Featured Post

NYOKA NA BUNDI WA KICHAWI WAPIGWA MARUFUKU KATIKA UCHAGUZI ZIMBABWE



HARARE, ZIMBABWE
ZAIDI ya raia milioni 5 wa Zimbabwe watapiga kura Julai 30 katika uchaguzi wa kihistoria. Lakini ni kitu gani kiachoufanya uchaguzi huu tofauti kutoka uchaguzi wa nyuma?

1) Uchaguzi wa kwanza ambao Mugabe hayupo
Tangu kuasisiwa kwa Zimbabwe mnamo 1980, ni mtu mmoja pekee aliyewahi kushinda uchaguzi kuliongoza taifa - Robert Mugabe. Alikuwa waziri mkuu mpaka pale mfumo wa urais ulipoidhinishwa mnamo 1987.

Lakini kiongozi huyo wa miaka 94 alitimuliwa uongozini mwaka jana na jeshi na wafuasi ndani ya chama chake waliokaisrishwa na hatua zilizoonekana kutoa nafasi kwa mkewe Grace Mugabe kumrithi uongozini.
Wiki kadhaa kabla ya mapinduzi hayo ya kijeshi Novemba, Mugabe alimfuta kazi naibu wake Emmerson Mnangagwa, na alionekana kusogea ili kutoa nafasi kwa mke wake ateuliwe kuichukua nafasi yake. 
Lakini yalikwisha kwa kutimuliwa kwake na Mnangagwa akaishia kuwa rais. Sasa ndiye mgombea wa urais wa Zanu-PF.
Na kuna mabadiliko kwa sasa katika namna ambayokampeni zinaendeshwa kwasababu vyama vyote vimefanikiwa kuandaa mikutano ya kisiasa na maandamano pasi kuingiliwa au kunyanyaswa tofuati na ilivyokuwa katika uchaguzi wa siku za nyuma. 
Waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi kutoka Ulaya na Marekani wamekaribishwa kwa mara ya kwanza tangu 2002.
Vyombo vya habari pia vimechangamka, Kuna maoni tofuati yanayotolewa - licha ya kwamba shirika la kitaifa la utangazaji bado linaonekana kutoa kauli ya chama tawala.

