Featured Post

WAZIRI KIGWANGALLA AWAPA NOTISI YA SIKU 45 WALIOVAMIA PORI LA AKIBA KIJERESHI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Kijereshi na Meneja wa pori hilo, Dianna Chambi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Alitoa siku 45 kwa wananchi wote waliovamia kingo/bafa za hifadhi hiyo kuondoka kwa hiari yao. Kulia ni Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti, Johnson Msella.
Na Hamza Temba-Simiyu
.........................................................

*Atoa miezi mitatu kwa Muwekezaji kurudisha Serikalini hati miliki ya kipande cha ardhi kilichopo ndani ya Pori hilo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewapa siku 45 wananchi wanaoishi kinyume cha Sheria ndani ya kinga (bufer zone) za Pori la Akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu. 

Ametoa agizo hilo jana alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Baada ya kushuhudia makazi na shughuli nyingine za kibinadam ndani ya pori hilo, Dk. Kigwangalla aliamua kutoa agizo hilo na kusema kuwa sheria za uhifadhi wa wanyamapori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa kisheria pamoja na kingo zake (buffer zone) ambazo ni mita 500 kutoka kwenye mpaka halisi wa eneo la hifadhi.

"Mpaka itakapofika tarehe 31 mwezi ujao (Septemba) wananchi wote hawa wawe wameshaondoka eneo hili kwa hiari yao wenyewe, muwatangazie na mpime eneo hili vizuri muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka.

"Na ikifika tarehe 1 Septemba kama kuna watakaokuwa wamekaidi agizo hili, basi mfanye oparesheni maalum muwaondoe na msafishe kila kitu, ni lazima ifike mahali kila mmoja aheshimu sheria za nchi" alisema Dk. Kigwangalla kuuagiza uongozi wa pori hilo.

Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa muwekezaji wa hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp kurudisha kwa Kamishna wa Ardhi hati miliki ya kipande cha ardhi chenye ukubwa wa hecta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwakuwa ni batili.

Aimesema pori hilo lilianzishwa mwaka 1994 wakati muwekezaji huyo anadai kumilikishwa eneo hilo mwaka 1995 jambo ambalo haliwezekani mtu binafsi kupewa hati ya kumiliki eneo lililopo ndani ya eneo jingine tena hifadhi.

Aidha, amemtaka pia muwekezaji huyo kuheshimu sheria na taratibu za uwekezaji katika eneo hilo ikiwemo kulipa ada na tozo mbalimbali.
 
Pori la Akiba Kijereshi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 65.72 linasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na lilipandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba mwaka 1994 kwa Tangazo la Serikali Na. 215 la terehe 10 Juni, 1994 na hiyo ni kutokana na umuhimu wake kiuchumi na kiikolojia hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Dianna Chambi (wa pili) kuhusu wananchi waliovamia hifadhi hiyo alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.  
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua koki ya maji katika eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Logolambogo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipolitembelea Pori la Akiba Maswa jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alipowasili mkoani humo jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la kingo/bafa la Pori la Akiba Maswa ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli kilimo alipolitembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mbunge wa Itilima, Njaru Silanga na Meneja wa Pori hilo, Lusajo Masinde.

Comments