- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mazao ya michikichi yaliyokuwa
yakikamuliwa kuwa mafuta ya kula wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga
mkoani Kigoma kujionea kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta ya
mawese katika gereza hilo Julai 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojiwa na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, Kulia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni na kulia kwa
Waziri Mkuu ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba. (Picha na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeliteua Gereza la Kwitanga
lililopo wilayani Kigoma kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa zao la
michikichi nchini.
Hivyo ameuagiza uongozi wa gereza hilo
waongeze nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na
kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi na kupanda miche
mipya ya michikichi na kukata ya zamani. Waziri Mkuu ameyasema
hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati alipotembelea gereza hilo
akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufufua
zao la michikichi mkoani Kigoma.
Amesema Serikali imedhamiria
kwa dhati kufufua kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma, hivyo kila
mwananchi lazima awe na shamba la michikichi.Katia hatua nyingine,
Waziri Mkuu ameuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma Bw. Sabas Matolo
kuhakikisha Gereza la Kwitanga linawezeshwa kwa kuwa na zana bora na za
kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na vifaa vya kuvunia ili waweze
kuongeza uzalishaji wa mafuta.
Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Bw.
Matolo awahamishe askari ambao ni wataalamu wa kilimo wenye ujuzi wa
zao la michikichi kutoka kwenye Magereza mengine mkoani Kigoma na
kuwahamishia katika gereza la Kwitanga ili kuimarisha uzalishaji.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kitalu cha kuzalisha miche ya Michikichi
cha Asasi ya Seed Change katika kijiji cha Simbo kwenye jimbo la Kigoma
Vijijini Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo,
Alex Chetkovic.
Wananchi
wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza wakimshangilia Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati aliposimama kijijini hapa kuwasalimia Julai 29,
2018. Alikuwa njiani kwenda Uvinza kuendelea na ziara ya mkoa wa
Kigoma.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba
wilayani Uvinza alipokuwa safarini kwenda Uvinza akiwa katika ziara ya
mkoa wa Kigoma Julai 29, 2018.
Comments
Post a Comment