2) Orodha ndefu ya wagombea
Kuondoka kwa Robert Mugabe kumefungua fursa ya wengi kuingia katika siasa - na majina 23 yatajumuishwa katika orodha ya wagombea wa urais.
Vyama 55 vya kisiasa pia vinagombea katika uchaguzi wa ubunge. Wadadisi wanasema hili linadhihirisha uoga uliokuwepo wa rais wa zamani wakati wa utawala wake wa miaka 37.
Miongoni mwa wanoajaribu bahati yao wamerudi nyumbani kutoka uhamishoni kuanza upya azma zao kisiasa. Lakini wagombe awakuu wa urais ni Emmerson Mnangagwa wa chama tawala Zanu-PF na Nelson Chamisa wa muungano wa upinzani MDC Alliance.
Hata hivyo, kuna mzozo kuhusu karatasi ya upigaji kura iliyo na pande mbili, inayomfanya Mnangagwa aonekana juu katika upande wa pili. Upinzani unasema ni kwenda kiyume na sheria, lakini mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Priscilla Chigumba amesema haikuwezekana wagombea wote kuwa katika upande mmoja wa karatasi - kwasababu ingekuwa pana sana wakati mpiga kura atakapoikunja baada ya kupiga kura na hivyo haingeweza kuingia ndani ya sanduku.
"And you want to tell me @ZECzim is credible if this is what the ballot paper looks like and they say it was a cost cutting measure, dividing candidates equally on each s half would have saved that extra little penny? #Zimbabwe is a big joke #EnoughIsEnough #ElectionsZW pic.twitter.com/tqhLdtYNj2
    — #Hayipariyani (@MatricksDeCoder) 13 Julai 2018
Evan Mawarire hagombei katika uchaguzi wa urais, hatahivyo anawania kiti cha udiwani katika mji mkuu Harare. Mchungaji huyo alipata umaarufu kwa kuushutumu wazi utawalal wa Mugabe. Aliweka video katika mitandao akieleza hasira yake kuhusu hali ya maisha na uongozi nchini humo na kuwataka raia nchini wajivunie bendere ya taifa hilo na waitishe mageuzi.
Baad aya hapo aliandaa maandamano ya siku mbili mnamo Julai 2016 - maandamano yalio makubwa kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja - na alishtakiwa kwa kujaribu kuipindua serikali. Aliondoshewa mashtaka wiki moja baada ya Mugabe kuondoka madarakani.
3) Wapiga kura hewa
Tume ya uchaguzi Zimbabwe Electoral Commission (Zec) imeidhinisha mfumo wa kuwasajili wapiga kura kwa mfumo wa kunasa alama za vidole, ambao inasema umefanikiwa kuwatambua watu wanaojisajili zaidi ya mara moja.
Inasema mfumo huo mpya, ambao ulitoa fursa kwa kila mtu nchini kujisajili upya, unamaanisha kwamba sasa daftari la wapiga kura lipo 'safi' na halina wapiga kura 'hewa'.
Kwa jumla watu 5,635,706 wamesajiliwa - 238,409 chini ya kiwango kilichokuwepo mnamo 2013, liocha ya idadi jumla ya kuongezeka kwa 2% kwa idadi jumla ya watu kwa mwaka.
Katika siku za nyuma, njia moja iliyoshuhudiwa ya udanganyifu katika uchaguzi ni kutumia majina ya watu waliofariki katika daftari la wapiga kura.
Tume imekana tuhuma za hivi karibuni kwamba wapiga kura hewa takriban 250,000 wamefanikiwa kujumuishwa kwenye orodha.
Zec inasema mfumo huo mpya wa kuwatambua wapiga kura umeweza kutambua visa kama hivyo, na kwamba takriban watu 92,000 ambao walijisajili awali wametolewa kutokana na hitilafu tofuati.
Mashine hizo za kunasa alama za vidole hazitotumia siku ya kupiga kura, lakini tofuati na uchaguzi wa siku za nyuma, watu wataweza kupiga kura katika vituo vya kupiga kura walikojisajili tu. Na picha na kitambulisho zilizotumika kuwasajili ndizo zitakazotumika kuwatambua wakati wa upigaji kura.

4) 'Wanyama wa Uchawi' wapigwa marufuku
Tume ya uchaguzi imepiga marufuku mambo tofuati katika nembo za wagombea, wakiwemo wanyama na risasi - licha ya kwamba bunduki zinaruhusiwa.
Hii ndiyo orodha ya vitu vilivyopigwa marufuku kujumishwa katika nembo, kama ilivyoorodheshwa katika mtandao wa Zec: Duma, Tembo, Chui, Simba, Bundi, Swila, na Faru.
Hakuna ufafanuzi uliotolewa kuhusu kwanini hawaruhusiwi.
Chama tawala Zanu-PF kinatumia picha ya magofu makuu ya Zimbabwe kama nembo yake - jengo la mawe kutoka ufalme wa zamani uliopo kati ya miti miwili inayodhihirisha umoja.
Upinzani MDC ina picha ya mkono ulio wazi kudhihirisha uwazi.

5) Kupungua kwa chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
MKurugenzi wa shirika la kutetea wapenzi wa jinsia moja anasema kumepungua kwa kiwango kikubwa chuki dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsia moja, wakati wa kampeni Zimbabwe, eneo ambako uhusiano na hata ndoa za aina hiyo zimepigwa marufuku. Kwa wakati mmoja Mugabe alisema wapenzi wa jinsia moja 'wanashinda hata nguruwe na mbwa' na kudai kuwa mapenzi ya aina hiyo sio ya Kiafrika.
Wapenzi wa jinsia moja wanakabiliwa na unyanyapaa mkubwa Zimbabwe - imekuwa ni hatari kubwa kwa watu wa jamii hiyo kuishi kwa uwazi kuhusu hali zao na ni kutokana na hilo wengi wanaogopa kwenda hospitalini kupata matibabu wanaopougua.
Katika ishara nyingine kwamba huenda mitazamoa inabadilika, taasisi inayoratibu utoaji wa matibabu ya HIV na ukimwi nchini imetangaza kuwa inafungua vituo vitano kitafifa kuwahudumia wanaume walio katika uhusiano wa aina hiyo.
BBC

Comments