Featured Post

WAFANYAKAZI TPA TANGA WATOA MSAADA WA SIKUKUU YA IDDI KWA KAMBI YA WAZEE MWANZANGE


 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga Ally Senkole kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha Mwanzange Jijini Tanga ambapo walikabidhi vitu vyenye thamani ya sh.milioni 1.5

 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazee hao mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri
 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na vitu mbalimbali walivyonunua kabla ya kuwakabidhi wazee hao
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga Ally Senkole akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vitu hivyo
 sehemu ya vitu ambavyo vilikabidhiwa.

 Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5 kwa kituo cha wazee wasiojiweza kilichopo eneo la Mwanzange Jijini Tanga

Msaada wa vitu hivyo ni vyakula mbalimbali ambavyo vitatumika kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo halfa ya makabidhiano ilifanyika juzi kwenye kambi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Bandari ya Tanga Hassan Senkole alisema waliona ni busara kupunguza sehemu ya mapato yao katika mwezi mtukufu wa ramadhani kuwasaidia wazee hao.

Alisema waliamua kutoa msaada huo ili kuwa sehemu ya jamii iliyowasaidia wazee hao katika sikukuu ya Eid EL Fitri ili nao waweze kusheherekea sikukuu hiyo bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile.

Comments