Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi
Lugola (wapili kulia) na Kamishna Jerenali wa Zimamoto, Thobias Andengenye wakisikiliza
maelezo kutoka kwa ofisa Mwamdamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Mabel Masasi juu ya huduma za anuani za makazi zinavyoweza
kusaidia utoaji haraka wa huduma za zima moto na uokoaji nchuni. Waziri Lugola
alikuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya Zimamoto Nchini,
iliyozinduliwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni miongoni mwa
taasisi za serikali zilizoshiriki katika maonesho ya Wiki ya Zimamoto na
Uokoaji kitaifa ambayo inafanyika jijini Dodoma kwa mara ya kwanza nchini.
Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutoa elimu juu ya namna
bora ya kuepuka majanga ya moto na kuwawezesha wananchi kuzifahamu vyema
shughuli nyiongi zinazofanywa na jeshi hilo ambazo si tu kuzima moto kama
inavyofahamika na wananchi wengi lakini ni pamoja na kusaidia katika majanga
mbalimbali na ajali.
TCRA kama mdau mkubwa
wa zimamoto mbali na kusaidia katika mawasiliano baina ya wananchi na Jeshi la
Zimamoto kuwa rahisi na ya bure kwa mujibu wa sheria lakini pia kupitia mradi
wao wa anuani za makazi unasaidia Jeshi hilo na wananchi kuweza kufikiwa kirahisi.
Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Mawasiliano, Mabel Masasi
alimwambia Waziri Kangi lugola kuwa kupitia anuania za makazi zimeweza
kurahisisha jeshi hilo kufika katika maeneo mengi kirahisi kwa kutaja jina la
mtaa na namba ya nyumba la eneo husika.
Waziri wa Mambi ya Ndani, Kangi Lugola
akiuliza jambo katika banda hilo la TCRA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi
Lugola (wapili kulia) na Kamishna Jerenali wa Zimamoto, Thobias Ndengenye
wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) juu ya huduma za anuani za makazi zinavyoweza kusaidia utoaji haraka wa
huduma za zima moto na uokoaji nchuni. Waziri Lugola alikuwa akitembelea
mabanda ya maonesho ya Siku ya Zimamoto Nchini, Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
jana.
Wananchi na maofisa mbalimbali wa Jeshi
la Zimamoto wakiwa katika Banda la TCRA kupata vipeperushi na maelezo
mbalimbali ya kazi za taasisi hiyo.
Comments
Post a Comment