- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA ALOYCE
NDELEIO
Sayansi
ya teknolojia-nano ni tegemeo kubwa katika sekta nyingi zikiwemo za
uzalishaji wa vyakula, nishati na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA). Lakini hoja ni nchi masikini zitamudu kudai sehemu ya faida? Je
teknolojia hiyo ni salama?
Chukua
unywele mmoja kutoka kichwani, fikiria kipenyo chake ambacho ni sehemu ya
maelfu kadhaa ya sentimeta na japo mara nyingi huonekana haiwezekani basi
fikra za aina hiyo ujue zinakupeleka kwenye vipimo halisi vya skeli za
nano-meta, zinazotoa msingi wa teknolojia mpya ya teknolojia-nano.
Waliobahatika
kusoma Fizikia wanao upeo wa vipimo vya aina hiyo kwa kutumia kifaa cha
“Micrometer Screw Gauge” kinachopima vipenyo vya vitu kama nyuzi au unywele.
Wengine
wanatumia teknolojia-nano bila kujua na mfano hai ni dawa ya kusafisha maji ya
Water Guard ambapo vifuniko viwili au vidonge viwili vyenye ujazo ulio
chini ya mililita kumi husafisha maji yenye ujazo wa lita zaidi ya 18.
Teknolojia-nano
kwa tafsiri rahisi ni sayansi ya vitu vidogo mno, lakini mtazamo wake ni mpana.
Inaonekana kama mapinduzi ya kiteknolojia kama ilivyo kwa intaneti, na wigo
wake hupanuka zaidi.
Wanaoiunga
mkono wanaona mkondo huu mpya wa sayansi unasaidia kukabiliana na baadhi
ya matatizo makubwa na nyeti katika maendeleo.
Faida
zake muhimu ni pamoja na kusafisha maji, mfumo wa nishati, tiba,
uzalishaji wa vyakula na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Teknolojia-nano
inafanya kazi kwa kudhibiti atomi moja kwa moja na molekuli kuzalisha
vitu au vifaa, ni mfumo ambao ni mdogo, mwepesi, wa haraka na ulio na ufanisi
mzuri.
Yamekuwepo
mazungumzo kuhusu umuhimu wa teknolojia-nano katika uzalishaji kwa gharama
zilizo nafuu katika machimbo ya madini na kuzalisha teknolojia
nyingine zinazoiunga mkono.
Uhifadhi
na ukusanyaji wa nishati ya jua umeanza kupitia teknolojia- nano na
utapunguza kiwango cha kaboni inayotoka viwandani.
Msingi au
tabia kuu ya teknolojia-nano ni jinsi malighafi hubadilika zinapofanya kazi
ndani ya wingi na mtazamo wa kidarubini ambapo vifaa vinavyotumiwa huweza
kuzalisha joto au mwanga.
Hali hii
inawezesha kuibuka kwa njia zote za matumizi na kuibua baadhi ya maswali muhimu
licha ya wasiwasi kuhusu madhara ambayo teknolojia-nano inaweza
kuambatana nayo.
Baadhi ya
hoja zinasema ni mapema mno kuchukua mkondo huo kwani bado haujazoeleka.
Wengine wanaangalia pengo kati ya nchi tajiri na maskini na kama nchi maskini
zitaingia kwenye mapinduzi ya teknolojia-nano.
NDOGO
LAKINI NZURI
Nchi zilizoendelea
duniani kama Australia, Ulaya, Japan na Marekani zinawekeza katika teknolojia
hii mpya, lakini kwa mtazamo mwingine teknolojia-nano ni tegemeo maridhawa kwa
nchi maskini.
Ripoti ya
Mradi wa Milenia wa Umoja wa Mataifa wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu;
Ubunifu: Matumizi katika Maendeleo; inahitimisha, “Teknolojia-nano
inaweza kuwa mahsusi na muhimu kwa nchi zinazoendelea kwani
inahusisha nguvu kazi kidogo, ardhi na hata ukarabati mdogo; ina uzalishaji
mkubwa gharama kidogo na inahitaji wastani mdogo wa malighafi na nishati.”
