Featured Post

MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI AWAPOKEA WAMAREKANI JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa, Elibariki Kingu, akihutubia katika hafla ya kuwapokea viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri kutoka Marekani waliotembelea Zahanati ya Kanisa hilo ya Kijiji cha Msungue iliyopo Kata ya Sepuka mkoani Singida jana. Zahanati hiyo inasimamiwa na kanisa hilo Dayosisi  ya Kati.

 Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akimuonesha picha ya vitanda vya Hospitali vinavyo sambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), Mkurugenzi wa Uhusiano Kati ya Sinodi ya Kusini Mashariki ya Minessota na makanisa ya nje ya Marekani, Callemia Chatelaine. Kushoto ni Mganga wa zahanati hiyo.



 Mganga wa zahanati hiyo akiwaelekeza jambo wageni hao walipotembelea chumba cha maabara cha zahanati hiyo.



 Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akiwaelekeza jambo wageni hao eneo ilipofungwa mfumo wa maji katika zahanati hiyo.
 Muonekano wa meza kuu katika hafla hiyo.
 Wananchi wa Kijiji cha Sengue wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Sepuka, Juma Mghenyi akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Wageni hao wakifurahi ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikipigwa na wasanii kutoka kikundi cha umoja cha Kijiji cha Sengue.



 Mbunge Elibariki Kingu, akicheza sanjari na wasanii wa kikundi cha umoja cha Kijiji cha Sengue.
 Askofu Steve Delzar kutoka Sinodi ya Kusini Mashariki (Minessota) ya Makanisa ya nje ya Marekani, akicheza pamoja na wasanii wa kikundi cha Umoja cha Kijiji cha Sengue Kata ya Sepuka.
 Wasanii wa kikundi cha Umoja wakitoa burudani.


Viongozi wa chama, Kanisa la KKKT na Serikali wakiwa kwenye hafla hiyo.

Comments