:-
(i)
Kufanya
marekebisho katika kipengele cha 1 (a) Sehemu B ya Jedwali la Tano la Sheria ya
Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-CMA, 2004) ili kuingiza vilainishi
kwa ajili matengenezo ya ndege (Lubricants for Aircraft), sare (uniforms),
kalenda, shajara na peni kwenye orodha inayopata msamaha wa Ushuru wa Forodha
kwenye huduma za ndege. Lengo la kutoa msamaha huo ni kuiwezesha nchi yetu
kusaini mikataba ya Kimataifa ya Huduma za Anga ambayo haikuweza kusainiwa hapo
awali kutokana na kutokuwepo kwa msamaha huo.
Hatua hizi za Ushuru wa
Forodha kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 31,074.0
(g) Sheria ya Bajeti, SURA 339
48.
Mheshimiwa
Spika, ili kuwezesha utekelezaji wa Miradi Mikubwa yenye
manufaa kwa Taifa kama vile Ujenzi wa Miundombinu, Ununuzi wa Ndege, Mabehewa
au Vichwa vya Treni, Miradi ya Umeme n.k, inapendekezwa kurekebisha Kanuni ya
23 ya Kanuni za Sheria ya Bajeti za mwaka 2015, ili kumpa Mamlaka Mlipaji Mkuu
wa Serikali kuongeza muda wa matumizi ya fedha za mwaka wa fedha uliomalizika
hususan zinazohusu Miradi ya Maendeleo. Hivi sasa Kanuni hii imeweka ukomo wa
miezi mitatu (3) wa kutumia fedha za mwaka wa fedha uliomalizika, ambapo baada
ya muda huu wa miezi mitatu (3) kuisha, fedha hizo hupaswa kurejeshwa Mfuko
Mkuu wa Serikali. Utaratibu huu wa sasa
wa kurejesha fedha za miradi, Mfuko Mkuu wa Serikali baada ya kumalizika kwa
muda wa miezi mitatu (3) unaathiri utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kutokana
na kutokuwepo kwa fedha za kulipia Hati za Madai hadi hapo mgao mpya wa fedha
utakapotolewa kwenye bajeti ya mwaka mpya wa fedha.
(h) Marekebisho madogo madogo katika baadhi
ya Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali.
49.
Mheshimiwa
Spika, napendekeza kufanya marekebisho mengine madogo madogo
yasiyo ya kisera katika sheria mbalimbali za kodi pamoja na sheria nyingine ili
ziwe sanjari na azma ya kurahisisha utekelezaji wake. Marekebisho hayo
yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 na Matangazo ya
Serikali (Government Notices).
(i) Kuanza utekelezaji wa Mpango wa
Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa biashara (Blueprint) kwa kurekebisha Ada na Tozo
mbalimbali.
50.
Mheshimiwa
Spika, kufuatia matokeo ya mkutano wa Mh. Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini uliofanyika ikulu,
Dar es salaam, tarehe 7 Juni, 2019, Serikali inapendekeza kufuta au kupunguza
ada na tozo hamsini na nne (54)
zinazotozwa na Wizara, Idara na taasisi zinazojitegemea ili Kuondoa kero na urasimu
kwa wafanyabiashara na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Hatua hizi
ni sehemu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango
wa kuboresha Mfumo wa udhibiti wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to
Improve the Business Environment).
Aidha, hatua hii imelenga kuondoa muingiliano wa majukumu ya kiutendaji
baina ya Wizara, Taasisi na Mamlaka za Udhibiti. Marekebisho hayo yataainishwa
katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 na Matangazo ya Serikali
(Government Notices). Marekebisho hayo yatajumuisha:-
I.
Mamlaka ya Dawa (TFDA)
(a)
Kufuta tozo za Kushikilia usajili wa dawa za
chanjo (Vaccines and Biologicals) inayotozwa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani
mia hamsini (150); dawa za mitishamba (Herbal medicines) inayotozwa kwa kiasi
cha Dola za Kimarekani mia hamsini (150); vifaa tiba (medical devices)
inayotozwa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani mia moja (100); vitendanishi
(diagnostics) inayotozwa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani mia mbili hamsini
(250); chakula kinachotozwa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani mia moja (100); vipukusi
(antiseptics and diagnostics) vinavyotozwa kwa kiasi cha shilingi laki moja
(100,000/=); na tozo za bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi (retention fees
for domestic products);
(b)
Kufuta tozo za Kudurufu cheti cha usajili wa
vitendanishi inayotozwa kwa kiasi cha Dola za Kimarekani mia moja (100);
(c)
Kufuta tozo za ukaguzi wa maduka mapya ya
kuuzia vyakula inayotozwa kwa kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000);
(d)
Kufuta tozo za usajili wa maduka ya reja
reja ya dawa za mifugo kati ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) hadi shilingi
laki moja (100,000/=);
(e)
kufuta tozo ya ukaguzi wa viwanda vya samaki
nchini iliyokuwa inatozwa kwa kiwango cha kati ya shilingi laki mbili
(200,000/=) hadi shilingi laki mbili na elfu hamsini (250,000/=);
(f)
Kufuta tozo ya ukaguzi wa maduka mapya ya
samaki ya shilingi elfu hamsini (50,000/=); na
(g)
Kufuta tozo ya leseni ya mwaka ya biashara
ya samaki kati ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) hadi shilingi laki tatu
(300,000/=).
