- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
RICHARD MWANGULUBE/BUKOBA
Mkoa wa Kagera umefanikiwa kujenga viwanda 91 katka kipindi cha mwezi Disemba 2017 na Juni mwaka 2018 ambapo kati ya hivyo 38 ni Viwanda vidogo ambapo ka ujumla wake vimefanikiwa kutengeneza ajira kwa watu 672.
Ujenzi huo wa viwanda unatokana na mkakati wa ‘Mkoa huo wa kujenga viwanda vipatavyo 100’ kwa mwaka mkakati ambao kitaifa uliozinduliwa mjini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo Oktoba mwaka jana 2018.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera(RAS) Diwani Athumani aliieleza alipozungumza na Gazeti la Tanzanite One Ofisini kwake mjini Bukoba katika mahojiano maalumu kwamba Viwanda hivyo ni vya kuchakata nafaka na mafuta ya alizeti, viwanda vya matofali,useremala,ushonaji nguo, kukoboa kahawa pamoja na viwanda vya sabuni.
Diwani Athumani Alisema pamoja na viwanda vidogo vinavyoendelea kujengwa lakini tayari kuna Viwanda vikubwa vitano alivyovitaja kuwa ni Kiwanda cha KADERES Plc kilichopo wilaya ya Karagwe kilichoanza uzalishaji mwezi juni mwaka huu 2018 kinachohusika na uchakataji wa maharage kwa kuyachambua kuondoa mawe, kusafisha, kuyapanga katika madaraja na kuyafungasha tayari kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
Athumani alitaja viwanda kingine kuwa cha usindikaji kahawa cha Amir Hamza (T) Ltd ambacho kimejengwa katika wilaya ya Bukoba eneo la Kibuye na Kiwanda cha maji ya kunywa cha Bunena Dev Co Ltd kilichopo katika Manispaa ya Bukoba.
Viwanda vingine vilivyoko katika hatua ya mwisho ya ujenzi ni Mayawa kilichoko katika Manispaa ya Bukoba ambacho kitazalisha maji ya matunda,mvinyo na maji ya kunywa,Kiwanda cha usindikaji wa nyanya na pilipili cha Victoria Edibles Limited kinacojengwa Bukoba Vijijini na Kiwanda cha Vinywaji Vikali cha Ambiance (T) Distilleries Limited kinachojengwa katika Manispaa ya Bukoba eneo la Miembeni.
Aidha Athumani alisema Wawekezaji watano wameonyesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vikubwa ambao ni Kampuni ya Gesap Agro Farming Co Ltd ya Morogoro kwa kujenga kiwanda cha maziwa katika wilayani Missenyi na Kampuni ya BenBuild Investment Limited iliyoanza ujenzi wa Kiwanda cha Vigae eneo la Kihanga wilayani Karagwe.
Wawekezaji wengine ni KADERES PLC anayetarajia kujenga kiwanda cha kahawa wilayani Muleba,Sying Investment Company Limited ya nchini China inayotarajia kujenga kiwanda cha nyama katika wilaya ya Missenyi na Kampuni ya Ndyanga Co Limited ya Muleba kujenga kiwanda cha maji wilayani Muleba.
Viwanda vikubwa vya muda mrefu vilivyoko mkoani humo ni pamoja na cha sukari cha Kagera Sugar kilichobinafishwa mwaka 2001.
Viwanda vya uchakataji samaki vya Kagera Fish Co Ltd kilichopo eneo la Kemondo wilaya ya Bukoba na Supreme Perch Ltd kilichopo Nyamukazi wilaya ya Bukoba.
Kiwanda cha Chai Kagera kilichopo Maruku wilaya ya Bukoba kilichobinafishwa na Serikali mwaka 2000 kutoka iliyokuwa Mamlaka ya Chai Kagera.
Vingine ni viwanda vya kahawa vya TANICA kilichopo Manispaa ya Bukoba ,BUCOP kilichopo katika wilaya ya Bukoba eneo la Custom kilichoanzishwa mwaka 1935 na Kiwanda cha Olam (T) Ltd kilichopo katika wilaya ya Missenyi eneo la Bunazi.
"Mkoa wa Kagera wenye Halmashauri nane ambazo ni Biharamulo,Bukoba Vijijini,Manispaa ya Bukoba,Kyerwa,Karagwe,Missenyi
Pia amevitaja Viwanda vingine kuwa ni Kiwanda cha chai Kagera (Kagera Tea Co.Ltd ambacho kipo eneo la Maruku Wilaya ya Bukoba ambacho kilibinafisishwa na Serikali mwaka 2000 na kukabidhiwa kwa mwekezaji ambaye ni mzawa.
Pia kuna Kiwanda cha TANICA ambacho kipo katika Manispaa ya Bukoba na ambacho kilibinafisishwa na Serikali na kukabidhiwa Chama cha Ushirika cha Mkoa (KCU 1990). Ameeleza Diwani Athumani.
Alifafanua kwamba Mkoa wa Kagera bado unazo fursa nyingi na muhimu kwa ajili ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao unaweza kufanywa katika sekta za Kilimo,Viwanda, Utalii, Uvuvi, Ufugaji ambapo Mkoa tayari umetenga zaidi ya hekta 58,000.
Hata hivyo alitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika fursa za uwekezaji kuwa maeneo mengi ya uwekezaji na ujenzi wa Viwanda hayajapimwa, urasimu na mlolongo mrefu na ukiritimba katika upimaji wa ardhi na kukosekana kwa mfumo mzuri na wa haraka katika upimaji wa ardhi ilikuvutia zaidi wawekezaji
Pia Changamoto nyingine ni upungufu wa watumishi katika halmashauri za Wilaya za Mkoa huo alieleza Diwani Athumani Katibu Tawalawa Mkoa huo wa Kagera.
Comments
Post a Comment