DAR
ES SALAAM, TANZANIA
RAIS
mstaafu wa Marekani Barack Obama amekuwa kwenye ziara barani Afrika ambapo
sehemu ya ziara hiyo imekuwa ya faragha na nyingine ya wazi.
Kuna mambo mengi sana
ambayo ameyatenda na kuyasema wakati wa ziara hiyo yake ya kwanza Afrika tangu
alipostaafu urais mapema mwaka jana.
Obama alianza ziara
yake kwa usiri mkubwa, mapumzikoni katika hifadhi ya taifa ya Serengeti nchini
Tanzania.
Picha zake akiwa
mbugani zilianza kuenezwa mitandaoni mwanzoni lakini hakukuwa na thibitisho
rasmi kwamba alikuwa nchini humo.
Kilichofahamika wazi
tu ni kwamba alitarajiwa kuwa nchini Kenya mnamo 15 Julai kukutana na Rais
Kenyatta na baadaye 16 Julai afike nyumbani kwa babake Kogelo, Siaya magharibi
mwa Kenya.
Serikali ya Tanzania
ilisalia kimya kuhusu uwepo wake Tanzania hadi pale alipoondoka nchini humo na
kutua jijini Nairobi.
Ni hapo ambapo Msemaji
Mkuu wa Serikali, kupitia mtandao wa Twitter alipakia picha mbili za Waziri wa
Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Augustine Mahiga akiwa na Bw Obama katika uwanja
wa ndege.
Ujumbe ulioambatana na
picha hizo ulikuwa: "Rais Mstaafu wa Marekani @BarackObama amehitimisha
mapumziko ya siku 8 pamoja na familia yake katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
nchini."
Fasiri ya ujumbe hiyo
ilikuwa kwamba picha hizo zilikuwa za wakati wa kumuaga baada yake kukamilisha
ziara yake ya siku nane nchini humo.
Obama alikuwa na mke
na watoto
"Amefurahi
sana kuja, yeye mkewe na watoto wake. Na amekuwa hapa nchini kwa siku nane.
Nilimpokea hapa, akaomba kwamba mapokezi haya yawe kimya kimya kwa sababu
angependa awe na faragha huko mbugani," alisema Dkt Mahiga kwenye video
fupi iliyopakiwa katika ukurasa wa Twitter wa msemaji wa serikali ya Tanzania.
Baadhi ya picha ambazo
zimekuwa zikienea mitandaoni zinamuonesha mke wa Obama, Michelle, akiwa pamoja
na mumewe.
Michelle hata hivyo
hakusafiri na mumewe Kenya na wala hakuonekana nchini Afrika Kusini.
Bw Obama alipozuru
Kenya akiwa rais mwaka 2015 pia hakuandamana na mkewe na watoto ingawa nchini
Tanzania mwaka 2013 alikuwa ameandamana na Michelle.
Badala ya kuingia
Kenya, Michelle na watoto wao Malia na Sasha walifululiza hadi Ulaya kuhudhuria
tamasha ya muziki ya Jay-Z na mke wake Beyonce jijini Paris, Ufaransa.
Michelle aliketi
karibu na mamake Beyonce, Tina Knowles Lawson, kwenye viti vya mbele wakati wa
tamasha hiyo in the front row - and even getting a quick onstage smile from
Jay-Z. Wakati mmoja alisimama kucheza akiwa na binti yake Sasha, ingawa hakuna
taarifa kumhusu Malia.
Familia
ya Jay-Z ambaye jina lake halisi ni Shawn Corey Carter na ya Obama zina urafiki
wa karibu. Barack Obama alishiriki kwenye sherehe ya kumuingiza Jay-Z kwenye
orodha ya watunzi nyimbo maarufu, Songwriters Hall of Fame , na kumweleza
rapa huyo kama "kitu halisi cha Marekani".
"Nafikiri mimi na
Bw Carter tunaelewana vyema," alisema. "hakuna mtu yeyote ambaye
alituona tukiwa vijana angetarajiwa tuwe hapa tulipo leo."
Zawadi ya Magufuli
"Nimemkabidhi
zawadi kutoka kwa mheshimiwa rais ambayo imechorwa na kijana wetu ambayo inaonyesha
wale nyumbu wanapovuka Mto Mara ambayo inaitwa The Great Migration , moja
ya maajabu ya dunia," alisema Dkt Mahiga.
Kwa
mujibu wa waziri huyo, Obama alisema picha hiyo itamkumbusha kitu adimu na
adhimu ambacho alikishuhudia mbugani.
Kiongozi huyo alisema
kwamba angependa kurejea na kwamba atawashawishi marafiki zake wafike pia
kutembea.
Kukutana na Kenyatta
na Odinga
Alipowasili nchini
Kenya, Obama alilakiwa na dada yake Auma Obama - ambaye ana uhusiano wa karibu
sana naye - pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali na mara baadaye akaelekea
ikulu ambapo alikutana na Rais Uhuru Kenyatta na naibu Rais William Ruto.
Kiongozi
huyo wa zamani wa Marekani baadaye alikutana na kiongozi wa upinzani Kenya
waziri mkuu wa zamani Raila Odinga katika inayoaminika kuwa mgahawa wa Villa
Rosa Kempinski katika mtaa wa Westland, Nairobi na huenda ndiko alikolala kabla
ya kuelekea Kogelo Jumatatu asubuhi.
