Featured Post

ZIWA LENYE MAJI LAGUNDULIWA KATIKA SAYARI YA MARS


 
Ziwa la rangi ya kijani likiwa na mabaki ya chumvi pembezoni



WATAFITI wamepata ushahidi wa kwanza wa maji katika sayari ya Mars. Kile wanachoamini kuwa ziwa kiko katika eneo lenye barafu nyingi la kusini na lina ukubwa wa kilomita 20.

Utafiti wa awali ulipata ishara za maji yanayopita katika sakafu ya sayari hiyo, lakini hiyo ni ishara ya kwanza ya maji kuonekana katika sayari hiyo katika siku za hivi karibuni.
Maziwa yaliogunduliwa na Nasa yalionyesha kwamba maji yalikuwepo katika sakafu ya sayari hiyo katika siku za nyuma.
Hata hivyo, hali ya anga ya sayari hiyo ni baridi na hivyobasi kufanya maji yake kubadilika na kuganda.
Matokeo yake yanafurahisha kwa sababu wanasayansi wametafuta kwa muda mrefu ishara ya kuwepo kwa maji katika sayari ya Mars lakini hawakufanikiwa kupata ushahidi wowote.
Pia itawafurahisha wale wanaofanya utafiti wa kuwepo kwa uhai mbali na duniani-licha ya kwamba matokeo hayo hayajatoa ushahidi wowote wa kuwepo kwa viumbe.
Ugunduzi huo ulifanyika kwa kutumia kifaa chenye radar kilichokuwa ndani ya kituo cha anga cha Ulaya kwa jina Mars Express orbiter.

Ziwa hilo liko chini ya barafu kusini mwa eneo la barafu la Mars

"Pengine huenda sio ziwa kubwa sana , alisema Profesa Orosei kutoka taasisi ya maswala ya angani inayohusika na asili ya nyota na viumbe vyengine vilivyopo mbinguni', alimbaye ndiye aliyeongoza utafiti huo.
Kifaa cha Marsis hakikuweza kubaini upana wa maji hayo, lakini kundi hilo la watafiti linakadiria kuwa na upana usiopungua mita moja.
''Hii ina inathibitisha kuwepo kwa ziwa lenye maji , na sio maji yalioyeyuka yaliopo kati ya mwamba na barafu, kama ilivyo katika maeneo mengine ya barafu duniani'', aliongeza Profesa Orosei. 

Mchoro unaonyesha matokeo ya kifaa cha marsis Radar juu

Je ziwa hilo lilipatikana vipi?
Vifaa vyenye radar kama vile Marsis huchunguza sakafu ya sayari kwa kutuma mawimbi ya ishara na kuchunguza kile kitakachorudi.
Mstari mweupe uliopo juu ya picha unaonyesha mwanzo wa mkusanyiko wa maji yalioganda na kuwa barafu na vumbi.
Chini ya hilo, watafiti waligundua kitu kisicho cha kawaida yapata kilomita 1.5 chini ya barafu.
''Katika rangi ya samawati unaweza kuona kutoka chini ikilinganishwa na kutoka kwa sakafu. Hiki ni kitu kinachoonyesha wazi kwamba kuna ishara ya kuwepo kwa maji'' , alisema Profesa Orosei. 

Mchoro wa matokeo ya kifaa cha Marsis-unaonyesha rangi ya samawati chini ya sakafu ya Mars ikidhihirisha uwepo wa maji

Hii ina maana gani kwa Uhai?
Hakuna lolote la dhahiri bado.
Dkt. Manish Patel kutoka chuo kikuu cha Open University alielezea: Tulibaini tangu kitambo kwamba sakafu ya Mars haiwezi kuruhusu kuwepo kwa uhai kama tunavyoijua hivyobasi ugunduzi wowote wa maisha sasa unapatikana chini ya sakafu ya Mars.
Hapo ndipo tunapopata ulinzi dhidi ya mionzi hatari na viwango vya hali ya hewa vinavyoruhusu uhai.
Muhimu zaidi ni kwamba hilo linaruhusu maji yanayoweza kukimu uhai. Lengo la kutafuta maji hayo ni muhimu katika utafiti wa kutafuta uhai duniani.
Na huku matokeo hayo yakionyesha kuwepo kwa maji, hayathibtishi chochote zaidi ya hilo.
''Hatujakaribia kugundua uhai , Dkt Patel aliambia BBC, lakini kile kinachofanyika na matokeo hayo ni kutafuta eneo ambalo linaweza kukimu mahitaji ya uhai katika Mars''.
Nyuzi za joto za maji hayo na kemia zinaweza kusababisha matatizo kwa kiumbe chochote cha Mars.
''Ili maji hayo kusalia licha ya baridi iliopo, maji hayo huenda yana chumvi nyingi ndani yake. Huenda maji hayo yana chumvi nyingi zaidi kwa kiumbe chochote kuweza kutumia'' , alielezea Dkt Claire Cousins, mwanasayansi wa maswala ya angani kutoka chuo kikuu cha St Andrews, nchini Uingereza.

Je ni hatua gani inayofaa kuchukuliwa?
Huku uwepo wake ukitoa fursa nzuri kwa wale wanaotaka kujua iwapo kulikuwa na uwezekano wa kuwepo kwa uhai katika Mars , ziwa hilo ni sharti kufanyiwa uchunguzi zaidi.
''Kile kinachohitajika sasa ni kuhakikisha kuwa utafiti kama huo unafanyika kwengineko ili kutafuta ishara kama hizo na iwapo inawezekana maelezo mengine kuchunguzwa''.
''Huenda hii ni fursa nyengine kwa ujumbe wa Mars kwenda kuchimba maji hayo yaliopo chini ya sakafu ya sayari hiyo kama inavyofanyika katika maziwa mengine yaliopo katika maeneo ya baridi duniani kama vile eneo la Antarctica'', aliongezea.
Eeneo hilo limelinganishwa na Ziwa Vostok, ambalo liko kilomita 4 chini ya sakafu ya barafu ya Antarctic ice.

CHANZO: BBC

Comments