Lengo la hatua hizi ni
kuweka mazingira rafiki ya kibiashara na uwekezaji ili kuchochea uzingatiaji wa
sheria kwa hiari na kuongeza wigo wa wadau wanautumia huduma za TFDA (customer
base).
Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 2,500.0
II.
Shirika la Viwango Tanzania
Napendekeza kufanya
marekebisho ya Sheria ya Shirika la Viwango Tanzania kwa:-
(a)
Kufuta tozo ya shilingi elfu hamsini
(50,000/=) ya maombi ya alama ya ubora (TBS mark);
(b)
Kufuta tozo ya nembo ya ubora (TBS mark
guarantee) ya asilimia kumi na tano (15) ya tozo ya gharama za mwanzo za
ukaguzi wa ubora (transport costs and overhead fees);
(c)
Kufuta tozo ya dhamana ya cheti cha kutumia
nembo ya ubora (TBS mark licence). Tozo hii hutozwa kwa kiwango cha asilimia
hamsini (50) ya gharama za usafirishaji na upimaji wa Sampuli kutoka sokoni na
viwandani;
(d)
Kufuta tozo ya shilingi elfu hamsini
(50,000/=) ya ununuzi wa fomu ya maombi ya bidhaa zinazotoka nje kwa bidhaa
zote;
(e)
Kufuta tozo ya gharama za ugenzi
(calibration of equipment based on industrial metrology). Tozo hii hutozwa
kulingana na umbali wa sehemu (Kwa mfano Dar es salaam - chini ya umbali
wa kilometa 5 kutoka TBS ni shilling
elfu kumi (10,000/=); umbali wa kati ya kilometa 5 hadi 7 kutoka TBS ni shilingi
elfu hamsini (50,000/=); na umbali wa zaidi ya kilometa 7 kutoka TBS ni
shilingi laki moja (100,000/=); na
(f)
Kufuta tozo ya asilimia 0.2 ya gharama ya
mzigo na usafirishaji ya udhibiti wa vipodozi, vifaa tiba ikiwa ni pamoja na
kondomu, mabomba ya sindano (syringes), glavu (gloves), pamba (cotton wool) na
bendeji (bandage).
Lengo la hatua hii ni
kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara na wazalishaji, kupunguza gharama katika
uendeshaji wa vifaa vya viwandani na kupunguza tozo za kero.
Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 2,687.4
Aidha, napendekeza kufanya
marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) kwenye eneo la usimamizi wa viwango ambao
unajumuisha ubora na usalama wa chakula na vipondozi ili Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) liendelee kusimamia eneo la chakula na vipodozi kwa ujumla kama
ilivyo kuwa tangu mwaka 1975. Hivyo basi, Shirika la Viwango litachukua jukumu
la kuunganisha utaratibu wa usajili wa majengo (premises registration), Usajili
wa bidhaa (product registration), udhibiti wa bidhaa (certification) na
udhibiti wa bidhaa kutoka nje (import inspection) kwa ujumla. Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) itaendelea kusimamia madawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi
ili kuongeza ufanisi katika eneo hili.
III.
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
Napendekeza kufanya
marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Majumbani na
Viwandani, Sura 182 kwa kufuta tozo zifuatazo:-
(a)
Kufuta tozo ya huduma ya kusitisha kibali
cha awali na kutoa kibali kipya inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani
hamsini (50);
(b)
Kufuta tozo ya huduma ya kubadilisha taarifa
za kibali inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani hamsini (50);
(c)
Kufuta tozo ya usajili wa kampuni ya Wakala
wa Forodha (Clearing Agent) inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani mia
tano (500) kila kipindi cha usajili;
(d)
Kufuta tozo ya huduma ya kubadilisha taarifa
za usajili inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani mia moja (100) kila
kipindi cha usajili;
(e)
Kufuta tozo ya huduma ya ukaguzi wa dharura
inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani mia tatu (300) kwa kila ukaguzi;
(f)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili (maintenance fee) kwa viwanda vya magodoro
inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani elfu moja (1,000) kila mwaka;
(g)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa viwanda vya rangi inayotozwa kwa kiwango
cha Dola za Kimarekani elfu moja (1,000) kwa mwaka;
(h)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa viwanda vya nguo inayotozwa kwa kiwango
cha Dola za Kimarekani elfu moja (1,000) kwa mwaka;
(i)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa viwanda vya ngozi inayotozwa kwa kiwango
cha Dola za Kimarekani elfu moja (1,000) kwa mwaka;
(j)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa viwanda vya plastiki inayotozwa kwa
kiwango cha Dola za Kimarekani elfu moja (1,000) kwa mwaka;
(k)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa viwanda vinginevyo vikubwa inayotozwa kwa
kiwango cha Dola za Kimarekani elfu moja (1,000) kwa mwaka;
(l)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa viwanda vidogo vidogo inayotozwa kwa kiwango
cha Dola za Kimarekani mia mbili hamsini (250) kwa mwaka;
(m) Kufuta
ada ya kulinda cheti cha usajili kwa
wasambazaji wakubwa inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani elfu moja
(1,000) kwa mwaka; na
(n)
Kufuta ada ya kulinda cheti cha usajili kwa
wasambazaji wa kati inayotozwa kwa kiwango cha Dola za Kimarekani mia tano
(500) kwa mwaka.
