Featured Post

KATIBU JUMUIYA YA WAZAZI CCM AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA UNYAMBWA MKOANI SINGIDA

 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Erasto Sima, akihutubia wakati akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Unyambwa, Abdulaziz Hamisi Labu (kushoto), katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata hiyo mkoani Singida. Uchaguzi mdogo utafanyika katika kata hiyo tarehe 12 mwezi ujao baada ya diwani wa awali kufariki dunia.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimnadi mgombea huyo.
 Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew Mwiru akimdani mgombea huyo.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kampeni.
 Madiwani wa wilaya hiyo wakimuombea kura mwenzao kwa wananchi.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa kampeni.
 Taswira ya meza kuu kwenye mkutano huo.
 Mke wa mgombea udiwani huyo, Farida Iddi akimuombea kura mume wake.
 Viongozi mbalimbali wa CCM na wanachama wao wakiserebuka katika mkutano huo wakati wa kumkaribisha Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Erasto Sima ili kuhutubia.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (katikati), akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru. Kulia ni Mkuu wa Wilaya mstaafu wa Wilaya ya Nchemba.
 Viongozi mbalimbali wa Kata hiyo wakitambulishwa.
 Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Abdulaziz Labu akijinadi.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akicheza sanjari na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Erasto Sima baada ya kwisha mkutano huo wa kampeni.
Makada wa CCM wakiserebuka na viongozi wao baada ya mkutano huo wa kampeni kumalizika.

Na Dotto Mwaibale, Singida
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Erasto Sima amewaomba wanaccm wa Kata ya Unyambwa mkoani Singida kuhakikisha wanamchagua Abdulazziz Labu kuwa Diwani wa Kata hiyo.

Sima ambaye alikuwa ni mgeni rasmi alitoa ombi hilo wakati akihutubia kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni ya mgombea udiwani huyo uliofanyika jana katika kata hiyo.

"Ndugu zangu wanaccm wenzangu msituangushe mchagueni Labu ili awaletee maendeleo katika kata yenu" alisema Sima.

Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akihutubia kwenye mkutano huo alisema atashirikiana na diwani huyo kuhakikisha changamoto ya maji iliyopo katika kata hiyo inapatiwa ufumbuzi.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini Lusia Mwiru aliwaomba wananchi na makada wa CCM wa Kata hiyo tarehe 12 mwezi ujao kumchagua Labu kuwa diwani ili ashirikiane na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kuwaletea maendeleo.

Kwa upande wake mgombea huyo aliomba kura kwa kuwaambia wananchi hao kuwa akichaguliwa atawafanyia mambo makubwa ya kuwaletea maendeleo akianzia pale alipoishia mtangulizi wake ambaye amefariki.


Comments