- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA ALOYCE NDELEIO
BIOTEKNOLOJIA asilia au za kitamaduni inamaanisha njia za
asili na zamani zilizotumiwa na viumbe hai kutengeneza bidhaa mpya au kuboresha iliyokuwepo.
Katika uhalisia wake zaidi ni kwamba chimbuko la njia hizo
linaweza kuonekana kwenye mifumo ya maisha ya binadamu tangu alipoanza kuhama kutoka uwindaji na ukukusanyaji wa
matunda kama chakula na kuzalisha mahitaji yake kupitia kilimo.
Binadamu akiwa ni mkulima aliweza kukusanya mimeapori na
kuanzisha kilimo chake na kuwa na mbegu nzuri kwa ajili ya kuotesha msimu wa
uliofuatia ambazo zilichaguliwa kutoka mazao yaliyopatikana msimu wa mavuno.
Jinsi binadamu alivyozidi kugundua aina mbalimbali za mimea
basi ndio wakati huo alianza kutafuta
mbegu zake na kuzikuza ili kupata mbegu bora ambazo zilitumika kwa miaka
kadhaa.
Mara nyingine mbegu hizo zilittumika kutoka kizazi kimoja
hadi kingine, aidha ni katika kipindi hicho binadamu aliweza kufahamu tabia
mbalimbali za mimea na jinsi inavyoweza
kuhimili aina kadhaa za magonjwa.
Katika bioteknolojia hizo za asili ndiko binadamu aliweza
kubaini ni aina ipi ya mbegu iliyo na
ladha nzuri na inayotoa mazao mengi.
Hali kama hiyo pia ilikuwepo kwa upande wa wanyama
waliowafuga, ambapo mbinu kama
zilizotumika kwenye mbegu za mimea zilitumika
kupata aina nzuri ya wanyama kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Karne zilizopita watu waligundua njia za usindikaji wa asili
ambao ulitokea katika seli zilizokuwa hai kwa bahati mbaya. Japo hawakuwa na
maelezo ya kisayansi kuhusu hatua hizo walitumia matokeo waliyokuwa wanayaona
katika maisha yao ndani ya kaya zao.
Kwa mfano waligundua chakula kilikuwa kinaweza kubadilika
ladha na hata viambatanisho vyake na kwamba inakuwa si rahisi kuharibika.
Kadhalika waligundua kuwa ipo haja ya kuvundisha unga wa
ngano, kuukanda kwa ajili ya kuoka mikate, zabibu zikavundishwa
na kuzalisha mvinyo na kupata siagi
kutoka kwenye maziwa.
Kufutia majaribio ya hapa na pale, na baadaye kuingia kwa
teknolojia ya juu, watu walijifunza kudhibiti hatua hizo na kutengeneza bidhaa
nyingi zinazotokana na bioteknolojia.
Maendeleo ya sayansi yaliwezesha kuhamishwa kwa teknolojia
nyingi zilizokuwa zinatumika majumbani
na kuziingiza katika matumizi na hivyo kugundua mbinu mpya.
Kwa hali hiyo baioteknolojia za asili ni pamoja na kuchagua
mbegu, kutafuta mbegu nzuri na hata kuvundisha baadhi ya mazao.
Bioteknolojia mpya
Bioteknolojia ya kisasa inahusisha mbinu kadhaa ambazo
zinajumuisha kwa makusudi matumizi ya
vinasaba, seli na tishu hai katika njia
zinazotabirika na zinazodhibitika kuleta mabadiliko katika muundo
wa vinasaba katika kuunda kiumbe au kutengeneza tishu mpya.
Mfano wa mbinu hizi ni pamoja na kuunganisha DNA au
uhandisi vinasaba, kuboresha tishu n.k.
Bioteknolojia ya kisasa ilianza mwaka 1953 baada ya
kugundulika kwa DNA (deoxyribonucleic acid) na jinsi mawasiliano ya vinasaba
yanavyotoka kizazi kimoja hadi kingine.
Ugunduzi huu uliwezekana kutokana na ugunduzi wa awali wa
vinasaba uliofanywa na Mwanasayansi Gregor Mendel, ambao uliweka misingi ya
mpito kutoka bioteknolojia ya asili na ya kisasa.
Aidha, uliwezesha kuzalisha mabadiliko yaliyotakiwa ndani ya
viumbe kwa kubadili moja kwa moja vinasaba kwa njia iliyodhibitiwa na
inayochukua muda mfupi ikilinganishwa na mbinu za asili.
Ugunduzi huo ulikuwa sanjari na kupanuka kwa teknolojia na
sayansi kama vile biokemia na
saikolojia, na hivyo kufungua uwezekano wa matumizi mapya ya biotekonolojia
ambayo yalikuwa hayafahamiki kwenye mifumo
ya asili.