Aidha, napendekeza pia
kufanya marekebisho ya Sheria ya
Usimamizi na udhibiti wa Kemikali za Majumbani na Viwandani Sura 182, ili
kurekebisha viwango vya tozo kama ifuatavyo:-
(a)
Kutoza tozo ya shilingi elfu arobaini
(40,000/=) ya usajili wa kemikali kwa kila kemikali kwa kipindi cha usajili
badala ya Dola za Kimarekani ishirini (20);
(b)
Kutoza tozo ya shilingi laki mbili
(200,000/=) kwa wafanyabiashara wakubwa na shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa
wajasiriamali wadogo kwa kila cheti cha usajili (Certificate holder
registration);
(c)
Kutoza tozo ya shilingi laki mbili
(200,000/=) badala ya Dola za Kimarekani mia moja (100) kwa wafanya biashara
wakubwa na shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa wafanyabiashara wadogo kwa
Usajili wa eneo la kuhifadhia kemikali (Premises registration);
(d)
Kutoza tozo ya shilingi laki tatu
(300,000/=) kwa siku kwa kila mtu ya
kuchambua kemikali chakavu badala ya Dola za Kimarekani mia tatu (300);
(e)
Kutoza tozo ya shilingi laki mbili
(200,000/=) ya kuainisha na kuidhinisha njia ya kuteketeza kemikali badala ya
Dola za Kimarekani mia tano (500);
(f)
Kutoza tozo ya shilingi laki tatu
(300,000/=) kwa kila siku kwa kila mtu ya
kusimamia kupakia, kusafirisha, kushusha na kuteketeza kemikali chakavu
badala ya Dola za Kimarekani mia tatu (300);
(g)
Kutoza tozo ya shilingi laki tatu
(300,000/=) ya ukaguzi wa maghala na sehemu za kuhifadhia kemikali badala ya
Dola za Kimarekani mia mbili (200);
(h)
Kutoza tozo ya shilingi laki moja na elfu
hamsini (150,000/=) kwa kila siku kwa kila mtu kwa tathmini ya njia za Usafirishaji na ukaguzi
wa dharura (Transportation Routes assessment and emergency inspection) badala
ya Dola za Kimarekani mia moja (100);
(i)
Kutoza tozo ya shilingi laki moja na elfu
hamsini (150,000/=) kwa siku kwa kila mtu kwa kusindikiza kemikali hatarishi
badala ya Dola za Kimarekani mia moja (100); na
(j)
Usafirishaji wa kemikali hatarishi na
kemikali zingine ndani na nje ya nchi utatozwa tozo kama zilivyoainishwa kwenye
Jedwali Na. 3 hapa chini:-
Jedwali Na 3.
Kiasi cha kemikali kinachosafirishwa kwa MT
|
Ada
ya sasa
(USD)
|
Ada
inayopendekezwa
(USD)
|
Kati
ya 0.1 - 10
|
1-2 kila MT
|
10
|
10.1
- 200
|
1
kila MT
|
|
201
- 1000
|
400
|
|
1001
- 5000
|
600
|
|
5001
- 10,000
|
800
|
|
10,001-
20,000
|
1,200
|
|
20,001-
40,000
|
1,500
|
|
40,001+
|
2,000
|
Aidha, ili kutimiza matakwa
ya sheria ya kutumia fedha za kitanzania, tozo zote zilizokuwa zinatozwa kwa
dola za kimarekani zitatozwa kwa fedha za Kitanzania isipokuwa kwa shehena za
kemikali zinazoenda nje ya nchi (On-transit). Lengo la hatua hizi ni kupunguza
wingi na ukubwa wa tozo ili kuweka mazingira bora ya biashara nchini. Aidha,
mizigo ya kemikali inayopitishwa katika bandari ya Dar es salaam itaongezeka na
hivyo kuongeza mapato ya Serikali.
Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 450.0
IV.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Sekta ya Mifugo
Napendekeza kufuta tozo
mbalimbali kwenye Sekta ya mifugo kama ifuatavyo:-
(a)
Kufuta tozo ya shilingi 5,000 ya vibali vya
vyombo vya kusafirisha maziwa chini ya lita 51;
(b)
Kufuta tozo ya shilingi 50,000 ya usajili wa
vituo vya kukusanyia maziwa lita 201 kwa siku;
(c)
Kufuta tozo ya shilingi 5,000 ya usajili wa
wazalishaji wa maziwa chini ya lita 51 kwa siku;
(d)
Kufuta tozo ya shilingi 500,000 ya usajili
wa wasambazaji wa pembejeo za maziwa;
(e)
Kufuta tozo ya shilingi 15,000 ya usajili wa
wafugaji wadogo wa mifugo ya nyama;
(f)
Kufuta tozo ya shilingi 50,000 ya usajili wa
wafugaji wa kati wa mifugo ya nyama;
(g)
Kufuta tozo ya shilingi 75,000 ya usajili wa
wafugaji wakubwa wa mifugo ya nyama;
(h)
Kufuta tozo ya shilingi 20,000 ya usajili wa
wasimamizi wa minada ya awali;
(i)
Kufuta tozo ya shilingi 30,000 ya usajili wa
wasimamizi wa minada ya upili na mipakani;
(j)
Kufuta tozo ya shilingi 50,000 ya usajili wa
minada ya upili na mipakani;
(k)
Kufuta tozo ya shilingi 30,000 ya usajili wa
wafanyabiashara wa minada ya awali;
(l)
Kufuta tozo ya shilingi 60,000 ya usajili wa wafanyabiashara wa minada ya
upili na mipakani;
(m) Kufuta
tozo ya shilingi 100,000 ya usajili wa wafanyabiashara wa nyama na bidhaa zake
nje ya nchi;
(n)
Kufuta tozo ya shilingi 1,000 ya kibali cha
kusafirisha kuku nchini (vifaranga 100 kwa siku moja); na
(o)
Kufuta tozo ya shilingi 200 ya kibali cha
kusafirisha kuku mkubwa nchini.
Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha takribani shilingi milioni 16,689.8
V.
Wizara ya Maliasili na Utalii
Napendekeza kufuta ada ya
Leseni ya kufanya biashara ya Utalii inayohusisha uwindaji wa kitaalamu
(professional hunting) iliyokuwa inatozwa kwa dola za kimarekani mia mbili (USD
200) kwa raia wa Tanzania na dola za kimarekani elfu moja (USD 1000) kwa raia
wa kigeni. Lengo la hatua hii ni kupunguza tozo zinazotozwa katika sekta ya
utalii, na kuvutia watalii. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali
kwa kiasi cha takribani Dola za Kimarekani elfu themanini (USD 80,000).
VI.
Wizara ya Maji
Napendekeza kufuta ada ya
matumizi ya maji kwa watumiaji wenye visima nyumbani ambayo ilikuwa inatozwa
kuanzia shilingi laki moja (100,000/=) na kuendelea kulingana na matumizi ya
maji. Lengo la kufuta tozo hiyo ni kupunguza gharama kwa wananchi wanaochimba
visima vya maji kwa matumizi binafsi nyumbani na kuwezesha upatikanaji wa maji
hayo kwa gharama nafuu. Hata hivyo, ili kudhibiti uchimbaji holela wa visima,
itabidi visima hivyo viendelee kusajiliwa na Bodi za Maji za Mabonde.
Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 1,961
Aidha, Serikali itaendelea
kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa Mpango wa kuboresha Mfumo wa udhibiti wa Biashara (BLUEPRINT). Lengo ni kuendelea kuweka
mazingira bora ya kuvutia uwekezaji, katika kipindi cha muda wa kati na muda
mrefu. Hatua hii inatoa fursa kwa wajasiriamali kuanzisha biashara mpya zitakazo
ongeza ajira na kukuza uchumi. Kwa kuzingatia kuwa, Serikali imewekeza katika
kuboresha mazingira ya udhibiti wa mazingira ya biashara, kupitia mpango wa
BLUEPRINT, hivyo basi, ni matarajio na wito wa Serikali kwamba wawekezaji wa
ndani na nje, watachangamkia fursa hii kwa kuanzisha na kuendeleza uwekezaji
mpya ili kukuza faida za biashara na kuweza kulipa kodi stahiki kwa hiari na
kuongeza mapato ya Serikali.
(j) Hatua za Kisera na Kiutawala katika
Kuboresha ukusanyaji wa mapato
51.
Mheshimiwa
Spika, napendekeza kuweka utaratibu mpya wa kuondoa mizigo
bandarini ambapo wananchi wa kawaida wataruhusiwa kutoa mizigo yao bila ya kuwa
na ulazima wa kutumia Wakala wa Forodha (Clearing and Forwarding Agents). Hata
hivyo, utaratibu huu hautahusisha mizigo inayopitishwa hapa nchini kwenda nje
ya nchi (Transit Cargo). Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania itaandaa utaratibu
wenye kueleweka kwa urahisi ili kuwawezesha Wananchi kugomboa mizigo yao kwa
gharama nafuu zaidi na bila kuchelewa.
52.
Mheshimiwa
Spika, Serikali inapendekeza kuchukua hatua mbalimbali za
Kisera na Utawala kwa lengo la kuimarisha na kurahisisha ukusanyaji mapato.