Obama aikuwa amezuru
nchini Kenya mara tatu 1987, 1992 na 2015 wakati alipokuwa akihudumu kwa awamu
ya pili ya urais.
Kukumbuka mapokezi ya
nyumbani siku ya kwanza
Obama aliongoza
ufunguzi wa kituo cha vijana cha elimu kwa jina Sauti Kuu, ambacho kilianzishwa
na dada yake Auma Obama, kilichofufua kumbukumbu ya safari yake ya kwanza
kabisa nyumbani mwa baba yake akiwa na miaka 27.
Alisimulia "baada
ya kutua Nairobi nilipanda treni ya kasi ya chini sana kisha nikaliabiri basi
lililokuwa limebeba kuku na viazi vitamu kando yangu," aliongeza kuwa
alipanda gari la uchukuzi la umma lililokuwa limejaa watu kuliko basi kwenda
nyumbani mwa Mama Sarah Obama, bibi yake wa kambo.
Alisimulia jinsi
alivyooga nje na alivyomshika kuku kuwa kitoweo cha jioni alipohisi njaa wakati
akiwa ameenda kuzuru kaburi la baba yake.
Alizungumzia pia
ufisadi ambao umekithiri katika mataifa mengi ya Afrika na mivutano ya kisiasa.
Ujumbe mkuu kwa
Afrika na Dunia hotuba ya Mandela
Shughuli kuu zaidi ya
ziara ya Obama Afrika ilikuwa kutoa mhadhara wa Nelson Mandela kama sehemu ya
maadhimisho ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa rais huyo wa kwanza mweusi wa
Afrika Kusini ambaye alipigana vikali dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi
nchini humo.
Ilikuwa mara yake ya
kwanza kutoa hotuba kuu jukwaani duniani tangu alipoondoka madarakani mapema
mwaka jana na kukabidhi mamlaka kwa Rais Donald Trump.
Mandela Day is about taking action to change the world
for the better. In these young people, I see Madiba's example of persistence
and hope. They are poised to make this world more peaceful, more prosperous,
and more just. pic.twitter.com/GJDuOs1hkH
Haki
miliki ya picha
AFP Inakadiriwa watu
15,000 walihudhuria mhadhara huo
Obama alisema kwamba
Marekani changamoto dhidi ya utandawazi mwanzoni zilitoka kwa wanasiasa wa
mrengo wa kushoto na kisha zikaanza kutokea kwa wanasiasa wa mrengo wa kulia.
Alisema madhara ya
kudorora kwa uchumi wa dunia mwaka 2008 - na kutomakinika kwa wasomi na
watawala - vilizifanya ahadi zilizotolewa kwa watu kuwa hewa tu.
"Siasa za kuwatia
watu hofu na kutoridhika na kuwa na misimamo mikali zilianza kuwavutia watu. Na
siasa za aina hiyo sasa zinashika kasi," Obama amesema.
"Viongozi wenye
nguvu kuu kisiasa wameanza kuchipuka...wale walio mamlakani hujaribu kuhujumu
kila taasisi au utamaduni unaoipatia demokrasia maana," aliongeza.
Ubaguzi na Ufaransa
kushinda Kombe la Dunia
Katika mhadhara huo wa
Mandela,Bw Obama alisema hushangaa sana kwamba wakati huu ni lazima kwake
kuwakumbusha watu kuhusu kuwaheshimu watu wa rangi, asili, dini na wapenzi wa
jinsia moja.
Amesema
anashangazwa na hilo kwamba linafanyika miaka mingi baada ya Nelson Mandela
kuondoka gerezani.
"Inaonekana ni
kama tunaelekea kwa siasa za kukaripiana, mapambano ya kuhakikisha haki za
msingi bado hayakamilika kwa kweli. Ni lazima tuwe macho dhidi ya watu
wanaojaribu kujitukuza kwa kuwashusha hadhi wengine," amesema.
Barack Obama alisema
usawa katika jamii huwezesha vipaji vya kila mmoja kuifaa jamii.
"Itazame timu ya
taifa ya kandanda ya Ufaransa," amesema. "Si wote walionekana kama wa
asili ya zamani ya Ufaransa, lakini wote ni Wafaransa - ni Wafaransa."
Ufaransa walishinda
Kombe la Dunia Jumapili kwa mara ya pili katika miaka 20, wakiwa na kikosi
ambacho wengi wa wachezaji ni wahamiaji au wazazi wao walikuwa wahamiaji.
Vitabu sita anavyotaka
watu wasome kwa sasa
Obama huwa kawaida
anatoa ushauri kuhusu vitabu anavyovisoma, nyimbo anazozisikiliza na vitabu
ambavyo angependa watuwasome.
Ijumaa wiki iliyopita,
katika kilichoonekana pia kama njia ya kuficha alikokuwa, alidokeza kwamba
angefanya ziara Afrika na kutoa orodha ya vitabu vilivyoandikwa na Waafrika na
kuhusu Waafrika ambavyo angependa watu wavisome.
This week, I’m traveling to Africa for the first time
since I left office – a continent of wonderful diversity, thriving culture, and
remarkable stories. As I prepare for this trip, I wanted to share a list of
books that I’d recommend for summer reading: https://t.co/W4Jc0N23iy
Comments
Post a Comment