- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
THERESA MAY NA MTIHANI WA UINGEREZA KUBORESHA BIASHARA NA AFRIKA BAADA YA KUJITENGA NA UMOJA WA ULAYA
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NAIROBI, KENYA
Uingereza ina uhusiano wa kihistoria na mataifa mengi ya
Afrika. Uhusiano huo bado unaendelea kuwa na maana, lakini kitu kimoja ambacho
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekutana nacho katika ziara yake ya
Afrika ni kuwa nchi yake inagombea nafasi na mataifa mengine yanayowekeza kwa
kiwango kikubwa.
Hii leo Bi May ametua Kenya baada ya kuzuru Afrika Kusini na
Nigeria. Hii ni ziara ya mwanzo kwa Bi May barani Afrika akiwa mamlakani. Nchi
yake imenuwia kuimarisha mahusiano yake na mataifa ya Afrika kipindi hiki
ambacho wanakaribia kujitenga na Umoja wa Ulaya (EU).
Akiwa jijini Cape Town, Bi May ameahidi nchi yake kuwekeza
pauni bilioni 4 barani Afrika mara baada ya nchi yake kuondoka EU mwakani.
May pia amesema anatarajia kusain makubaliano na serikali ya
Kenya kurejesha mabilioni ya pesa yaliyotoroshewa Uingereza kinyume cha sheria.
"Azma ya Uingereza baada ya kujitoa EU mwezi Machi 2019
ni kuimarisha ushirikiano wake na dunia kwa ujumla…Wiki hii natarajia kuwa na
mjadala wa namna gani wa kufikia azma hiyo pamoja na bara la Afrika kwa
kusaidia katika uwekezaji wenye tija na kukuza ajira pamoja na kuimarisha
ulinzi na usalama," ilisema sehemu ya taarifa ya Bi May kabla ya ziara
yake.
Hatahivyo, hilo linaweza kuwa jambo gumu.
Kabla ya May kuwasili Kenya, rais wa taifa hilo Uhuru
Kenyatta alikuwa Marekani ambapo alifanya mazungumzo na rais Donald Trump na
wawili hao kusaini makubaliano kadha ya kibiashara yenye thamani ya $900
miloni.
Baada ya kukutana na Bi May, Bw Kenyatta ataelekea Uchina
kwenda kushiriki mkutano wa uhusiano baina ya Uchina na Afrika.
Uingereza kwa sasa inabadili sharia zake ili kuruhusu bidhaa
kutoka Afrika zinaingia nchini humo kwa namna sawa kama ilivyo sasa hata baada
ya kujitenga na EU.
Uingereza yajaribu kuivutia Afrika baada ya Brexit.
Nchi za Afrika, nyingi zikiwa makoloni ya zamani ya
Uingereza zitalazimika kujipanga upya katika uhusiano wao na nchi hiyo hususan
baada ya kujitenga na EU. Endapo Uingereza itashindwa kuafikiana vizuri na EU kabla
ya pande hizo mbili kutengana basi ni Dhahiri uhusiano wa kibiashara baina ya
Uingereza na Afrika pia utayumba.
"Kenya mathalan mzunguko wake wa biashara baina ya EU
na Uingereza ni asilimia 50 kwa 50, hivyo basi inawabidi waingie makubaliano
mazuri na pande zote mbili sababu inahitaji masoko yote hayo kuuza chai, bidhaa
ghafi na mazao mengine," mchumi Tony Waitima ameiambia BBC.
Kenya ndio nchi kinara kwa kuuza maua waridi (roses) katika
Umoja wa Ulaya, na ni nchi ya tatu kwa kuuza maua kwa ujumla duniani. Kilimo
cha maua kinategemewa moja kwa moja na watu 500,000 kwamujibu WA Baraza la Maua
la Kenya hivyo kupata makubaliano mazuri kutoka pande zote mbili ni jambo
muhimu zaidi.
Pamoja na juhudi za Uingereza kuishika Afrika kibiashara
lakini ni wazi kuwa bara hilo kwa sasa linabembelezwa kutoka kila kona.
Comments
Post a Comment