Hatua hizo ni pamoja na:-
(i)
Ili
kuondoa malalamiko ya wafanyabiashara dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imeamua kuanzisha kitengo huru cha
kupokea malalamiko na taarifa za kodi (Office of Tax Ombudsman) ambacho
kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, kitengo hiki kitahusisha
kupokea na kupitia malalamiko ya taarifa za Kodi zitakazotolewa na walipakodi
au watu wenye nia njema. Baadhi ya majukumu ya Kitengo hiki ni kama yafuatayo:-
(a)
Kupokea malalamiko ya rushwa dhidi ya
watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania;
(b)
Kupokea malalamiko ya ukadiriaji wa Kodi na
uthamanishaji wa bidhaa usio wa haki wala uhalisia dhidi ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania;
(c)
Kupokea malalamiko ya matumizi ya nguvu
katika ukusanyaji kodi dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania;
(d)
Kupokea malalamiko ya ufungaji wa biashara
bila kufuata sheria na taratibu dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania; na
(e)
Kupokea malalamiko pamoja na kero nyingine
zinazofanana na hayo dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
(ii)
Ili
kuongeza ukusanyaji wa mapato ya kodi za ndani, serikali inakamilisha manunuzi
ya mfumo unganishi wa kielektroniki (Intergrated Domestic Revenue Adminstration
System- IDRAS) katika kukusanya kodi na mapato yasiyo ya kodi ili kuleta uwazi
na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato. Pia mfumo huu utarahisisha ulipaji wa
kodi na kupunguza rushwa miongoni mwa watumishi wasio waaminifu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania;
(iii)
Kuendelea
kusimamia matumizi ya mfumo wa
kukusanyia kodi wa kielektroniki (Electronic Fiscal Device Management System)
ambao umefanyiwa maboresho makubwa na kuanza kazi tangu tarehe 1 June, 2019,
ili kudhibiti na kubaini udanganyifu unaofanywa katika matumizi ya mfumo huo.
Aidha, hatua hii itadhibiti uvujaji wa mapato katika urejeshaji wa kodi ( Tax
refund), utoaji wa risiti bandia, n.k;
(iv)
Kutokana
na wimbi la vijana wengi kujihusisha na michezo ya kubahatisha na kusahau
majukumu ya ujenzi wa taifa, Serikali ikishirikiana na Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha imebuni na kutengeneza mfumo maalum ambao utatumika kudhibiti
uchezaji wa michezo hii (Responsible Gaming). Pia, Mfumo huu utatumika kudhibiti udanganyifu ambao
unafanywa na waendeshaji wa michezo ya kubahatisha ili Serikali ipate mapato
yake halali;
(v)
Kutokana
na malalamiko ya walipa kodi kuhusu ukadiriaji wa kodi na uthaminishaji wa
bidhaa usio na haki wala uhalisia, Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mapato
Tanzania kuanzisha dawati la kushughulikia mapingamizi ya makadirio ya kodi
ambapo pingamizi za uthamanishaji na utambuzi litashughulikiwa ndani ya masaa
ishirini na nne (24); na
(vi)
Kutoa
unafuu wa kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita (6) kuanzia wakati
mfanyabiashara au mwekezaji anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).
Hatua hii inatofautiana na hali ilivyo sasa ambapo mfanyabiashara anapopewa TIN
anaanza kufanyiwa tathmini (tax assessment) ya mapato yake ya biashara na
kutakiwa kulipa kodi. Hatua hii itawezesha wafanyabiashara na wawekezaji wapya
kupata muda wa kujiandaa na mahitaji yanayotakiwa katika shughuli wanazofanya
na kuondoa usumbufu au dhana ya woga wakati wa kuanzisha biashara. Mfano kuna
mahitaji ya Leseni ya biashara na vibali vingine muhimu.
(k) Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya
za Kodi.
53.
Mheshimiwa
Spika, hatua hizi za kodi zinazopendekezwa zitaanza
kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2019, isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo.
V. SURA
YA BAJETI KWA MWAKA 2019/20
54.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia shabaha, malengo
pamoja na sera za bajeti kwa mwaka 2019/20, Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla
ya shilingi trilioni 33.11 zinatarajiwa kukusanywa na
kutumika katika kipindi hicho. Jumla ya mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya
Halmashauri) yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 23.05, sawa na asilimia 69.6
ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi
ya jumla ya shilingi trilioni 19.10 sawa na asilimia 12.9 ya Pato la Taifa. Mapato
yasiyo ya kodi kwa mwaka 2019/20 yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 3.18 na
mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni Shilingi bilioni 765.5.
55.
Mheshimiwa Spika, Serikali inatarajia kukopa shilingi
trilioni 4.96 kutoka soko la ndani. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 3.46 ni kwa ajili ya kulipia
hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na kiasi cha Shilingi bilioni 1.50
sawa na asilimia 1.0 ya Pato la Taifa ni mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia
miradi ya maendeleo. Kwa lengo la kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi ya
miundombinu, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 2.32 kutoka soko la
nje kwa masharti ya kibiashara.
56.
Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo
wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 2.78 ambayo ni asilimia 8 ya bajeti.
Misaada na mikopo hii inajumuisha miradi ya maendeleo shilingi trilioni 2.31;
Mifuko ya Pamoja ya Kisekta shilingi bilioni 199.5; na Misaada na Mikopo nafuu
ya Kibajeti (General Budget Support-GBS) shilingi bilioni 272.8.
57.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Serikali
inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 33.11 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha
hizo, shilingi trilioni 20.86 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa
ni asilimia 63.0 ya bajeti, ikijumuisha Shilingi trilioni 9.72 kwa ajili ya
ulipaji wa deni la Serikali na shilingi trilioni 7.56 kwa ajili ya mishahara.
Aidha, shilingi trilioni 3.58 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (Other
Charges-OC) ikijumuisha shilingi bilioni 460.5 kwa ajili ya matumizi yatokanayo
na vyanzo vya ndani vya Halmashauri. Aidha, kwa mwaka 2019/20, Serikali imetenga
fedha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na maandalizi ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
58.
