Featured Post

DC KASESELA : KAMPUNI YA TIGO IMEOKOA MAISHA YA VIJANA KWA KUAJILI VIJANA WENGI HAPA NCHINI.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ameipongeza kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa Tigo kwa kuajili wafanyakazi wengi vijana hapa nchi na kuongeza wigo wa upatikaji wa ajira na kuokoa vijana wengi kukosa ajira mtaani.

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amezindua duka la huduma kwa wateja la kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa Tigo lililopo manispaa ya Iringa mtaa wa miomboni
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akipata huduma kutoka kwa mfanyakazi wa duka la huduma kwa wateja la kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa Tigo lililopo manispaa ya Iringa Mtaa wa Miyomboni.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ameipongeza kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa Tigo kwa kuajili wafanyakazi wengi vijana hapa nchi na kuongeza wigo wa upatikaji wa ajira na kuokoa vijana wengi kukosa ajira mtaani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja lililopo miomboni manispaa ya Iringa,Kasesela alisema kuwa kamapuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira kwa vijana wengi kwenye vitengo mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo.

“Ukipita mtaani hata hapa tulipo utaona kuja vijana wamevaa sare za tigo na wanafanyabishara ya kuuza na kutoa huduma kwa wateja wa kampuni ya tigo hivyo nasema kuwa kamapuni hii katika wilaya yangu ya Iringa wanaongoza kwa kutoa ajira kwa vijana” alisema Kasesela

Kasesela aliongeza kwa kusema kuwa kuna vijana wengi wamejiajili au wamejiliwa na watu binafsi kwa ajili ya kutoa huduma ya Tigo Pesa,vifulushi mbalimbali ya mtandao huo jambo ambao limesaidia watu binafsi kuongeza ajira na kukuza mitaji ya biashara kwa kupitia mgongo wa kampuni hiyo.

“Leo hii ukipita kila mahali lazima ukutane na huduma ya Tigo Pesa na huduma nyingine za mtandao huu kutokana na watu binafsi kujiajili kwa kuuza na kununua biadhaa za kampuni hii ya Tigo ambazo sasa ndio yamekuwa maisha yao ya kila siku yanayowaingizia kipato” alisema Kasesela

Kasesela alisema, kampuni ya mawasiliano ya mtandao wa tigo ndio kamapuni inayoongoza kwa kutoa huduma nzuri na bora kwa watuaji wake na kuboresha huduma zake mara kwa mara kwa lengo la kutoa mawasiliano mazuri kwa watumiaji.

“Mimi nimekuwa nikitumia mtandao wa tigo toka mwazo ulipoanza kufanya kazi hapa nchi hivyo navyosema mtandao wa mawasiliano wa kampuni ya tigo unafanya vizuri namaanisha kwa kuwa nimetumia mitandao mingi sana” alsema Kasesela

Kasesela alisema kuwa uwepo wa duka la huduma kwa wateja katika manispaa ya Iringa limesaidia kuboresha,kutatua kero na kukuza huduma kwa watumiaji wa huduma za mtandao huo na kuwaomba waongeze maduka mangine kama hayo katika baadhi ya maeneo ya manispaa ya Iringa ili kutoa huduma kwa uhuru.

“Hili duka halitoshi maana hao wateja mia thelethini ni kidogo sana na wilaya ya Iringa inawakazi wengi na kwa asilimia kubwa wanatumia mtandao huu katika mawasilianoyao,hivyo lazima muongeze maduka mengine kwa kuwa manispaa ya Iringa ndio inahudumia karibia wakazi wote wa mkoa wa iringa kwa kupata huduma mbalimbali hivyo kuwa na duka moja haitoshi” alisema Kasesela

Kwa upande wake meneja mauzo wa kanda ya Iringa wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo Abraham Abbas alisema kuwa uzinduzi wa tuka hilo ndaini yamanispaa ya Iringa litarahisishia kutoa na kupata huduma bora kwa wateja wa mtandao huo.

“Moja ya jitihada za kampuni yetu ya Tigo ni kukikisha tunatoa huduma bora kwa wateja wetu hivyo kuzindua duka hili kutatusaidia kuongeza wateja wengi huku tukitoa huduma iliyo bora kwa wakati wengi wa mkoa wa Iringa” alisema Abbas

Abbas alisema kuwa duka hilo la huduma kwa mtaeja litakuwa linahudumia zaidi ya wateja mia thelathini kwa siku hivyo idadi hiyo itafanikisha kuboresha na kutoa huduma kifanisi zaidi.

“Tuwakaribishe wateja na wananchi ambao sio wateja kufika katika duka hili ili kujua huduma ambazo zinatolewa katika duka letu hili” alisema Abbas

Comments