- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano, Dkt. Leonard Chamuriho akishuka katika ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoanza rasmi shughuli zake rasmi leo Jumapili Julai 29, 2018 kwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro. Anayemlaki ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na baadhi ya Watendaji wengine wa Sekretarieti ya Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Anna Mghwira akisalimiana na mmoja wa Marubani wa ndege mpya ya
Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianza rasmi
kazi zake leo Jumapili Julai 29, 2018. Ndege hiyoitaanza kufanya safari zake katika mikoa mitatu ya Dar es
Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe akizungumza na Watendaji,
Watumishi na Wananchi mbalimbali waliohuduhuria katika hafla ya kuanza kazi kwa
ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoanza kazi zake leo
Jumapili Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkoa wa Mwanza John Mongella, na Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho akisalamiana
na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira muda mfupi baada ya kushuka katika
ndege ya Serikali ya Boeing 787-8 Dremaliner iliyoanza safari zake leo Jumapili
Julai 29, 2018. Ndege hiyo itaanza kufanya safari zake katika Mikoa mitatu ya
Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro.
Mhudumu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),
akitoa maelekezo kwa abiria waliopanda ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dremaliner
muda mfupi kabla ya kuondoka Jijini Dar es Salaam kuanza safari zake nchini kwa
kuanzia na Mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Mwanza na Dar es Salaam.
(PICHA
NA MAELEZO)
Comments
Post a Comment