Tofauti ya bioteknolojia
mpya na ya zamani
Kabla ya kugundulika kwa vinasaba na DNA mabadiliko ya
vinasaba ndani ya viumbe ikiwemo mimea. Kwa mfano mmea uliokuwa na muonekano wa
kufanana uliweza kupandikizwa kwenye mmea mwingine kwa matumaini kwamba kupitia
njia ya chavua tabia hiyo au ukuaji wake
ungehamishiwa kwenye machipukizi ya mimea mama.
Hata hivyo katika
bioteknolojia ya kisasa kufikia malengo tarajiwa ndani ya kiumbe hufanyika
katika kiwango cha kinasaba.
Kutokana na hali
hiyo kinasaba kilichokusudiwa
kwenye mabadiliko kinatambuliwa, kuhamishwa na
kupandikizwa kwenye seli za kiumbe ili kuzalisha mabadiliko ya kinasaba.
Kadhalika katika mbinu nyingine mpya za bioteknolojia ni
kama vile kuweka vinasaba kwenye joto
kubwa ili kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa katika muundo wa kinasaba au tishu
za mmea.
Katika hali hiyo kubadilisha mbegu ni mbinu ya bioteknolojia ambayo imekuwa
inatumika kuuweka mmea katika tabia mpya, ili ziweze kutumiwa baadaye kuendana na mabadiliko yanayokuwepo.
Matumizi ya bioteknolojia
Bioteknolojia ya kisasa ipo katika matumizi mengi kuliko
ilivyo kwa bioteknolojia ya asili. Kwa uhalisia ni kwamba bioteknolojia ya asili ililenga katika
mahitaji ya chakula na kilimo kwa
kutumia mbinu kama vile kuchagua mbegu
au kuziloweka.
Kukua kwa Sayansi na Teknolojia kumepanua mtazamo ambao
baioteknolojia inaweza kutumia kwa kuhusisha mazingira, afya ya binadamu na wanyama kama vile
maendeleo ya chanjo na dawa na kutambua vyanzo vya magonjwa; nishati
kama vile kuzalisha dizeli; misitu kama vile kuzalisha viuatilifu na
upandikizaji wa miti katika miti mingine na maeneo mengine.
Mbinu za
baioteknolojia
Kukua kwa Sayansi na Teknolojia kumeibua maendeleo ya
aina mpya ya mbinu za bioteknolojia ambazo zilikuwa hazipo
katika mbinu za asili za bioteknolojia.
Mfano bioteknolojia ya sasa inajumuisha mbinu kama vile
kuunganisha DNA sanjari na masuala ya kutengeneza vinasaba.
Miongoni mwa mbinu
zinazotumika katika bioteknolojia
za kisasa zimeanzishwa kutokana na matokeo ya kuongezeka kwa uelewa
wa vinasaba na viumbe wadogo. Mfano
bioteknolojia ya asili ya kuchagua mbegu
kutoka mimea inayofanana pindi inapochanganywa.
Hata hivyo kupitia teknolojia ya kuunganisha DNA ndani ya
bioteknolojia za kisasa, vinasaba vinaweza kuhamishwa kati ya
aina mbili zisizofanana, mfano
kati ya bakteria na binadamu.
Mbinu za kisasa pia kama vile kuunganisha DNA kumewezesha
kupatikana kwa bidhaa mpya kwa kiwango
kikubwa kuliko inavyowezekana katika mbinu za asili za bioteknolojia.
Muda na usahihi
Kugundulika kwa
muundo wa chembechembe za DNA na namna ambavyo habari za vinasaba
zinahamishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kumewezesha kuhamisha vinasaba, hivyo
tofauti zilizopo kati viumbe kwa kutumia teknolojia ya kisasa kunakuwa ni kwa kasi na
hutumia muda mfupi kuliko kutumia teknolojia za asili.
Japo sio lazima sana kwamba kila seli inayotumika katika
hatua mojawapo inajumuisha kuhamisha
kinasaba lakini ukweli ni kwamba uwezekano wa
kujumuisha seli na kinasaba kinachokusudiwa kwa
kiwango kikubwa inatumika kwa
kutumia mbinu mpya za baioteknolojia kuliko kutumia bioteknolojia za asilia.
Lakini kwa kutumia mbinu za asili itachukua muda wa vizazi
vingi na muda mwingi wa kuzalisha mimea na wanyama walio katika mkondo unaotakiwa miaka mingi kwani inakuwa ni kujaribu kwa
kubahatisha .
Uelewa wa vinasaba halisi unaweza kuhamishwa pamoja na
teknolojia za kisasa kumeweza kupunguza
muda unaotumika katika kupata matokeo kuliko ambavyo ingetumika katika mbinu asilia za
bioteknolojia.
Comments
Post a Comment