Mheshimiwa Spika, matumizi ya maendeleo yanatarajiwa
kuwa shilingi trilioni 12.25, sawa na asilimia 37.0 ya bajeti yote, ambapo
kiasi cha Shilingi trilioni 9.74 ni fedha za ndani na shilingi trilioni 2.51 ni
fedha za nje. Kati ya fedha za maendeleo zilizotengwa, shilingi trilioni 2.48
ni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge; shilingi trilioni 1.44 ni kwa ajili ya mradi wa
kufua umeme Mto Rufiji; shilingi bilioni 788.8 ni kwa ajili ya mifuko ya Reli,
Maji na REA; shilingi bilioni 450 ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu
ya juu; na shilingi bilioni 288.5 kwa ajili ya elimu msingi bila ada. Aidha,
Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 600.0 kwa ajili ya kulipa madeni
yaliyohakikiwa ya watumishi, watoa huduma na makandarasi wa barabara, maji na
umeme.
59.
Mheshimiwa Spika, kwa
kuzingatia mfumo wa bajeti kama nilivyoeleza, sura ya bajeti kwa mwaka 2019/20
ni kama inavyooneshwa katika Jedwali A.
Jedwali A: Mfumo wa Bajeti ya Mwaka
2019/20
Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango
VI. HITIMISHO
60.
Mheshimiwa Spika, bajeti ni nyenzo ya kufikia matarajio ya wananchi wetu.
Hivyo, katika kuandaa bajeti hii, Serikali iliwashirikisha wadau mbalimbali
wakiwemo, Kamati ya Bunge ya Bajeti, wafanyabiashara, taasisi za umma na
binafsi, wananchi wa kawaida, na wataalam wa kodi hususan wale walioshiriki vikao
vya kazi vya kikosi kazi cha maboresho ya kodi (Task Force and Think Tank) kujadili na kushauri juu ya mapendekezo
ya maboresho ya kodi na tozo mbalimbali. Baadhi ya wadau walituletea maoni na
ushauri kwa maandishi au barua pepe. Nakiri kuwa walitupatia mrejesho ambao
umesaidia kuboresha será na vipaumbele
vya nchi yetu kwa mwaka 2019/20 na siku zijazo. Napenda kwa niaba ya
Serikali kuwashukuru sana kwa michango hiyo mizuri ambayo tumejitahidi
kuizingatia. Ni matarajio ya Serikali kwamba wadau hao wataendelea kufanya
hivyo katika mchakato wa bajeti zitakazofuata.
61.
Mheshimiwa Spika, bajeti ya 2019/20 inahusu kuendeleza juhudi za kujenga
msingi wa uchumi wa viwanda ili kupanua fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa
uchumi wa Taifa na ustawi endelevu wa jamii
na hatimaye kuondokana na umaskini, ujinga na maradhi. Hususan, bajeti hii
imelenga:
(i)
Kuimarisha
na kujenga miundombinu ya kisasa ili kuongeza uwezo wa Taifa katika uzalishaji
viwandani hasa vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa nchini
na kutoa huduma bora (afya, elimu na maji) kwa wananchi. Aidha, miundombinu hiyo
itasaidia kuongeza biashara nchini, kikanda na kimataifa;
(ii)
Kujenga
mazingira mazuri ya kufanya biashara na uwekezaji kwa kushughulikia changamoto
zilizobainishwa katika mpango wa kuboresha mazingira ya biashara (Blueprint);
(iii)
Kuimarisha
kilimo (uzalishaji wenye tija na masoko ya mazao, ufugaji, uvuvi, na misitu)
kwa kuzingatia umuhimu mkubwa wa sekta hii katika uchumi wa Taifa (chakula,
ajira, kipato cha mwananchi, mchango katika fedha za kigeni na muunganiko wa
sekta hii na maendeleo ya viwanda);
(iv)
Kudumisha
amani na usalama katika Taifa; na Kujenga misingi ya Taifa kujitegemea kiuchumi
62.
Mheshimiwa Spika, safari ya kuijenga Tanzania mpya imeiva lakini haitakuwa
rahisi hasa tukizingatia mabadiliko yanayoendelea katika uchumi wa dunia,
ushindani mkali wa kibiashara, mabadiliko ya haraka ya teknolojia na demografÃa
na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo, bahati nzuri
ni kuwa, katika historia ya nchi yetu, Watanzania ni watu jasiri katika
mapambano dhidi ya changamoto zinazojitokeza na kila wakati zilipojitokeza
tulizishinda kwa kutumia ubunifu na
nguvu ya umoja wa Watanzania.
63.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa tuko imara zaidi chini ya uongozi shupavu wa
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Uchumi wetu unaendelea kukua kwa
kasi kubwa, ambapo mwaka 2018 ulikua kwa asilimia 7.0 na kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi
kinazidi kupungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 26.4 mwaka
2017/18. Naamini pasipo shaka yoyote kwamba kwa umoja wetu, uongozi makini,
kufanya kazi kwa bidii na kwa kutumia rasilimali za nchi yetu vizuri,
tutaijenga Tanzania mpya, ambayo itakuwa kitovu kikuu cha uchumi (Economic hub)
katika ukanda wa Afrika Mashariki katika muda usiozidi miongo miwili ijayo.
