Featured Post

AFISA MIRADI UMOJA WA ULAYA AFANYA ZIARA SHINYANGA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WATOTO

Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union – EU) John Villier amefanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni mkoani Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto la Save The Children.
Ziara hiyo imeanza Jumatano Agosti 29,2018 kwa Afisa Miradi huyo kukutana na wadau wanaoshiriki katika kutekeleza mradi huo wakiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga, Shirika la Save The Children na Shirika la Agape Aids Control Programme (AACP) ambao kwa pamoja wanaendelea kushirikiana katika kufanikisha mradi huo.

Akiwa katika ziara yake, John Villier pia amekutana na wanafunzi wa shule ya Msingi Mwamashele iliyopo kata ya Mwamashele kupitia “Tuseme Club” pamoja na kikundi cha watu wazima katika kijiji cha Itilima kata ya Itilima halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambao hukutana na kujadili namna ya kukabiliana na mila na desturi kandamizi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Villier alieleza kufurahishwa na jinsi mradi huo wa kutokomeza mila na desturi kandamizi unavyotekelezwa kwani umesaidia kupunguza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.

“Nimefurahi kuona kazi kubwa inayofanywa na Save The Children na AGAPE kwa kuwa na ushirikiano wa karibu na serikali pamoja na jamii katika kupiga vita mila na desturi kandamizi ambazo zinasababisha watoto wakose haki zao na kushindwa kutimiza ndoto zao,naomba tuendelee kushirikiana zaidi ili kuwakomboa watoto wanaopewa mimba na kuolewa katika umri usiotakiwa”,aliongeza Villier.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa kufadhili mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Save The Children na kueleza kuwa kumekuwepo mafanikio makubwa akibainisha kuwa sasa jamii imebadilika na imeanza kuachana na mila na desturi kandamizi.

“Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi,Umoja wa Ulaya na Save The Children tunatambua mchango wenu,kwa kweli sasa mila na desturi potofu zimeanza kupungua katika baadhi ya maeneo,mafanikio haya yanatokana na nyinyi kuwa karibu na serikali na wadau wengine”,alieleza

Aidha alisema mradi huo umekuwa chachu kwa maafisa maendeleo ya jamii kuwajibika zaidi kwa kuyafikia maeneo ya pembezoni ambayo haikuwa rahisi kuyafikia na kuwapa elimu wananchi.

Naye Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali na wadau wote wa maendeleo katika kupiga vita mila na desturi potofu katika jamii.

