Featured Post

RAIS WA FIFA AKUTANA NA TRUMP KWA AJILI YA MAZUNGUMZO YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2026

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA), Gianni Infantino, leo amekutana na Rais wa Marekeni Donald Trump na kupata wasaa wa kuzungumza machache kuhusiana na fainali za Kombe la Dunia.


Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa mwaka 2026 ambapo taifa la Marekani litakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na nchi za Canada pamoja na Mexico.
Infantino amekutana na Trump na kuzungumzia mambo mbalimbali haswa kuhusiana na maandalizi ya kuelekea fainali hizo ambazo zitahusisha nchi tatu.
Mbali na mazungumzo hayo, Infantino alimkabidhi Trump jezi namba 26 kama sehemu ya kutambua mchango wake wa kupokea kwa mikono miwili fainali hizo kufanyika nchini humo kwa mwaka 2026
Imekuwa mara ya kwanza kwa Trump kukutana na Rais wa FIFA tangu atangazwe kuwa kiongozi mkuu wa Marekani akichukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Barack Obama baada ya kumaliza muda wake.

Comments