Brazil,
China, Korea Kusini, India na Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zinazoendelea
au zilizo kwenye uchumi mpito ambazo zimeshajiwekea programu za kitaifa za
utafiti wa teknolojia-nano na Shirika la Utafiti la Kilimo la Brazil
lilizindua Mpango wa Taifa wa Kimaabara wa teknolojia-nano kwa ajili ya Kilimo
cha Biashara.
Miradi ya
utafiti inajumuisha uzalishaji wa nyuzi-nano kutoka kwenye nazi na katani
zitakazotumika kuimarisha nyuzi za kawaida sanjari na teknolojia-nano
kuanzisha miundombinu itakayowezesha kuzalisha viuatilifu.
Miongoni mwa nchi zinazoendelea Afrika Kusini inaongoza katika sekta hii ikiwa na dazeni moja ya Vyuo Vikuu, Mabaraza manne ya Sayansi na Kampuni kadhaa zilizo hai katika tafiti na maendeleo.
Miongoni mwa nchi zinazoendelea Afrika Kusini inaongoza katika sekta hii ikiwa na dazeni moja ya Vyuo Vikuu, Mabaraza manne ya Sayansi na Kampuni kadhaa zilizo hai katika tafiti na maendeleo.
Aprili
2006, Afrika Kusini ilizindua Mkakati wa Taifa wa Teknolojia-nano ukiwa ni
uwekezaji wa Rand (fedha za Afrika Kusini) milioni 170 sawa na Euro milioni
18.6 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Bidhaa za
kwanza kuzalishwa zinatarajiwa kutokana na miradi ya kusafisha maji, uwekezaji
wa vifaa vinavyotumia nishati ya jua, mikakati ya kuongeza rutuba kwenye udongo
na malighafi nyingine zinazotokana na viumbe hai kwa ajili ya kuzalisha
dawa za tiba.
Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Zululand
tayari imeonesha matokeo yenye matumaini kwenye uchunguzi wa
matumizi ya malighafi-nano katika kusafisha maji na uhifadhi wa nishati.
Aidha
kiwanda cha kutengeneza karatasi cha Sappi kinafanya majaribio ya
vingamuzi-nano kwenye miti ili kubaini wadudu waharibifu na fangasi. Kadhalika
wanafizikia kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town wanaendesha mradi wa matumizi ya
chembechembe-nano za silikoni katika uchapaji wa eletroniki.
Lengo la
mradi huo ni kuanzisha seli za nishati ya jua ambazo zinaweza kuchapishwa
kwenye karatasi, nyepesi za gharama nafuu ambazo ni mbadala wa paneli
zinazotumiwa sasa.
VIFAA
SAFI KWA UZALISHAJI CHAKULA
Wanasayansi
tayari wameanzisha matumizi mengi ya gharama nafuu kwa kutumia mbinu-nano
kuongeza rutuba ya udongo na uzalishaji wa mazao zikiwemo vingamuzi-nano vya
kufuatilia afya ya mimea na wanyama na chembechembe zenye sumaku kwa ajili ya
kuondoa vitu vinavyoweza kuchafua udongo.
Mirija-nano
itapunguza gharama za ujenzi wa majumba ya kuotesha mimea kama mboga (green
house), kupunguza shinikizo kwenye ardhi na vyanzo vya maji.
Katika
nyanja ya uzalishaji wa chakula, zimeanzishwa mbinu za kuboresha
ufuatiliaji wa bidhaa za kilimo, hitaji linalokua kwenye soko la kuuza nje.
Nchini
Marekani watafiti wa Chuo Kikuu cha Berkeley wanashughulikia njia za kutambua
bakteria au virusi kwa kutumia mfumo wa kielektoniki wa
teknolojia-nano.
Njia hiyo
itabaini dalili za awali za magonjwa ya mazao kufuatana na mabadiliko ya kukua
na kupumua.
Wataalamu
wa teknolojia-nano katika Chuo Kikuu cha Michigan wameshaanza tathmini ya
viumbe kwa kutumia vingamuzi-nano ambavyo hupandikizwa kwenye mifugo ili
kubaini chembechembe za kirusi mapema kabla dalili za ugonjwa kuthibitika.
Katika
nyanja hiyo ya uzalishaji wa chakula mbinu zimeanzishwa kuboresha namna
ya kutambua vyanzo vya mazao ya kilimo kulingana na mahitaji ya soko la nje la
bidhaa za kilimo.
