Featured Post

TANZANIA NA CHINA ZATIA SAINI MAKUBALIANO YA KUENDELEZA URITHI WA UTAMADUNI Inbox x


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga  kulia) akimkabidhi  Naibu Waziri wa  Mambo Kale wa China, Li You (kushoto)  zawadi ya kinyago maarufu kwa jina la kinyago cha ujamaa  mara baada ya kusainiana mkataba wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na China katika Nyanja za urithi wa Utamaduni uliolenga kubadilisha na kushirikiana utaalamu katika masuala ya malikale pamoja  na kubadilishana taarifa.   Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ( Picha na Lusungu Helela-MNRT).


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Waziri wa  Mambo Kale wa China, Li You (kushoto) mara baada ya kusainiana mkataba wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na China katika Nyanja za urithi wa Utamadani uliolenga kubadilisha na kushirikiana utaalamu katika masuala ya malikale  pamoja na kubadilishana taarifa. Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam( Picha na Lusungu Helela-MNRT)

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akisaini hati ya makubaliano na Naibu Waziri wa Mambo Kale wa China, Li You (kushoto) kati ya Serikali ya Tanzania na China katika Nyanja za urithi wa Utamadani uliolenga kubadilisha na kushirikiana utaalamu katika masuala ya malikale pamoja  na kubadilishana taarifa. Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam( Picha na Lusungu Helela-MNRT)

Serikali ya Tanzania  na Jamhuri ya Watu wa China, zimetiliana saini ya hati ya Makubaliano ya  (Memorandum of Undestanding) kubadilishana na kushirikiana katika nyanja ya urithi wa utamaduni (Malikale).
Utiaji saini huo umefanyika leo jijini Dare Salaam  kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu Waziri wa Malikale wa Jamhuri ya Watu wa China, Li You.
Utiaji saini huo umeshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen Gaudence Milanzi pamoja na wajumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China.
Makubaliano hayo baina ya nchi mbili yamelenga katika   kukuza ushirikiano katika masuala ya Malikale,  kubadilisha utaalamu pamoja na  wasimamizi katika nyanja ya urithi wa utamaduni.
Aidha, utiaji saini huo utatoa fursa kwa wataalamu hao kuweza  kutembeleana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu  baina ya nchi hizombili  ikiwa ni pamoja  na kutoa mafunzo ya kitaaluma kwa wasimamizi wa masuala ya Malikale.
Vilevile, utiaji saini huo utasaidia katika kulinda na kuhifadhi maeneo ya urithi wa dunia pamoja na kupambana na usafirishaji haramu wa rasilimali za kiutamaduni.
Pia utiaji saini huo, utawezesha  katika mabadilishano katika kuweka kumbuku, ubainishaji na  utunzaji  wa makusanyo ya makubusho na masuala ya uhamasishaji jamii pamoja utoaji wa huduma kwa jamii.
Shughuli hiyo ya utiaji saini imekuwa sehemu ya kukuza pamoja na kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya Nchi ya China na Tanzania.




Comments