- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA ALOYCE
NDELEIO
Elimu
imekuwa ni moja ya nguzo zinazoleta ufanisi kwenye utendaji wa serikali
ikizingatiwa kuwa ndiyo inayosimamia sehemu kubwa ya sekta za umma.
Lakini
kuporomoka kwa kiwango cha elimu kunakuwa tishio kwamba elimu itakuwa duni na
sekta za umma zitakuwa na watendaji dhaifu ambayo watashindwa kupambana na
vikwazo katika uzalishaji na ukuzaji wa uchumi.
Katika
mazingira hayo ni kwamba kundi la watendaji wa serikali watakaokuwepo kwenye
uongozi wataendesha mambo kisanii na hivyo kuathiri dhana nzima ya utawala
bora.
Ufanisi wa
serikali ni muhimu kwenye maendeleo kiuchumi. Kwa ujumla ustawi wa maendeleo ya kiuchumi kwenye nchi
zilizoko pembezoni ambako serikali zinashindwa kupunguza kiwango cha rushwa,
utekelezaji wa sheria na kuboresha mazingira kwa maendeleo ya sekta binafsi
kumekuwa kunachangiwa na ukosefu wa elimu bora.
Takwimu
zinaonesha kwamba upo uhusiano chanya kati ya elimu bora miongoni mwa
wafanyakazi wa serikali na wigo tofauti wa ufanisi wa serikali kwa maana
kwamba watumishi wa serikali wanapokuwa
na elimu nzuri, kiwango cha rushwa kinakuwa kidogo wakati kiwango cha
ukusanyaji kodi kikiwa kikubwa.
Kwa upande
mwingine usimamizi wa fedha za umma unakuwa mzuri na huungwa mkono zaidi na
soko binafsi au sekta buinafsi.
Kiwango
kikubwa cha elimu kwenye usimamizi na utawala huwa kinahusiana na kuwepo kwa
kiwango kidogo cha rushwa ndani ya utawala husika.
Kwa mujibu
wa mwongozo wa kimataifa wa mwaka 2012 unaohusu kuondokana na athari
zinazozikabili nchi ambao unajulikana kwa kiingereza kama International Country
Risk Guide2012 ni kwamba upo uhusiano
kati ya kiwango cha elimu anachokuwa amekipata mtumishi na vidokezo vya rushwa.
Kutokana
na hali hiyo kiwango cha elimu kwenye
uongozi wa umma kinaendelea kufungamana
na kiwango kidogo cha rushwa.
Vidokezo
hivyo vinabainisha kuwa sehemu kubwa ya nguvu kazi iliyopata elimu inaweza
kuchangia kwenye kiwango kikubwa cha maendeleo kwa kusaidia kupunguza matumizi mabaya ya ferdha za umma na hivyo
kuwezesha sekta binafsi kufanya kazi.
Aidha
inaelezwa kuwa pindi watumishi wa umma wanapokuwa na elimu nzuri nchi husika
zinakuwa na uwezo wa kukusanya kodi ya
mapato. Uhamasishaji wa mapato ni moja ya changamoto kubwa kwenye uchumi
unaoendelea na ukiwa mkubwa ni lazima uchukuliwe kama alama ya uwezo wa kujenga taifa.
Uhusiano
katika ya vigezo vya elimu inayopatikana na kodi ya mapato inayokusanywa kwa
asilimia ya Pato la Ndani la Taifa (GDP) ni chanya miongoni mwa nchi nyingi.
Tafiti zinabainisha kuwa watumishi wa umma waliopata elimu nzuri wamekuwa na
ufanisi katika kusimamia kodi, kuhakikisha uwepo wa uadilifu, uelewa na
kuwezesha maendeleo kwenye sekta binafsi.
Wigo
mwingine wa ufanisi wa serikali ni katika kuangalia uwezo wa nchini katika kuunga mkono maendeleo, usimamizi na
uendeshaji wa soko binafsi kama vile sekta ya fedha za ndani ambazo baadaye
hugeuzwa na kutoa mchango muhimu katika
kukuza na kukua kwa uchumi.
Mwongozo
huo unabainisha kuwepo kwa mkondo hasi wa uhusiano wa kitakwimu na kiuchumi kati ya elimu na uongozi ukiwemo usimamizi na
ushindani ambapo inaelezwa kwamba nguvu kazi iliyo na elimu ya uongozi wa umma
inasaidia kukuza viwango vya sekta ya fedha za ndani na hivyo kuhuisha maendeleo
ya sekta binafsi na kukua kwa uchumi.
