- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kujenga miundo mbinu ya barabara hasa za ndani kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika
kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa
ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. “Serikali
imetoa shilingi bilioni 6 kujenga barabara ya Rujewa – Ubaruku inajengwa
kwa kiwango cha lami”.
Makamu wa Rais ameipongeza kampuni ya
Kapunga Rice Project Ltd kwa kujenga kituo cha afya kitakacho hudumia
watu zaidi ya elfu kumi na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Aidha
Makamu wa Rais amesema migogoro yote itafanyiwa kazi kuhakikisha haki
inapatikana kwa kila mmoja.
Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la
Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed ameahidi kuwalipia deni la shilingi
milioni 800 wakulima wanaodaiwa deni waliokupa kununulia power tiler
. Mbunge huyo wa Mbarali amesema kuwa Serikali ya awamu imetoa shilingi
milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.
Akizungumza
na Wananchi wa Kapanga katika mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameahidi kutoa mifuko
200 kutoka kwenye Taasisi yake ya Tulia Trust kusaidia ujenzi wa Wodi ya
Wazazi katika kituo cha Kapunga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia mchele unaozalishwa na kampuni ya Kapunga Rice Project
Ltd, kulia ni Mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw. Nillard Chawdry akimpa
maelezo Makamu wa Rais namna wanavyotumia teknolojia ya kisasa katika
kukoboa na kufungasha mpunga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
akihutubia wananchi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika
kituo cha afya Kapunga,pichani kushoto ni Mkuu wa kampuni ya Kapunga
Rice Project Ltd Bw. Nillard Chawdry. Kituo hicho kimejengwa na Kapunga
Rice Project Ltd kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu 10 na kulaza
Comments
Post a Comment