Nchini
Marekani wanasayansi wamekuwa wanafanyia kazi -Kutambua Uhifadhi kwa
Skeli-nano, mbinu ambazo zinalenga kupata muendelezo wa kufuatilia
uzalishaji kupitia mfumo wa uzalishaji, kutambua dalili za virusi vya magonjwa,
wadudu na hata kuwepo kwa mazao ambayo viini tete vimeboreshwa.
Kutokana
na masharti au mahitaji ya kiafya ambayo yamekuwa ni mzigo kwa
wazalishaji wa nchi zinazoendelea, kuingia kwa teknolojia-nano kutakuwa ni
baraka kubwa.
Moja ya
matumizi ya teknolojia-nano ni kusafisha maji. Mifumo kadhaa ya kuchuja maji
imeanzishwa ili kuondoa chumvichumvi ndani ya maji au kuondoa taka au uchafu
kwenye maji ya umwagiliaji na yanayotumiwa majumbani.
Michujio
kadhaa yenye matundu ya kipimio cha mita-nano inaondoa kwa asilimia 100
bakteria au virusi na hata chembechembe zinazosababisha maambukizi kadhaa ya
magonjwa.
UZAO
MPYA ZANA ZA TEHAMA
Teknolojia-nano
inatarajiwa kuleta manufaa, kwenye TEHAMA kwa kuongeza kasi na ubora wa
kuunganisha na kuzifanya kompyuta kuonesha vifaa na kuunganishwa ambako maskini
watamudu.
Wataalamu
wanatabiri kuwa teknolojia-nano itafungua njia kwa wimbi jingine la maendeleo
ya TEHAMA yanayojumuisha mfumo wa kompyuta ambao umewekwa katika mazingira
yatakayokuwa ya kudumu, unaoingiliana na unaounganika.
Vifaa
vinavyoendana na vifaa vya kompyuta vitakuwa na matumizi mengi katika
mawasiliano, vikitumika kama simu, viunganisho vya intaneti, vifaa vya burudani
na video na vingamuzi vya mtandao na takwimu.
Vifaa hivyo vitahitaji vyanzo vya nguvu na utafiti upo njiani kuanzisha seli ambazo zinatumia mionzi ya jua itakayotumika kwenye vifaa vya mawasiliano kama simu selula na kwa ajili ya kuongeza nishati kwenye betri kwa kutumia mwanga wa jua au mwanga wa vyanzo vingine.
Vifaa hivyo vitahitaji vyanzo vya nguvu na utafiti upo njiani kuanzisha seli ambazo zinatumia mionzi ya jua itakayotumika kwenye vifaa vya mawasiliano kama simu selula na kwa ajili ya kuongeza nishati kwenye betri kwa kutumia mwanga wa jua au mwanga wa vyanzo vingine.
Katika
nyanja ya huduma ya afya teknolojia-nano inatoa vipande vya plastiki vyenye
ukubwa wa sarafu ambavyo vinaweza kutumika kubaini aina mbalimbali za magonjwa
kwenye tone la damu mahususi kwa ajili ya kliniki ndogo au zahanati.
Teknolojia-nano
inaonekana kupenyeza kwenye mfumo wa utoaji wa dawa ambao ni mzuri na unafaa
kwa mazingira ya nchi zinazoendelea ukizikwamua kutoka kwenye mfumo wa taratibu
wa utoaji wa dawa.
Inakuwa
ni suluhisho kwa maeneo ambayo wahudumu wa afya ni wachache na hata vifaa vya
kuhifadhi dawa ni duni au havipo. Kwa hali hiyo changamoto iliyopo ni kuifanya
teknolojia-nano ipatikane.
Malighafi
zenye muundo-nano tayari zinatumika kuunda uzao mpya wa seli za nguvu ya jua,
seli za mafuta ya haidrogeni na mfumo mpya wa kuhifadhi haidrogeni ikiwa ni
tumaini jipya kwa nishati safi.
Aidha vifaa vya nishati ya jua bado ni gharama kubwa kwa watumiaji wa nchi zinazoendelea. Hata hivyo teknolojia-nano inawezesha uzalishaji malighafi zisizo na gharama kwa ajili ya vifaa vya nishati ya jua ambavyo vinaweza kuwekwa kwenye paa la nyumba.
