Featured Post

VIONGOZI WA DINI WAWE SEHEMU MUHIMU KATIKA MIKAKATI YA KUJIKINGA NA EBOLA



NA WAMJW-KIGOMA
VIONGOZI wa dini zote wametakiwa kushirikishwa kwenye maandalizi ya mapambano ya ugonjwa wa ebola ambao umetaatifiwa upo nchi jirani ya Jamhuri ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo endapo itatokea utaingia nchini Tanzania ili kuweza kuutokomeza kabisa.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati alipotembelea Mkoa wa Kigoma akiongozana na timu yake ya wataalam kwa ajili ya ukaguzi wa nyenzo na afua mbalimbali zilizowekwa ili kupambana na ugonjwa wa ebola leo Mkoani humo.
“Afua muhimu ya mkoa wowote katika kupambana na ugonjwa huu ni kuwashirikisha vizuri viongozi wa dini zetu pamoja na viongozi wa kimila na jamii kwani ndio wanaokutana na wanajamii kwa muda mwingi zaidi hivyo kuwashirikisha kwao elimu juu ya kujikinga na Ebola itakuwa kubwa zaidi na hatimae tutafanikiwa kujikinga na ugonjwa huu” alisema Prof. Bakari.
Aidha Prof. Bakari Kambi amesema kuwa Mkoa wa Kigoma upo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa Ebola kwa kuwa kuna mipaka mingi iliyo wazi ambayo inaingiza wageni kutoka Burundi na Congo ambapo ugonjwa huo umetaarifa upo maeneo ya nchi ya Congo.
Mbali na hayo Prof. Bakari Kambi ameuoingeza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa jitihada na mikakati waliyoiweka na kuifanyia kazi ili kuweza kudhibiti ugonjwa wa Ebola endapo utaingia Mkoani humo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote amesema kuwa Kigoma amesema kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika maeneo yote ya Mkoa huo.
“Utambuzi wa joto la Mwili kwa wageni kutoka nchi jirani ya Congo wanaoingia kupitia bandari ya Kigoma, Manyovu, Kibirizi, Mabamba , Uwanja wa Ndege , Kituo cha Gari Moshi bado unaendea kufanyika kwa uhakika kwa kutumia Thermo scanner ili kudhibiti ugonjwa huo” alisema Dkt. Chaote.
Aidha Dkt. Chaote amesema kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa jamii, watumishi wa Afya, madereva wa magari ya kubebea wagonjwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kujikinga na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.
“Tumetoa mafunzo kwa timu za kitaalam mbalimbali za Mkoa pamoja na kuhakikisha madawa, vifaa tiba na PPE vipo vya kutosha wakati wote katika vituo vyote vilivyoanishwa kupokea na kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola” alisema Dkt. Chaote.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Kambi ameambatana na jopo la wataalam ikiwemo idara ya uhakiki ubora wa huduma za afya , Kitengo cha Dharura na Maafa,Elimu ya Afya kwa Umma , Kitengo Cha mawasiliano Wizara ya Afya zote kutoka Wizara ya Afya pamoja na Wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kukagua na kujiridhisha mikakati ya kujikinga na Ebola endapo itaingia nchini.




Comments