- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NEW YORK, MAREKANI
RAIS wa Marekani Donald Trump amezionya kampuni za
mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na Facebook kwa kile alichokiita kuminya
taarifa zake na za mrengo wa kihafidhina.
Trump ameitaka mitandao hiyo kuwa makini baada ya awali
kuishutumu Google kwa kupindua matokeo ya taarifa pale mtumiaji wa mtandao huo
anapotafuta habari kumhusu Trump.
Hata hivyo, Google wamekanusha shutuma kuwa mtandao wao unaupendeleo
na kusema hawafungamani na itikadi yoyote ya kisiasa.
Akiongea na wanahabari katika ikulu ya White House, Trump
amesema, "Google wamekuwa wakihadaa watu wengi, ni jambo zito sana."
Akaziongeza pia kata lawama Twitter na Facebook,
"inawapasa wawe makini, hauwezi ukawafanyia watu mambo haya…tunapokea
maelfu ya malalamiko juu ya jambo hili."
Rais Trump hatahivyo hajabainisha ni hatua gani hasa ambazo
utawala wake unapanga kuzichukua.
Awali mshauri wa Trump wa masuala ya uchumi, Larry Kudlow
amesema utawala kwa sasa unaangalia ni namna gani wataliendea suala hilo kwa
kuangalia kanuni za udhibiti.
Hatua gani Trump atachukua dhidi ya mitandao?
Wachambuzi wa mambo wanasema ni vigumu kwa Trump
kuthibitisha madai yake na haieleweki hasa namna gani atalishughulikia suala
hilo.
Hoja iliyopo ni kuwa, hatua yoyote ya kuiubadilisha mtandao
wa Google itapelekea kuvunjwa kwa katiba ya Marekani hususan uhuru wa habari,
japo yawezekana hatua zikachukuliwa kibiashara zaidi.
Akitumia mtandao wake pendwa wa Twitter, Trump aliishutumu
Google kwa kuzipa kipaumbele habari hasi kutoka kwenye vyombo vya habari
alivyovitaja kama vya mrengo wa kushoto (waliberali).
Juma lililopita Trump pia aliishutumu mitandao ya kijamii
kuwa "inabagugua moja kwa moja sauti za Republican/kihafidhina," na
kuahidi kuwa "hatokubali kuacha hilo liendelee."
Facebook na Twitter bado hawajatoa mrejesho juu ya shutuma
hizo ila Google wamezipinga vikali.
"Kusaka taarifa kwenye mtandao wetu hakutumiki kuweka
agenda za kisiasa na hatufanyi upendeleo wowote kwa itikadi za kisiasa,"
imesema taarifa ya Google.
Mhadhiri mwandamizi wa teknologia za kidijiti kutoka chou
cha King's College London Mercedes Bunz, ameiambia BBC kuwa haiyumkiniki kuwa
Google wamekuwa wakipangilia taarifa katika mtandao wao kwa upendeleo wa
kisiasa.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, mpangilio wa mtaandao huo
huangalia zaidi uhalisia wa taarifa na ukaribu wa kijiografia wa watumiaji
wake.
Comments
Post a Comment