Aidha vifaa vya nishati ya jua bado ni gharama kubwa kwa watumiaji wa nchi zinazoendelea. Hata hivyo teknolojia-nano inawezesha uzalishaji malighafi zisizo na gharama kwa ajili ya vifaa vya nishati ya jua ambavyo vinaweza kuwekwa kwenye paa la nyumba.
MATUMIZI
KUMI KWA NCHI ZA KUSINI
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Maadili ya viumbe cha Chuo Kikuu cha
Toronto, Canada umebaini matumizi kumi ya teknolojia-nano ambayo yanaweza kuwa
ya manufaa kwa nchi zinazoendelea.
Matumizi
hayo ni pamoja na uhifadhi wa nishati, uzalishaji na kuibadilisha nishati
hiyo, uwezeshwaji na ufanisi, uzalishaji wa kilimo, kusafisha maji, ungamuzi na
kubaini magonjwa.
Mengine
ni mfumo wa kutoa dawa, usindikaji na uhifadhi wa vyakula, kubaini uchafuzi wa
hewa na marekebisho yake, ujenzi, ufuatiliaji wa afya, kudhibiti na kutambua
magonjwa na vyanzo vyake.
TUMAINI
NA HATARI
Si kila
mmoja anakubaliana na nadharia ya teknolojia-nano kuwa ni enzi mpya ya kipekee.
Miongoni mwa wapinzani ni asasi zisizo za Serikali (Azise) ya Kundi la
Mmomonyoko, Teknolojia na Uimarishaji (ETC), ambalo linaonya juu ya hatari ya
kiafya na mazingira, pia athari kwa wakulima wadogo maskini wa nchi za Kusini.
Azise
hiyo inasema kuwa wakulima wadogo wanaweza kujikuta hawaambulii kitu kwenye
mazao ya biashara kama mpira na pamba kwa kuwepo malighafi mbadala yanayotokana
na teknolojia-nano.
Inasema
kuwa nchi za Kusini zina nguvu kazi kubwa, hivyo kuingiza teknolojia-nano
ambazo zinapunguza fursa za ajira, kunamaanisha kupungua kwa ajira na kuanza
kutoa mafunzo upya.
Makundi
kama hayo yanashinikiza ifanyike tathmini juu ya athari za afya na mazingira
kabla matumizi ya teknolojia-nano hayajaenea.
Ipo hofu
pia kwamba chembechembe-nano zinaweza kujikusanya katika mfumo wa mzunguko wa
chakula. Ukinzani mwingine unadai kwamba teknolojia mpya inachupa haraka mno
hivyo kwamba miundo ya usimamizi inashindwa kutafuta nafasi yake.
Hofu hiyo
inatokana na sababu kuwa mwanya wa maendeleo hauwianishwi na majukumu ya
uchunguzi, ikiwemo hatari kuwa hili litasababisha jamii kurudishwa nyuma kama
ilivyotokea kwenye suala la bioteknolojia.
Hata
hivyo ripoti ya Kamisheni ya Ulaya inatahadharisha kuwa jamii na
wawekezaji kujiaminisha kwenye teknolojia-nano ni muhimu kwa maendeleo ya
muda mrefu na matumizi yenye manufaa.
MISAMIATI-NANO
Katika
mlolongo mzima wa teknolojia nano ipo misamiati kadhaa ambayo ni pamoja ni
“Nano-meta” sehemu moja bilioni moja ya mita. “Miundo-nano” ni muundo
mdogo kuliko nanometa 1,000 kipimo ambacho ni wastani wa kipenyo cha seli
moja ya viumbe hai.
Mengine “Teknolojia-nano” ni nyanja ya utafiti na maendeleo yanayohusisha ujenzi wa miundo kwa skeli za chembechembe.
Mengine “Teknolojia-nano” ni nyanja ya utafiti na maendeleo yanayohusisha ujenzi wa miundo kwa skeli za chembechembe.
“Mirija-nano”
ni mirija ambayo muundo wake wa jumla wa molekuli umeundwa na atomi za kaboni.
Mirija
hii ni imara kuliko chuma kwa kiwango cha mara 100 na inaweza kustahimili joto
hadi nyuzi joto za sentigredi 3,600 na zina upana wa nano-mita kadhaa.
Comments
Post a Comment