- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA MWANDISHI WETU
UTAWALA bora
unaainishwa kuwa ni utawala unaofanya kazi kwa uwazi, unaowajibika, wenye
kutawala kwa sheria, wenye ufanisi na ulio na taasisi zilizo halali.
Katika hali
hiyo inaaminika kuwa utawala wa aina hiyo ni nyenzo muhimu kwenye
maendeleo ya kiuchumi ambapo utawala dhaifu husababisha uchumi kukua taratibu
ambapo wakati wengine wakikimbia utawala huo huwa unachechemea.
Utawala wa aina
hiyo ni muhimu kwenye kupata maendeleo na wakati huo huo ushirikishwaji
kidemokrasia kwa kuhakikisha kwamba maendeleo yanawiana na ni endelevu.
Taasisi za umma
zinatakiwa zimudu kusimamia rasilimali za umma na kuendesha masuala ya umma kwa
njia ambazo zinakuwa huru dhidi ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka
kwa kuzingatia utawala wa sheria na ambazo zinalinda na kukuza uelewa wa
watu kuhusu haki zao.
Kipimo halisi cha
utawala bora ni uwezo wa serikali kutambua haki za binadamu na kuipatia jamii
maendeleo kwa uwiano na kwa uendelevu. Utawala bora unatolewa kupitia uwazi,
uwajibikaji na ushirikishaji pamoja na mwitiko kwa mahitaji ya maskini, walioko
pembezoni na walio na uwakilishi mdogo.
Hata
hivyo dhana ya utawala bora imekuwa inapotoshwa na baadhi ya wapanga sera ambao
ndio wameshikilia taasisi za umma ili kukidhi matakwa au maslahi yao.
Wengi
wamekuwa wakitumia mwanya wa utandawazi kujenga mazingira ya rushwa na hivyo
kuifanya isambae kwa kiwango kikubwa. Sasa ndio hapo inapotokea shinikizo
kutoka nchi wahisani, mashirika ya misaada na wawekezaji kufuata sera
zinazaendana na ajenda za uliberali mamboleo.
Ajenda za
uliberali mambo leo zimezifanya nchi maskini kuwajibika kwa mashirika ya
misaada kuliko ambavyo zinawajibika kwa watu wao. Aidha nyingi zimekuwa
zinafanya shughuli zao ili kuwapendezesha wahisani kwa kujikomba na kuombaomba
na hata kuzigawa rasilimali kwa mikataba ya kilaghai.
Licha ya kwamba
utawala bora ni kichochea cha kukua kwa uchumi baadhi ya watendaji wamekuwa
wanawajibika kwa wawekezaji zaidi kuliko kwa wananchi wao na hali hiyo ndio imekuwa
inakwaza upatikanaji wa maendeleo.
Takwimu mbalimbali
duniani zinaonesha kuwa kukua kwa kasi na ufanisi mzuri kwenye maendeleo
kunahusiana na hali nzuri ya utawala bora na hususani kwenye ufanisi wa
serikali, ubora wa usimamizi, utawala wa sheria na udhibiti wa rushwa.
Kiungo kati ya
kukua kwa uchumi na vidokezo viwili vya ufanisi wa serikali na ubora wa
usimamizi ni mkubwa miongoni mwa nchi za Asia kuliko sehemu nyingine duniani.
Lakini inakuwa ni vigumu mno kuanzisha uhusiano wa kawaida kati ya vipengele
hivyo.
Mfano nchi nyingi
za Afrika, Tanzania ikiwemo zimekuwa zinajibainisha kuwa zilikuwa kwenye
kiwango sawa na nchi za Mashariki ya Mbali wakati zilipopata uhuru.
Lakini leo hii nchi kama Malaysia na Indonesia zimepiga hatua kubwa zaidi
ya maendeleo kuliko zile ambazo zilikuwa sawa kwenye miaka ya 1960.
Katika mazingira
hayo tafsiri inayoweza kupatikana kuhusu uhusiano kati ya ubora wa
serikali na ufanisi mkubwa kwenye maendeleo ni kwamba kila kimoja
kinachangia kukiboresha kingine.
Jambo jingine ni
kwamba umuhimu wa vipengele vya utawala bora unatofautiana ndani ya nchi
kulingana na hatua ya maendeleo iliyofikiwa. Katika nchi ambayo ina kipato cha
chini inatakiwa kupambana ili kuwa na serikali yenye ufanisi usimamizi
mzuri ulio bora na utawala wa sheria na udhibiti mkubwa wa rushwa.
Kwa mfano
inatakiwa kujiepusha na migogoro, kuzingatia haki za binadamu na kutoa
huduma muhimu za umma.
Ili nchi iweze
kuingia kwenye orodha ya nchi zilizo na kipato kikubwa inatakiwa kuboresha
utawala bora kwa kuzingatia na kuheshimu ushirikishwaji wa wananchi
na uwajibikaji wa serikali.
Nchi zilizo na
kipato cha kati na kikubwa zinaweza kunufaika na zawadi hii kubwa
kutokana na kutumia sauti za wananchi wake, uimara wa kisiasa na kuwepo kwa
taasisi zinazokubalika duniani.
Mfano wa taasisi
hizo ni pamoja na mfumo wa kisheria ulio na ufanisi, huduma zenye ubora wa hali
ya juu katika sekta ya afya na elimu na mfumo wa kifedha ambao umekaa katika
mpangilio unaokubalika.
Rushwa
kwenye mageuzi ya kuingia kwenye utawala bora hutofautiana
kulingana vidokezo binafsi vya maendeleo. Rushwa huzuia programu za huduma za
umma zisiwafikie maskini, wakati udhaifu kwenye mamlaka za usimamizi na
ufanisi serikalini huingia kwenye ulegevu.
Hali kadhalika
tabia za kijamii huathiri matokeo ya kijinsia na ushiriki kwenye masuala kama
ya usafi. Katika nchi ambayo inakabiliwa kwa mapana na soko kushindwa, serikali
ni lazima kuangalia namna kuondoa au kufanyia mageuzi vikwazo vyote
vinavyozuia maendeleo. Kwa kuwa nchi zinakuwa na mifumo tofauti ya
mazingira ya mwanzo huwa na namna tofauti ya kukabiliana na vikwazo,
zinahitaji kuwa na sera za mageuzi zinazofuatilia utawala bora.
Kama malengo ya
maendeleo yalivyo, vipimo vyote vya utawala bora lazima vifuatwe. Wapanga
sera si tu kwamba wanatakiwa kufuata kile ambacho ni rahisi kukitekeleza
lakini pia kwa utaratibu kwa kuangalia zaidi kwenye athari za maendeleo.
Taasisi zilizo na
ubora wa hali ya juu zitasaidia uchumi unaokua kwa haraka kuepuka
mitego inayotoka kwa nchi zilizo na kipato cha kati na kuwezesha uchumi
unaokua taratibu kuanzisha mazingira ambayo ni muhimu kwa uendelevu
wa ukuaji wa uchumi.
Utawala bora
unawezesha kuwepo kwa mgawanyo zaidi wa kazi ulio na ufanisi, tija kubwa kwenye
uwekezaji na utekelezaji wenye ufanisi wa sera za kiuchumi na kijamii na
njia nyingine muhimu za kukua kwa uchumi kuliko endelevu.
Comments
Post a Comment