- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MABADILIKO ya Tabianchi yameleta athari kubwa katika
maendeleo duniani ambapo kwa sasa ni vigumu kupatikana kwa vipindi vya mvua za
uhakika kama ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.
Maeneo mengi Tanzania yana shida ya upatikanaji wamvua za
uhakika na hivyo kuongeza uhaba wa maji hata kwa matumizi ya kawaida.
Kilimo cha kutegemea mvua sasa kimepitwa na wakati kwa
sababu ya mabadiliko ya tabianchi, hivyo ili kujiletea maendeleo ni vyema
kugeukia KILIMO ENDELEVU CHA UMWAGILIAJI.
Tunapoelekea kwenye TANZANIA YA VIWANDA tutambue kwamba
kilimo ndicho kinachozalisha malighafi, kwahiyo basi ni vyema tugeukia kilimo
cha umwagiliaji ambacho sasa tunaweza kukifanya kwa uhakika kwa kuchimba visima
virefu salama.
Taasisi za fedha zinazosapoti kilimo nazo hazitoi mikopo kwa
wakulima wanaotegemea anga linune mvua inyeshe, bali wanatazama watu wanaofanya
kilimo endelevu cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika zaidi. Kwahiyo kuchimba
kisima ndiyo suluhisho pekee linaloweza kutukomboa wakulima – iwe mmoja mmoja
au kwa vikundi vya ushirika.
KUPIMA MAJI
Tunapenda kuwaarifu wana-maendeleo wote kwamba tunatoa
huduma za kupima uwepo wa maji ardhini kabla ya kuchimba kisima.
Kumbuka kwamba, hata ukienda hospitalini, muuguzi lazima
atautafuta ulipo mshipa ili aweze kukudunga sindano. Kamwe hawezi kuchoma kila
sehemu ya mwili kwa sababu kufanya hivyo siyo tu anamuumiza mgonjwa, lakini pia
hawezi kutoa tiba sahihi kwa sababu dawa inapaswa kuingia katika mfumo wa damu
kupitia kwenye mshipa wa damu wa Vena.
Ndiyo sababu utakuta watoto wadogo wakati mwingine wauguzi
hulazimika hata kuwachoma sindano kichwani baada ya kuuona mshipa wa damu kwa
sababu mtu anapoumwa mara nyingi mishipa ‘hupotea’ au huwa haionekani kwa
urahisi.
Vivyo hivyo, kuchimba kila mahali ardhi kwa nia ya kutafuta
maji ni kuharibu ardhi pamoja na kuingia gharama zinazoepukika kwa sababu
mchimbaji wa kisima ukishamwambia kwamba achimbe mahali na mmekubaliana gharama
kwa kila meta moja, yeye atachimba na hata kama maji hayatapatikana lazima
ulipe gharama tu!
Sasa kwa kuepuka gharama hizi, sisi tunapima uwepo maji
katika ardhi unapotaka kuchimba kisima tukitumia vifaa vya kisasa kabia.
Vifaa vyetu vina uwezo mkubwa wa kupima uwepo wa maji katika
eneo la urefu wa meta 2000, yaani kilometa 2 (Long range water location
measurement) na kila cha meta 1200 yaani kilometa 1.2 (Geophysical) ambacho ni
kirefu sana.
Vifaa vyetu vina uwezo wa kutambua AINA YA MAJI kama MAJI
BARIDI (Fresh Water) au MAJI CHUMVI (Natural Water), wingi wake, mahali
yanakopatikana (kina) pamoja na wiani wake (density). Vifaa vyetu vinapima
kabisa hali ya chumvi (WATER SALINITY).
Tukishapima pia tunakupatia ushauri wa PUMP bora pamoja na
huduma nyingine kabla ya kuanza kuchimba.
