Featured Post

MKURUGENZI TUNDURU AONYA WATAKAOKWAMISHA MIRADI YA MAENDELEO


Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Gasper Balyomi, amewaonya watumishi wanaosimamia miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo kuacha mara moja tabia ya kupiga dili fedha za miradi ya wananchi na kwamba wote watakaobainika atawachukulia hatua.

Mkurugenzi huyo mpya wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Bw. Gasper Balyomi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa halmashauri hiyo na kudai kumekuwa na baadhi ya watumishi
wanaosimamia miradi ya maendeleo ya wananchi kupiga dili na kujilimbikizia fedha hali ambayo inarudhisha nyuma ustawi wa jamii.
Naye katibu tawala wa wilaya ya Tunduru, Gharibu Lingo amemuomba mkurugenzi huyo kuwa makini pia na watumishi wanaoendekeza ugomvi na vurugu kwa lengo la kukwamisha shughuli za maendeleo.

Comments