Featured Post

NHIF TANGA YATUMIA MAADHIMISHO YA MEI MOSI KUWAKUMBUSHA WAAJIRI KUTOA MICHANGO YA WATUMISHI WAO


 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Happines Sima akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo.

 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto ni Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Tanga Happines Sima akiweka sawa mwamvuli wakipita mbele ya mgeni rasmi
 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)



MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga umetumia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi dunia (Mei Mosi) kuwakumbusha waajiri kuhakikisha wanatoa michango kwa ajili ya watumishi wao.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Happines Sima ambapo aliwataka waajiri kuzingatia suala hilo.
Alisema pia wametumia fursa hiyo kuweza kuhamasisha waajiri ambao watumishi wao ambao hawajajiunga na mfuko huo wajiunge ili waweze kunufaika na fursa zilizopo ndani ya mfuko huo.
“Lakini pia katika maadhimisho haya tumeweka banda letu ili kuweza kuwasikiliza wafanyakazi na kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili “Alisema Meneja huyo.
Hata hiyo aliwataka wazazi na walezi kuwaandikisha watoto wao kwenye mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu pindi wanapougua.

Comments