NIMEKUWEKEA HAPA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI WAKATI WA ZIARA YA AFISA PROGRAMU WA UMOJA WA ULAYA JOHN VILLIER
Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifanya mazungumzo na viongozi wa Shirika la Save The Children katika ofisi za Shirika hilo Mjini Shinyanga leo Jumatano Agosti 29,2018 – Picha zote na Kadama Malunde – Malunde
Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akizungumza na viongozi wa Shirika la Save The Children na kuhoji masuala mbalimbali kuhusu Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni unaotekelezwa na Shirika la Save The Children kwa kushirikiana na Shirika la Agape Aids Control Programme (AACP) la Mjini Shinyanga wilaya ya Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akifafanua namna wanavyotekeleza mradi wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi katika mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akielezea namna jamii inavyoshirikishwa katika mradi huo ili kuufanya uonekane ni wa jamii na siyo wa shirika.
Katikati ni Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akielezea namna wanavyoshirikiana na shirika la AGAPE katika kutekeleza mradi wa Mila na Desturi Kandamizi katika mkoa wa Shinyanga. 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akizungumza katika kikao hicho na kubainisha kuwa serikali ya mkoa wa Shinyanga imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi mkoani Shinyanga.
Wa pili Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni ,Mary Zabron akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Hapa ni katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga : Kulia ni Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew.
Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifurahia jambo wakati akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew.
Wa pili kushoto ni Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akielezea lengo la ziara yake mkoani Shinyanga kwa Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew (katikati).
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew akielezea mchango unaotolewa na Umoja wa Ulaya na Shirika la Save The Children katika kutetea haki za watoto ikiwa ni pamoja na kupiga vita mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa ndoa na mimba za utotoni.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew akiwaomba wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya ndoa na mimba za utotoni.
Hapa ni katika Ofisi za Shirika la AGAPE Mjini Shinyanga : Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE John Myola akimwelezea Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier jinsi wanavyoshirikiana na shirika la Save The Children katika kutekeleza mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni mkoani Shinyanga.
Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za shirika la AGAPE.
Hapa ni katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu : Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akimtambulisha Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier. Katikati ni Mkurungezi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era.
Wa pili kushoto ni Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akieleza malengo ya ziara yake katika wilaya ya Kishapu.
Mkurungezi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akiushukuru Umoja wa Ulaya kwa kufadhili mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni ambao unatekelezwa na shirika la Save The Children kwa kushirikiana na shirika la AGAPE.
Ndani ya Ofisi ya Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Mwamashele wilayani Kishapu : Kushoto ni Afisa Miradi ‘Afisa Programu’ kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akiuliza swali kwa Mwalimu mku wa shule hiyo Justin Claud (wa kwanza kushoto) kuhusu changamoto zinazojitokeza kwenye ‘Tuseme Club’ ya wanafunzi wa shule hiyo. Jumla ya Tuseme Club 12 zipo katika shule 12 wilayani Kishapu. Klabu hizo zinasimamiwa na shirika la AGAPE kwa kushirikiana na Shirika la Save The Children.
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mwamashele ambao wanaunda ‘Tuseme Club’ wakicheza mchezo ikiwa ni sehemu ni ya kupeana elimu juu ya madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier na viongozi wa shirika la Save The Children wakishuhudia elimu iliyokuwa inatolewa na walimu wa shule ya msingi Mwamashele kwa Klabu ya wanafunzi ‘Tuseme Club’.
Kushoto ni Mwalimu Kalunde Majid akiendelea na kipindi kwa wanafunzi wa ‘Tuseme Club’.
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea darasani.
Wanafunzi wakionesha kwa vitendo kazi ya kuosha vyombo kuwa inafanywa na watu wa jinsi zote zote yaani kiume na kike na siyo kazi ya wanawake/wasichana tu.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni nchini ,Mary Zabron akiuliza swali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mwamashele.
Mwanafunzi akinyoosha mkono ili ajibu swali kuhusu madhara ya ndoa na mimba za utotoni.
Hapa ni katika kijiji cha Itilima kata ya Itilima wilayani Kishapu : Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akijitambulisha kwa kikundi cha wananchi wa rika mbalimbali katika kijiji cha Itilima waliokuwa wanaendelea na mdahalo kujadili namna ya kuondokana na mila na desturi kandamizi ili kupiga vita ndoa na mimba za utotoni. 
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier alisema alifarijika kuona namna wananchi wa kata ya Itilima walivyohamasika kujitoa kupiga vita mila na desturi kandamizi kwa watoto.
Wakazi wa Itilima wakiendelea na mdahalo kuhusu mila na desturi kandamizi.
Mdahalo unaendelea.
Mkazi wa Itilima akichangia hoja wakati wa mdahalo huo.
Wa pili kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni nchini ,Mary Zabron akiwaomba wananchi kuacha kufumbia macho mila na desturi zinazomkandamiza mtoto na kusababisha akose haki zake.
Mkazi wa Itilima Peter Mulwano ‘Mzee Goma’ akilishukuru shirika la Save The Children na AGAPE kuwafikia wananchi wa Kishapu kupitia mradi huo.
Afisa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni kutoka shirika la AGAPE, Peter Amani akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akiwataka wananchi kubadilika na kuachana na mila na desturi potofu zinachochangia kuwepo kwa mimba na ndoa za utotoni.

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Comments