Hasara za kutopima
Hasara za kutokupima kabla ya kuchimba ni kwamba, mtu
anaweza kuchimba na kupata maji, lakini kwa kuwa hakupima na kujua kiasi cha
maji, basi visima vingi utakuta vinakauka haraka wakati tayari watu
wamekwishaingia gharama. Matukio haya ni mengi sana.
Inawezekana kabisa kwa sababu amechimba bila kupima, maji
yaliyopatikana ni katika mikondo midogo iliyo ardhini (small underground
streams) ambayo inaweza kukauka. Lakini kama wangalipima na kujua kwa uhakika
wangeweza kujua maji yanapatikana katika kina gani.
Baadhi ya watu pia hukwepa gharama kuchimba visima virefu na
mara wanapochimba na kupata maji katika mikondo ya juu, basi huona hawana haja
ya kuendelea zaidi chini.
Kumbuka:
Upatikanajji wa maji ardhini unategemea na mikondo iliyopo
na ardhi yenyewe. Mfano, anayechimba bondeni kwenye mkondo wa maji anaweza
akachimba mita chache kulinganisha na anayechimba katika nchi kavu mbali na
bonde au mto. Hata maeneo ya mwambao wa Pwani nayo pia yanatofautiana – mmoja
anaweza kuchimba na kupata maji katika kina cha meta 60 lakini mwingine akapata
maji katika kina cha meta 100. Jambo mhimu hapa ni kupima. Tukikwambia kwamba
maji yatapatikana baada ya kupima ujue ni uhakika wa asilimia 90% utapata maji
ya uhakika kwa sababu vipimo vyetu ni vya kisasa na vya uhakika.
Muhimu:
Siyo kila mahali kunaweza kupatikana maji, hivyo
tunapogundua hivyo tunatoa ushauri wa kutochimba na kama kuna eneo jingine
mbadala unaweza kulipima.
Kama utahitaji tukufanyie utafiti peke yake (geo-physical
survey) halafu utatafuta mchimbaji (Driller) wewe mwenyewe hakuna shida pia.
Lakini tutakupa ushauri wa uhakika utakaokusaidia ili kisima chako kiwe cha
kudumu.
GHARAMA
Gharama zetu ni nafuu sana na tunaweza kwenda mahali popote
mkituhitaji. Aliye tayari kwa kupimiwa MAWASILIANO
YETU NI 0656-331974,
0787-426161, au +255 716
775334. Barua-pepe: maendeleovijijini@gmail.com.
GHARAMA ZA UCHIMBAJI
Kwa ujumla, gharama za uchimbaji wa kisima zinategemea
utafiti wa vipimo ulivyofanya.
Kwahiyo gharama za kuchimba kisima zinategemea mambo kadha
wa kadha:
- Kina
cha maji
Kama
nilivyosema awali, mahali pengine maji yanapatikana katika kina kifupi tu cha
meta 60, lakini sehemu nyingine unaweza kwenda hata meta 120 kulingana na
vipimo vinavyoonyesha yanakopatikana maji pamoja na wingi wake – water
quantinty.
- Aina
ya udongo
Hili
ni jambo la msingi sana. Mahali unakotaka kuchimba kisima ni lazima ijulikane
ni udongo wa aina gani. Gharama za uchimbaji zinatofautiana kutokana na aina ya
udongo. Kuchimba kwenye udongo wa mfinyanzi (CLAY SOIL) na udongo mchanganyiko
(MIXED SOIL) ni kazi kubwa kuliko kuchimba kwenye udongo wenye miamba (ROCKY
SOIL) au udongo wa kichanga/tifutifu (SANDY/LOAM SOIL).
Zipo mashine mbalimbali zinazotumika katika kuchimba visima
na katika maeneo yenye utata mashine yenye nyundo (HAMMER RIG) ndiyo inayofaa,
hasa kwenye miamba.
MAWASILIANO YETU NI 0656-331974, 0787-426161, au +255 716- 775334.
Barua-pepe: maendeleovijijini@gmail.com.
Comments
Post a Comment