64.
Mheshimiwa Spika, ninapoelekea mwisho wa hotuba hii, napenda kuchukua
fursa hii kuwashukuru Washirika wetu wa Maendeleo kwa misaada na mikopo nafuu
wanayoendelea kutupatia katika kutekeleza miradi na programu mbalimbali za
maendeleo nchini. Katika bajeti ya mwaka 2019/20, Washirika wa Maendeleo kwa
pamoja wanatarajia kuchangia jumla ya shilingi trilioni 2.78. Naomba niwatambue
kwa kuwataja mmoja mmoja: Nikianza na nchi za Canada, China, Denmark, Finland,
India, Ireland, Italia, Japan, Korea ya Kusini, Marekani, Norway, Poland,
Sweden, Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani, Uingereza, na Uswisi. Aidha,
zipo taasisi za kimataifa ambazo ni: Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki
ya Dunia, Arab Bank for Economic Development in Afrika (BADEA), Global Fund,
Kuwait Fund, Abu Dhabi Fund, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), Benki ya Uwekezaji
ya Ulaya (EIB), OPEC Fund, Global Environmental Facility (GEF), Shirika la
Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA), Mfuko wa kukinga Hatari ya Kimazingira
(GRMF), Climate Development Special Fund, African Legal Support Facility
(ALSF), Dignity, Global Agriculture and Food Security Program (GAFSP),na
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo UNICEF, IFAD, UNDP, UNFPA, Shirika la
Chakula na Kilimo (FAO), na United Nations Environment Programme (UNEP). Napenda
pia kutambua uhusiano mzuri tulionao na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Ni
matarajio yetu kuwa misaada ya kiufundi na fedha zilizoahidiwa na marafiki zetu
hawa zitatolewa kwa wakati na kwa kiasi kilichoahidiwa. Nasi kwa upande wa
Serikali tunaahidi kutumia misaada hiyo kama ilivyokusudiwa.
65.
Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hii kuwahimiza Waheshimiwa
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao na
taasisi za kimataifa hapa nchini Tanzania waongeze nguvu kukuza biashara kati
ya nchi zao na nchi yetu na kuhamasisha wenye mitaji toka nchi zao kuja
kuwekeza hapa Tanzania. Tanzania ni salama kwa uwekezaji wenye faida kwao na
kwetu. Aidha, wafanye jitihada zaidi kuhamasisha watalii kuja kujionea vivutio
vya utalii, ambavyo ni fahari ya Tanzania.
66.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano inatambua na kuthamini michango
yao katika maendeleo ya Taifa letu ili mradi isiambatane na masharti
yanayohatarisha uhuru wa Tanzania (national sovereignity), au kwenda kinyume na
mila na desturi zetu. Hata pale ambapo Serikali au mihimili mingine imefanya
maamuzi ambayo hawakubaliani nayo, ni vema na haki washirika wetu wa maendeleo watupe
muda wa kuyatafakari na kujadiliana nao kwa staha badala ya kuishinikiza
Serikali ibadili uamuzi wake ndipo watoe fedha, jambo ambalo halikubaliki hata
kidogo.
67.
Mheshimiwa Spika, kwa Watanzania wenzangu, napenda kuwasisitiza tuendelee
kushikamana katika kuijenga Tanzania mpya. Tuwe wazalendo na tena tukae macho
daima kulinda na kutetea maslahi ya Taifa letu. Tuongeze bidii kufanya kazi.
Enzi za kutegemea wajomba hazipo tena na habari njema ni kuwa: “Tukiamua Tunaweza”
na Serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
imethibitisha ukweli huo.
68.
Mheshimiwa Spika, naomba kwa niaba ya Serikali kupongeza mchango mkubwa wa
wafanyabiashara na wananchi wote ambao wamelipa kodi kwa mujibu wa sheria.
Aidha, napenda kutambua mchango adhimu wa mashirika na taasisi ambazo Serikali
ina hisa yaliyotoa gawio au asilimia 15 ya mapato ghafi kuingia katika Mfuko
Mkuu wa Hazina. Katika mwaka ujao wa fedha, Serikali inayataka mashirika yote
ya umma na taasisi ambazo Serikali ina hisa kuhakikisha kuwa wanatoa gawio au
mchango wa asilimia 15 ya mapato ghafi na Msajili wa Hazina asimamie kikamilifu
utekelezaji wa maagizo haya ya Serikali.
69.
Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu, mwezi Oktoba mwaka huu wa 2019
tutafanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Serikali kwa upande wake imejipanga
kikamilifu katika maandalizi ikijumuisha mahitaji ya kibajeti kwa ajili ya kufanikisha
uchaguzi huo. Ninawasihi wananchi wote wenye sifa wajitokeze kutumia haki yao
ya msingi ya kupiga kura. Aidha, katika kuchagua viongozi wa ngazi hiyo,
tafuteni Watanzania wenye sifa zifuatazo:
(i)
Awe mchapakazi mwenye kujitoa
sadaka kuwatumikia watu, hasa wananchi wa kawaida;
(ii)
Awe mwepesi kuona, kusikiliza
na kuguswa na shida za wananchi wake. Tena awe jasiri katika kupigania haki za
wanyonge na awe na uwezo na ubunifu katika kutatua kero za wananchi hao;
(iii)
Awe mwadilifu, anayechukia na
kupiga vita rushwa na ufisadi kwa matendo;
(iv) Anayetambua
fursa zilizopo katika eneo lake, kubuni mikakati ya kuwaendeleza wananchi anaowaongoza
na kuwatia watu wake hamasa ya kuthubutu kutumia fursa hizo;
(v)
Awe mtetezi hodari wa kulinda
mazingira na mpambanaji dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi;
(vi) Mwenye kutoabudu
nyadhifa; anayetambua kuwa nafasi na vyeo tulivyopewa ni vya muda tu. Ni vya
kupita! Thamani halisi ya kiongozi ni kufanya kazi kwa bidii na kuacha
kumbukumbu nzuri kwa ustawi wa eneo analoliongoza na Taifa kwa ujumla;
(vii) Awe kama mchezaji
mzuri wa kiungo katika timu ya ushindi, anayetambua kwamba mkono mmoja hauwezi
kupiga makofi ya shangwe;
(viii) Awe mwenye
kutambua kwamba kazi za kiongozi zina maana sana kwa kuwa zinamwezesha kubadilisha
maisha ya maelfu ya Watanzania, hasa wanyonge, kuwa bora zaidi;
(ix) Awe na uwezo
wa kuwaeleza wananchi kinaganaga kuhusu Serikali yao inawapeleka wapi na wajibu
wa kila mmoja ili waendelee kuiunga mkono; na
(x)
Awe anatoka ndani ya chama cha
siasa kinachotetea maslahi na haki za wanyonge na chama hicho ni CCM!
Naomba nikiri kuwa, sifa hizi nilizozitaja nimeziazima kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ridhaa
yake!
70.
Mheshimiwa Spika, nawaomba viongozi wote wa dini pamoja na waumini wote
kila mmoja kwa imani yake, tuendelee kumwombea Rais wetu mpendwa Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia afya njema,
hekima, busara na kumwongoza kwa kila jambo alifanyalo kuliletea Taifa letu
maendeleo.
71.
Mheshimiwa Spika, naomba nitumie
fursa hii kuwashukuru viongozi wenzangu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambao
wamekuwa msaada mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara na maandalizi
na uratibu wa bajeti hii ya Watanzania. Kipekee ninawashukuru Mheshimiwa Dkt.
Ashatu K. Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye ni Mbunge mahiri wa
Jimbo la Kondoa; Katibu Mkuu HAZINA na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bwana Doto M.
James, pamoja na Naibu Makatibu Wakuu, Bi. Amina Kh. Shaaban, Dkt. Khatibu M. Kazungu na Bwana Adolf H.
Ndunguru pamoja na watumishi wa ngazi zote wa Wizara ya Fedha na Mipango. Vile
vile, ninamshukuru Profesa Florens D. Luoga, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
pamoja na Naibu Gavana Dkt. Yamungu Kayandabila, Dkt. Bernard Kibesse na Bwana
Julian Raphael Banzi kwa kusimamia vema sekta nyeti ya fedha. Kwa nafasi ya
kipekee, napenda nimpongeze Dkt. Edwin Mhede kwa kuteuliwa na Rais kuwa
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Ni matumaini yangu na ya
Watanzania kuwa atakuwa chachu ya kujenga taswira mpya ya TRA itakayoongeza
mapato ya Serikali bila manyanyaso kwa wafanya biashara.
72.
Mheshimiwa Spika,
ninawashukuru viongozi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ofisi ya Msajili wa Hazina na Ofisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yao.
Nawashukuru Wakuu wote wa Idara na Vitengo, Taasisi na Wakala za Serikali
zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na wafanyakazi wake wote kwa
kazi nzuri wanazofanya na kuendelea kunipa ushirikiano wa dhati katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa
ufanisi wa hali ya juu.
73.
Mheshimiwa Spika, niwashukuru pia wananchi wenzangu wa Wilaya ya Buhigwe
na mkoa wetu wa Kigoma ambao walinilea na kunifundisha kufanya
kazi. Mwisho kabisa naishukuru familia yangu, hususan mke wangu mpenzi na
rafiki yangu Mbonimpaye, watoto, wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki zetu wote tuliopewa
na Mungu. Asanteni kwa kuniombea msaada wa Mungu katika kazi hii, usiku na
mchana. Nami ninasema kwa kila mmoja wao:
“Bwana akubarikie na kukulinda,
Bwana akuangazie nuru za uso wake, na
kukufadhili,
Bwana akuinulie uso wake, na kukupa
amani”
Hesabu
6: 24-26.
Nimalizie kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa baraka
zake na kuniwezesha kuwasilisha hotuba hii. Aidha, apende kuendelea kunijalia
uwezo na unyenyekevu wa kulitumikia Taifa letu na wananchi wake kwa uadilifu. Asanteni
sana Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kwa kunisikiliza.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU
IBARIKI TANZANIA
74.
Mheshimiwa Spika,
naomba kutoa hoja.
Comments
Post a Comment