Featured Post

WILAYA YA MANYONI MKOANI SINGIDA YATENGA ZAIDI YA EKARI 5000 KUPANDA MIKOROSHO MIPYA


 Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana akitazama moja ya mikorosho mipya iliyopandwa kwenye shamba mfano ambalo walilitembelea ili kuweza kuhamaisha zao hilo liliopo Kijiji cha Masigati.

Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini  yaliyofanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho ukafanyika akielezia mikakati ya wilaya yake kupanda zaidi ya ekari 5000 za mikorosho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana wakati wa ziara ya viongozi wa bodi kuhamasiha kilimo cha zao la Korosho kwenye maeneo mapya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akisistiza jambo kwa viongozi wa bodi ya Korosho nchini Afisa Kilimo Frank Mfutakamba kulia na Afisa Uhusiano Bryson Mshana kushoto wakati walipofanya ziara wilaya ya Manyoni kuhamasisha kilimo cha zao hilo.

Ofisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika  wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa bodi ya Korosho waliotembelea wilaya hiyo kushoto ni Afisa Uhusiano Bryson Mshana kulia ni Afisa Kilimo Frank Mfutakamba.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa kushoto akiagana na Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Frank Mfutakamba mara baada ya viongozi wa bodi ya korosho kumaliza mazungumzo naye.


NA MWANDISHI WETU, MANYONI
WILAYA ya Manyoni mkoani Singida imetenga zaidi ya ekari 5000 kwenye Kijiji cha Masigati kwa ajili ya kupanda mikorosho mipya baada ya wananchi kuhamasisha kupanda zao hilo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya korosho nchini ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini ambao yalifanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho.
Viongozi wa bodi hiyo ambao walifika kwenye shamba la mfano lililopo katika Kijiji cha Masigati kwenye Halmashauri ya Manyoni ambalo lilianza mwaka jana ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba na Afisa Uhusiano Bryson Mshana wakiwa kwenye uhamasishaji wa kilimo hicho kwenye maeneo mapya.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya hizo ekari zilizopandwa ni 1250 kwa msimu uliopita wa kilimo na msimu umekaribia mwezi Desemba mwaka huu wataanza tena kuendelea na upandaji wa mikorosho mipya.
“Pamoja na kwamba tumetenga ekari 5,000 kwa ajili ya kulima kilimo cha Korosho lakini mipango yetu ni kufikia ekari 10,000 alisema pamoja na hayo tutaendelea kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuweza kuchangamkia fursa ya zao hili na kupanda mikorosho kwa wingi, alisema.
Alisema wananchi wake wamehamasika baada ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa kupitia mikutano mbalimbali huku akiwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya kilimo hicho kutokana na kwamba maeneo yote yana uwezo kustawi zao hilo hivyo walipande kwani litawasaidia na kuwa mkombozi wa maisha yao.
“Lakini pia nisema kilimo hiki kimeweza kutoa fursa kwa watu kutoka mikoa mingine wameanza kulima korosho Manyoni hamasa bado inaendelea kwa halmshauri mbili za Manyoni na Itigi licha kwamba hawajafanya kilimo cha pamoja lakini watu wanalima Korosho,” alisema.
Alisema Halmashauri ya Manyoni wamekuwa na mpango wa kilimo cha pamoja kupitia ekari hizo elfu tano jambo ambalo limesaidia wananchi kupata ajira na hivyo kukuza uchumi wao kutokana na shughuli za upandaji zinazofanyika.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi aliishukuru bodi ya korosho kutokana na kwamba wao ndio wamekuwa chachu ya kuzalisha korosho kama zao la mkakati kwenye halamshauri yao limeanza na wao kama bodi walikuwa wa kwanza kuhamasisha wananchi.
Alisema kabla ya kuanza kilimo hicho Utaftiti ulifanyika na baada ya kugundua korosho inaweza kufanya vizuri hivyo bodi ya korosho waliomba ardhi na wazo lao kubwa lilikuwa la kwanza kupitia Halmshauri walifika Kijijini Masigati kuzungyumza na wananchi waliomba ardhi wakapewa eka 2000 wahamasisha vikundi vikaundwa wakaanza kugawa ardhi kwa vikundi.
Alisema kila kikundi kina ekari si chini ya 100 wameanza kusafisha mashamba wanalima korosho lakini wameamua mradi huo upanuliwe kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi huku akiwakaribisha watanzania wengine kuchangamkia fursa hiyo.

Comments