Featured Post

HAWA GHASIA AJIUZULU UENYEKITI KAMATI YA BUNGE YA BAJETI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia

DODOMA
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni wamejiuzulu nafasi hizo, leo Jumanne Agosti 28, 2018.
Ghasia, ambaye ni Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) na Soni (Babati Vijijini - CCM) wametangaza uamuzi huo leo asubuhi mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai, amethibitisha kujiuzulu kwa viongozi hao wa kamati.
"Ni kweli wamejiuzulu nafasi zao na mimi sijajua kwa nini wamejiuzulu," amesema.

Comments