- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
TEXAS, MAREKANI
Ofisa wa Polisi amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa
kumpiga risasi na kumuua kijana mweusi huko Texas, Marekani.
Roy Oliver, ambaye ni mzungu alifyatua risasi kwenye gari ambalo
lilikuwa litoka katika karamu moja huko Dallas mwezi Aprili 2017 na kumuua Jordan
Edwards aliyekuwa na umiri wa maiaka 15.
Ni nadra sana polisi kuhukumiwa kifungo kwa kuua. Mawakili
wa Oliver wanasema watakata rufaa.
Familia ya Jordan inasema kifungo hicho ni kifupi sana.
"Atakuwa huru baada ya miaka 15 na hicho si cha kutosha
wa sababu Jordan hatapata maisha tena," mama wa kambo wa Charmaine
Edwards, alisema.
Kipi kilitokea siku ya
mauaji?
Usiku wa tarehe 29 Aprili 2017 polisi waliitikia ripoti za
watoto waliokuwa wakinywa pombe kwenye karamu moja huko Balch Springs.
Polisi walikuwa ndani ya nyumba walipojaribu kumpata mwenye
nyumba wakati waliposikia kile walichoamini kuwa ni sauti za risasi, hali
iliyozua hofu nyumbani na kusababisha watu kukimbia.
Kulingana na nyaraka za polisi, polisi mwingine Tyler Gross
alijaribu kusimamisha gari lililokuwa limejaa ambao walikuwa wakiondoka kwenye
karamu.
Alitembea kwenda kwenye mlango wa abiria wa gari na kugonga
kioo, ambacho kilivunjika.
Kisha Oliver akafyatua risasi mara kadhaa kwenda kwenye gari
hilo, akampiga Jordan ambaye alikuwa amekaa mbele ya kiti cha abiria, nyuma ya
kichwa.
Oliver alisema aliamini kuwa gari hilo lilikuwa linarudi
nyuma kwenda kwa polisi mwenzake.
Hata hivyo, kamera ya polisi huyo ilionyesha kuwa gari hilo
lilikuwa likiondoka kwa polisi wakati risasi hizo zilipofyatuliwa.
Oliver alifukuzwa kazi muda mfupi tu baada ya mauaji hayo.
Watu wanahisi vipi
kuhusu hukumu hiyo?
Jaji huko Texas alimpata Oliver na hatia siku ya Jumanne na
Jumatano akahukumiwa miaka 15 jela.
Hii inamaanisha kuwa anaweza kupewa msamaha baada ya miaka
saba unusu.
Waendesha mashtaka walikuwa wanataka ahukumiwe kifungo cha
miaka 60.
Familia ya Jordan iliangua kilio na kuwakumbatia waendesha
mashtaka baada ya kusomwa hukumu.
Baba yake, Odell Edwaerds alisema alikuwa mwenye furaha
sana.
Hata hivyo, mama wake wa kambo alisema alitakiwa kifungo
kirefu cha miaka 25 hadi 30.
Wakili wa familia ya Edwards Daryl Washington, alisema
hukumu hiyo ni ishara kuwa kila Mwamerika mweusi aliyeuawa na polisi hakupata
haki.
Comments
Post a Comment