Elimu na taasisi
Hata hivyo
moja ya suala muhimu ni iwapo kiwango cha kupata elimu miongoni mwa wafanyakazi wa umma huwa ni
chimbuko la utawala bora au elimu ni matokeo ya kukua kwa taasisi.
Kama
taasisi ndio inakuza kiwango cha elimu inayopatikana, basi sera za umma lazima
ziangalie uimarishaji wa taasisi mahsusi ili kuhakikisha kuwa watumishi wa umma
walio na vipaji wanachaguliwa kujiunga
kwenye uongozi wa umma na hivyo mfumo wa elimu wa nchi kuwa umekuza
stadi zinazotambulika.
Kwenye
mada moja ya wataalamu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuhusu mchango wa taasisi kwenye kuimarisha
uchumi inabainisha kuwa uhusiano wa kawaida kati ya ubora wa mpangilio wa
kitaasisi kama vile kulenga kupunguza
athari za wawekezaji kuhamisha rasilimali na kipato cha sehemu kubwa ya nchi.
Kwa maana
hiyo kuna uhusiano mkubwa kati watumishi
wa umma walioelimika vizuri ndani ya sekta za umma na kiwango kikubwa cha
ustawi miongoni mwa jamii kwa ujumla.
Aidha
maana ya hali hiyo ni kwamba maamuzi yanayofanywa na watumishi wa umma walio na
vipaji huboresha ubora wa upatikanaji wa huduma na matokeo yake ni kukua kwa
uchumi.
Katika
mazingira ya aina hiyo ni kwamba wakati taasisi zikiwa imara kwenye sekta za
umma kunawezesha kupunguza kiwango cha utajiri ambao ungeibwa
na wafanyakazi wa umma ambao ni wabadhirifu jambo ambalo husababisha
wafanyakazi wabadhirifu kuondoka kwenye sekta za umma.
Wafanyakazi
hao huwa ni wanaoguswa na maslahi ya umma na hutoa huduma kwa umma kwa kuwa
wanakuwa na maarifa mazuri lakini pia
wakiwa wazuri kwenye kufanya maamuzi na hivyo kufikia hitimisho kuwa kiwango
kikubwa cha elimu alichopata mtumishi wa
umma kinahusiana na kiwango kidogo cha rushwa ndani taasisi.
Katika
hali hiyo inamaanisha kuwa kadri watumishi wa umma wanavyokuwa na maarifa zaidi
ndivyo kiwango cha utoaji wa huduma huwa bora pamoja na kuongezeka kukua kwa
uchumi.
Fedha
ambazo hutolewa kama motisha kwa watumishi huleta ustawi kwa jamii na hususani
inapotokea kwamba taasisi ni dhaifu. Kuwepo kwa programu za motisha kunaifanya sekta ya umma kuwa na mvuto kwa
umma kwa jumla na matokeo yake kuboreka
kwa huduma za umma na uchumi kukua.
Kwenye
msimamo wa sera ni kwamba ufanisi katika utendaji wa serikali unaweza
kupatikana na njia mojawapo ni kuimarisha
mfumo wa mahakama. Mfumo wa mahakama ulio na ufanisi ambao unatekeleza
sheria kwa haki unaweza kuwaondoa
watumishi kwenye kujaribu kuchezea sheria na mifumo ili kujitajirisha wenyewe kwa
kutumia mali za umma na hali kadhalika kusababisha watu binafsi kupambana na
rushwa sehemu yoyote yenye huduma za
umma.
Inapokuwepo
motisha husaidia kuwavuta watu walioelimika. Nchi mbalimbali duniani na hususan
kwenye uchumi unaoinukia ni muhimu kujikita kwenye mtazamo wa kuvutia watu
waliopata elimu nzuri kwenye utawala ili
kuboresha utoaji wa huduma na kukuza maendeleo ya uchumi.
Hali hiyo
ndio iliyowezesha nchi za Mashariki ya Mbali zikiwemo Malaysia na Singapore
kupiga hatua za haraka za maendeleo jambo lililowezesha sekta ya umma kuwa kuvutio kwa wafanyakazi bora ambao walitoa mchango mkubwa kwenye kukuza ubora
wa shughuli za serikali na mwishowe kuwa na uchumi mzuri ulio na
ufanisi.
Comments
Post a Comment